Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kuutafuta-ukweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kuutafuta-ukweli. Onyesha machapisho yote

2/05/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Utendaji (7)

Ubinadamu wenu ni wenye upungufu mno, hali yenu ya maisha ni ya chini na kushusha hadhi mno, hamna ubinadamu, na hamna utambuzi. Hiyo ndiyo maana mnahitaji kujiandaa na mambo ya ubinadamu. Kuwa na dhamiri , urazini, na utambuzi, kujua jinsi ya kuzungumza na kutazama vitu, kuwa makini kwa usafi, kutenda kama binadamu wa kawaida—vyote hivi ni ufundi ustadi wa ubinadamu wa kawaida. Mnapofanya hivi vizuri, ubinadamu wenu ni wa kiwango kinachohitajika. Kipengele kingine ni kujihami kwa ajili ya maisha yenu ya kiroho. Lazima mjue kazi yote ya Mungu duniani na muwe na uzoefu wa maneno Yake. Unapaswa kujua jinsi ya kutii mipangilio Yake, na jinsi ya kutimiza majukumu ya kiumbe aliyeumbwa.

2/01/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

   Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kristo

 Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

     Imesemwa “Yeye afuataye hadi mwisho ataokolewa,” lakini hili ni rahisi kuweka katika vitendo? Sio, na watu wengine hawawezi kufuata hadi mwisho. Pengine watakapokabiliwa na wakati wa majaribu, ama uchungu, ama jaribio, basi wanaweza kuanguka, na kutoweza kusonga mbele tena. Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu.