Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kuupata-ukweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kuupata-ukweli. Onyesha machapisho yote

2/01/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

   Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kristo

 Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

     Imesemwa “Yeye afuataye hadi mwisho ataokolewa,” lakini hili ni rahisi kuweka katika vitendo? Sio, na watu wengine hawawezi kufuata hadi mwisho. Pengine watakapokabiliwa na wakati wa majaribu, ama uchungu, ama jaribio, basi wanaweza kuanguka, na kutoweza kusonga mbele tena. Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu.