10/27/2017

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu. Hili litakufanya utii kikamilifu kazi ya Mungu, na hutakuwa na malalamiko, hutahukumu, au kuchambua, sembuse kutafiti. Zaidi ya hayo, nyote mtakuwa na uwezo wa kumtii Mungu hadi kifo, mkimruhusu Mungu awaongoze na kuwachinja kama kondoo, ili nyote muweze kuwa akina Petro wa miaka ya tisini, na muweze kumpenda Mungu kwa hali ya juu sana hata msalabani, bila malalamiko yoyote.

10/26/2017

Umeme wa Mashariki | Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele
Mwenyezi Mungu alisema, Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. 

10/25/2017

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?
Mwenyezi Mungu alisema : Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo.

10/24/2017

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu
Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa anajumuisha yote na tele zaidi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na tele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu.

10/22/2017

Umeme wa Mashariki | 5. Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mungu mwenye mwili Amekamilisha kazi ya "ujio wa siri wa Mwana wa Adamu" Aliyetabiriwa katika Biblia, na hivi karibuni Ataonekana kwa umma katika kila taifa na sehemu ulimwenguni. Watu wote katika kila taifa na sehemu walio na kiu cha kuonekana kwa Mungu watatarajia kuonekana kwa Mungu hadharani.

Umeme wa Mashariki | Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote
Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Uyahudi, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kwa kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi tu, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Wanaisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaokomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Wanaisraeli pekee, na si Mungu wa Wayahudi pekee;

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo utamjua Yesu Atakaporejea? Je, mtaelewa kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia wakati wa kurudi, na uaminifu wenu ni wa kusifika, na imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: wingu hili jeupe linaashiria nini?

Wimbo wa Injili | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Best Swahili Christian Worship Song

Kama Nisingeokolewa na Mungu


Kama mimi nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,

nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.

Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,

kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.

10/21/2017

Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme

Umeme wa Masharik,Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme
1. Mwanadamu hapasi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.
2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupasi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.
3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu. Sadaka hizi hazifai kufurahiwa na binadamu yeyote ila kasisi na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu pekee ndiye Anayeweza kumgawia kasisi sadaka hizi, na hakuna mwengine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi.

10/20/2017

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo
Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya ubinadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi ya miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Ubinadamu kabla ya kuumba ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaeleza moja kwa moja Yeye ni nani;

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana "Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu"



Ha … nyimbo ni nyingi na ngoma ni za madaha;

ulimwengu na miisho ya dunia zinakuwa bahari inayosisimka.

Ha … mbingu ni mpya na dunia ni mpya.

Eneo kubwa la ulimwengu limejaa kusifu; tunapiga ukelele na kuruka kwa shangwe.

Milima yajiunga na milima na maji mengi kujiunga na maji mengi, ndugu wote wa kiume na kike ni wandani.

Twamsifu Mungu bila kukoma. Viumbe wampenda Mungu,

wakija, mbele ya kiti chake cha enzi kwa furaha kuabudu pamoja.

Umeme wa MasharikiKazi | Kazi Katika Enzi ya Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa
Umeme wa MasharikiKazi | Katika Enzi ya Sheria
Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake. Israeli ndipo mahali ambapo Mungu Aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka kwenye vumbi la mahali hapo, Yehova Alimwumba mwanadamu; ndio msingi wa kazi Yake ya hapo ulimwenguni. Waisraeli, ambao ni kizazi cha Nuhu na Adamu, ndio waliokuwa msingi wa kazi ya Yehova ulimwenguni.