2/15/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,
3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
(Mat 18:12-14) Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi wale tisini na tisa, aende milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Na iwapo atapata kumwona, amini nawaambieni, anamfurahia huyo kondoo mmoja zaidi, kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni, kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.

2/14/2018

Upendo wa Mungu na wokovu | "Kutanafusi kwa Mwenye Uweza" Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho


Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake.

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

    Katika kazi yao, wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mambo mawili: Moja ni kufanya kazi kabisa kulingana na kanuni zilizowekwa masharti na mipangilio ya kazi. Wafanyakazi hawapaswi kukiuka kanuni hizi, wasifanye kazi kulingana na mawazo yao wenyewe, na siyo kulingana na mapenzi yao. Wanapaswa kuonyesha uhusiano kwa kazi ya familia ya Mungu, na kuweka maslahi ya familia ya Mungu kwanza katika kila kitu wakifanyacho. Jambo jingine pia ni muhimu, na ni kwamba, katika kila kitu wakifanyacho, kuzingatia kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, na kufanya kila kitu kwa ukali kulingana na neno la Mungu.

2/13/2018

Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuwachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Kwa maneno mengine, binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa hiyo, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani.

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)

Tangu watu waanze kuikanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu.

2/12/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni. Tena, Nimeishi miongoni mwa binadamu, Nimeuhisi uchungu ulioko katika ulimwengu wa binadamu, Nimeona kwa macho Yangu hali zote tofauti zilizopo miongoni mwa wanadamu.

21 Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

 21 Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

     Mwenyezi Mungu alisema, Kama huna uzoefu wa kitu, basi wewe hakika hutajua jinsi ya kukisimamia na utakisimamia vibaya. Hata kama unakisimamia, na ufikiri: “Mimi nimeeleza kiasi haya yote na nikasema mengi kulihusu. Wao pia wamelisikiza mara nyingi. Nimeongea sana kulihusu. Nafikiri yote ambayo nimeshiriki kuhusu tatizo hili kimsingi ni kweli, sivyo?” lakini kwa kweli, yote tu ni mafundisho, na wewe unatumia mafundisho kutatua tatizo. Mbona unasema ni mafundisho? Kila neno unalosema ni sahihi, lakini kile unachosema hakijaelekezwa kwa tatizo na hakifikii kiini cha tatizo hili–ambapo tatizo hili lipo, shida yake ni nini, kwa nini hawa watu wanaweza kufanya mambo kama hayo au ni hali gani imejitokeza ndani yao.

2/11/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
    Mwenyezi Mungu alisema, Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa katika kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wameamini katika Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa.
Kama ni maarifa au matendo halisi, wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo kwenye ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu.

Neno la Mwenyezi Mungu | 34 Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi

Neno la Mwenyezi Mungu  | 34  Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu. Je wewe hutenda vipi wakati watu walio chini yako wanakurai na kukupa sifa kwa matokeo unayozalisha katika kazi yako? Je wewe hutenda vipi wakati watu wanakupa mapendekezo? Je, wewe huomba mbele ya Mungu?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida

Kanisa la Mwenyezi Mungu,ndugu na dada,Wakristo wa China

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida

Watu wanapozidi kuwa wapokelevu wa maneno ya Mungu, ndivyo wanavyozidi kupata nuru na wanaendelea zaidi kufuatilia maarifa ya Mungu kwa njaa na kiu ya hali ya kuwa mwenye haki. Ni wale tu ambao wanapokea maneno ya Mungu wanaweza kuwa na matukio ya undani zaidi na yenye utajiri zaidi; ni wale tu ambao maisha yao yanakuwa ya kupendeza zaidi na zaidi. Kila mtu ambaye anafuatilia uzima lazima ashughulikie haya kana kwamba ni kazi yake, na ni sharti awe na hisia kuwa hawezi kuishi bila Mungu, na hakuna mafanikio yoyote bila Mungu, na kila kitu ni ubatili bila Mungu.

2/10/2018

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho "Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote



Mwenyezi Mungu alisema, "Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga."

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kumfuata Mungu

neno la Mwenyezi Mungu | Je, ushawishi wa giza ni nini?

Ushawishi wa giza ni utumwa wa Shetani, ni ushawishi wa Shetani, na ni ushawishi ambao una hali ya kifo.
Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako kwa Mungu kikamilifu, katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa ya Mungu, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya uangalizi na ulinzi wa Mungu.

2/09/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa
imani katika Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Nane

     Kufuatana na sifa za asili za wanadamu, yaani, uso halisi wa wanadamu, kuweza kuendelea hadi sasa hakujakuwa jambo rahisi kweli, na ni kwa njia hii tu ndio nguvu kuu ya Mungu imekuwa dhahiri. Kutegemea kiini cha mwili pamoja na upotovu wa joka kuu jekundu hadi sasa, isingekuwa uongozi wa Roho wa Mungu, mwanadamu angewezaje kusimama leo? Mwanadamu hastahili kuja mbele ya Mungu, lakini Anawapenda wanadamu kwa ajili ya usimamizi Wake na ili kazi Yake kuu iweze kufanikishwa kabla ya muda mrefu sana. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kulipa upendo wa Mungu kwa wanadamu katika maisha yao yote.