1/27/2019

Nyimbo za Injili "Anga Hapa ni Samawati Sana"


Nyimbo za Injili "Anga Hapa ni Samawati Sana" | The Kingdom of God Has Already Descended


I
Aa ... hii hapa anga,
oh ... anga iliyo tofauti sana!
Harufu ya kupendeza inasambazwa kote kwenye nchi, na hewa ni safi.
Mwenyezi Mungu alikuwa mwili na anaishi miongoni mwetu,
Akionyesha ukweli na kuanza hukumu ya siku za mwisho.
Maneno ya Mungu yanaweka wazi ukweli wa upotovu wetu,
tunatakaswa na kukamilishwa na kila aina ya jaribio na usafishaji.
Tunayaaga maisha yetu maovu na kubadilisha sura yetu ya zamani kuwa sura mpya.
Tunatenda na kuzungumza kwa maadili na kuruhusu maneno ya Mungu yatawale.
Moto wa upendo wetu kwa Mungu unawashwa mioyoni mwetu.
Tunasambaza maneno ya Mungu, kumshuhudia, na kusambaza injili ya ufalme.
Tunajitolea nafsi yetu yote kumridhisha Mungu, na tuko tayari kuteseka maumivu yoyote.
Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu kwa kubadilisha jaala yetu.
Tunaishi maisha mapya na tunakaribisha kesho mpya kabisa!

II
Ndugu wanapokutana pamoja, furaha inaonyesha kwenye nyuso zao.
Tunasoma maneno ya Mungu na kushirikiana ukweli, tunaungana katika upendo wa Mungu.
Sisi ni watu waaminifu, safi na wazi, hakuna ubaguzi kati yetu.
Tunaishi kwa ukweli, tukipendana, tukijifunza kutoka kwa nguvu za kila mmoja na kurekebisha upungufu wetu.
Kwa akili moja tunatimiza wajibu wetu na kutoa dhabihu yetu.
Katika njia ya kwenda katika ufalme, maneno ya Mungu hutuongoza kupita dhiki na taabu.
Maneno ya Mungu hufunua uweza Wake, na hushinda na kufanya kundi la washindi.
Wateule wa Mungu kutoka katika mataifa yote wanarudi mbele ya Mungu.
Watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu na kumwabudu milele.
Mapenzi ya Mungu yanatendwa duniani, ufalme wa Kristo umeonekana.
Haki na utakatifu wa Mungu vinadhihirika, mbingu na dunia zinafanywa upya.
Watu wa ufalme wanamwogopa Mungu na kuepuka mabaya, na wanaishi katika nuru.
Watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu na kumwabudu milele.
Mapenzi ya Mungu yanatendwa duniani, ufalme wa Kristo umeonekana.
Haki na utakatifu wa Mungu vinadhihirika, mbingu na dunia zinafanywa upya.
Watu wa ufalme wanamwogopa Mungu na kuepuka mabaya, na wanaishi katika nuru.
Ee, we … hii ni anga,
oh ... anga iliyo tofauti sana!

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya
Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni