1/28/2019

Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

1. Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu" (LAW. 11:45).
"Na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana" (EBR. 12:14).
"Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho" (YN. 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwena Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na uonekano wa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendeleaa na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupuwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.
kutoka kwa "Kuhusu Majina na Utambulisho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivyo, hata kama sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote, na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndio maana Mungu Anasema, "Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu." Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani, hiyo ndiyo sababu Mungu Alijiandaa tena kujihatarisha kuja katika mwili.
kutoka kwa "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani ilimlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi, lakini pia ilimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.
kutoka kwa "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa hivyo, Mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado ni ya dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo atakapotwaliwa na Mungu na kutakaswa. Lingine lisipofanywa ila kukemea mapepo katika mwanadamu na kumkomboa, huko ni kumshika tu kutoka kwa mikono ya Shetani na kumrudisha kwa Mungu. Hata hivyo, hajafanywa msafi ama kubadilishwa na Mungu, anabaki mpotovu. Ndani ya mwanadamu bado kuna uchafu, pingamizi na uasi; mwanadamu amerudi tu kwa Mungu kupitia kwa ukombozi, lakini mwanadamu hana maarifa kumhusu na bado anamkataa na kumsaliti Mungu. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama ilivyo kazi ya wokovu imegawanywa katika awamu tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya shetani vimegawanywa katika awamu tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu sio jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika awamu moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika awamu na vipindi, na vita vya kupigana na Shetani vinaambatana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. … Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, awamu tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika awamu tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizika kupitia kuzawadia mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu awe kamili. Kama jambo la kweli, vita na Shetani sio kuchukua silaha dhidi ya Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kuwa na ushahidi wa Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Awamu ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni awamu ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa utawala wa Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na mwanadamu kamwe hangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilika kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu wa usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha kazi yote ya Mungu ya usimamizi, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, ambayo ni kusema kuwa mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kuwa katika mateka ya Shetani. Shetani anashindwa kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye amechukuliwa mateka, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu ameachiliwa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, baada ya kuwa kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
kutoka kwa "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mpango wa miaka elfu sita umegawawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Alioyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, "Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni." Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na kwamba tu ile ya Enzi ya Neema ndiyo iliyofanywa, mwanadamu angefahamu tu kwamba Mungu Anakomboa mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengelele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Mungu kukamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria, na kukamilika kwa kazi Yake ya ukombozi haionyeshi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema imefika mwisho, lakini huwezi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni