Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maombi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maombi. Onyesha machapisho yote

10/29/2017

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

    Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

10/28/2017

Ni Wale tu Wanaolenga Vitendo Ndio Wanaweza Kufanywa kuwa Watimilifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu,
Umeme wa Mashariki | Ni Wale tu Wanaolenga Vitendo Ndio Wanaweza Kufanywa kuwa Watimilifu
Katika siku za mwisho, Mungu alikuwa mwili ili kufanya kazi Anayopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja binafsi kufanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa lengo la kuwafanya watimilifu watu wale wanaopendeza roho Yake. Tangu uumbaji hadi leo Anafanya tu kazi hiyo katika siku za mwisho. Ni katika siku za mwisho tu ndipo Mungu alikuwa mwili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa kama hicho. Ingawa Anastahimili mateso ambayo watu wataona vigumu kustahimili, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa binadamu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango wake hauvurugwi hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake asilia.

10/24/2017

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

10/15/2017

Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,Yesu,Injili
Umeme wa Mashariki | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumaini kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atasamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Wanatamani Yesu Mwokozi Awe Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi Ambaye Anapendeka, wa kirafiki na heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu.

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Umeme wa Mashariki ,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Maneno ya  Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini. Ni juu yenu basi kuwasiliana ufahamu wenu kuhusu hizi mada.
Mnapaswa kuelewa kusudi la Mungu na ni lazima muijue asili ya binadamu kupitia hii miaka saba ya majaribu. Kwa hakika, kila sentensi ya Mungu ina kusudi Lake, ambamo mmefichwa ukweli. Bila kujali ni suala gani linafanyiwa ushirika, au ni ukweli gani unaoenyeshwa, ndani yake mna njia ambayo watu wanapaswa kupitia, matakwa ya Mungu kwa watu, na kusudi la Mungu kwa wanaomtafuta.

10/11/2017

Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Umeme wa Mashariki | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya
Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru "mizigo" ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo. Inaonekana kwamba unafanya tu kazi hiyo kwa kutimiza wajibu, daima ukiamini kwamba unapaswa kufuata njia yako mwenyewe bila kujali jinsi watu wengine walivyo, na kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali jinsi watu wengine walivyo. Hamna uwezo wa kugundua uwezo wa wengine, na hamuwezi kujichunguza. Njia yenu ya kupokea vitu ni yenye makosa sana.

10/08/2017

Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo.

10/06/2017

Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu

Umeme wa Mashariki | Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu
Umeme wa Mashariki | Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu

             Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu

Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli.

10/05/2017

Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?
Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?
Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu.

10/02/2017

Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu
Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusishaMungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake.