4/17/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Lazima muwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, kuweza kula na kunywa maneno ya Mungu ninyi wenyewe, kupitia maneno ya Mungu ninyi wenyewe, na kuishi maisha ya kiroho ya kawaida bila uongozi wa wengine; lazima muweze kuyategemea maneno ya Mungu ya leo ili kuishi, kuingia katika uzoefu wa kweli, na kuona kwa hakika. Ni wakati huo tu ndipo mtaweza kusimama imara. Leo, watu wengi hawaelewi kikamilifu majonzi na majaribio ya siku za usoni. Katika siku za usoni, watu wengine watapitia majonzi, na wengine watapitia adhabu. Adhabu hii itakuwa kali zaidi; itakuwa ni kuwasili kwa ukweli. Leo, yote unayopitia, kufanya, na kuonyesha yanaweka msingi wa majaribio ya siku za usoni, na kwa kiwango cha chini mno, lazima uweze kuishi kwa kujitegemea.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (8)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (8)

Mwenyezi Mungu alisema, Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na Shetani; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo ya ni namna gani maisha na uzoefu wa mwanadamu ni ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, wanapokuwa wameamshwa kutoka kwa ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika.

4/16/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 12

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 12

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya. Tena, ni kama wanyama wakitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu wakikimbilia usalama katika mapango ya milimani; ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama;

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriwa na Yohana ilisikika kotekote katika nchi, hivyo ilienea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa Uyahudi, na kila mtu alimwita nabii. Wakati huo, Mfalme Herode alitamani kumuua Yohana, lakini hakuthubutu, kwani watu walimheshimu sana Yohana, na Herode aliogopa kwamba kama angemuua Yohana wangemuasi. Kazi iliyofanywa na Yohana ilikita mizizi miongoni mwa watu wa kawaida, na aliwafanya Wayahudi kuwa waumini. Kwa miaka saba alimwandalia Yesu njia, mpaka wakati ambapo Yesu alianza kutekeleza huduma Yake.

4/15/2018

Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo

Mwenyezi Mungu alisema, Ndani ya familia ya Mungu, kuna imani kadhaa tofauti katika Mungu; imani hizi tofauti lazima zitambulishwe ili kuona wewe ni wa gani.
Na imani ya aina ya kwanza, ambayo pia ni aina bora zaidi, mtu huyo ana uwezo wa kuyaamini maneno ya Mungu katika vitu vyote; ana uwezo wa kukubali ufichuzi wote wa Mungu, ushugulikiaji, na upogoaji; yeye ni mwagalifu kwa mapenzi ya Mungu, hupenda, ni mwaminifu kwa, na humwabudu Mungu, na ako tayari kutenda ukweli. Imani kama hiyo huzaa maisha, na inawezesha mtu kupata mabadiliko katika tabia na kupatwa na Mungu.
Na imani ya aina ya pili, mtu huyo anamwamini Mungu kwa kiasi, lakini pia ni mwenye tuhumu kwa kiasi.

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu🎬🎬

Christian Music Video Swahili "Hadithi ya Xiaozhen"(3): Wakiacha Wema na Kufuata Uovu

⭐⭐⭐🎼🎼❤️❤️*******^^*********^^*********^^*******❤️❤️🎼🎼👇👇👇

Katika ulimwengu huu wa mioyo mibaya ambapo pesa ni mfalme, ni machaguo yapi ambayo Xiaozhen aliye safi na mzuri aliyafanya, ya maisha na ya kuendelea kuishi …
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.

4/14/2018

Swahili Gospel Song | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo


Swahili Gospel Song | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo

🌺🌺🌺****************🎻🎻**************🎙️🎙️*******************🎼🎼
😇😇*******************💓💓****************🎧🎧
Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini.
Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza.
Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako, 
nina amani kabisa.
Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu.
Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako.
Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako.
Na bado Hunitendei kulingana na dhambi 
zangu lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu.

4/13/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mwenyezi mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesha ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea. Labda hii ni hali moja ambayo kwayo wanadamu hushirikiana na Mungu, ni ushirikiano usiokusudiwa wa mwanadamu na Mungu, ili utekelezaji huu unaoelekezwa na Mungu uwe wa kupendeza na wenye uhai, dhahiri sana.

Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake. Leo ni kwa sababu tu ya kutiwa moyo na Mungu na fadhili Zake ndio watu wamepokea usafishaji wa maneno Yake.

4/12/2018

Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

    12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake
(Yohana 20:26-29) Na baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwa ndani tena, na Tomaso pamoja nao: Kisha akaja Yesu, na milango imefungwa, na akasimama katikati, kisha akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Weka hapa kidole chako, na utazame mikono yangu; na ulete mkono wako uuweke ubavuni mwangu, na usiwe asiyeamini, bali uwe aaminiye. Naye Tomaso akajibu akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Tomaso, kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wanayo wale ambao hawajaona, ilhali wameamini.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Yesu

   
(Yohana 21:16-17) Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yona, je, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana; wewe unajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha kondoo wangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni, mwana wa Yona, je, unanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, je, unanipenda? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua mambo yote; wewe unajua ya kwamba nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.

Mungu Kuja Duniani na Kuwa Sadaka ya Dhambi

Kuja kwa Bwana Yesu hakumalizi tu enzi nzee iliyofungwa na sheria, na kuwaleta wanadamu kwa enzi mpya, lakini pia kunaboresha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kunaashiria mwanzo mpya, hatua mpya ya kuanzia, kwa kazi ya Mungu ya usimamizi miongoni mwa wanadamu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu

~~~~~~~~~~~~~~                                    ~~~~~~~~~~~~~~

×××××××××××××××××××

👇👇🌺🌺🌺👇👇🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺👇👇🌺🌺🌺👇👇🌺🌺🌺

Mwenyezi Mungu alisema, Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilielezewa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake.

4/11/2018

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”


1. Tangu watu waanze kukanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mwenyezi mungu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Utakatifu wa Mungu (III)

    Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Anatumia maarifa, sayansi, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii kutupotosha.) Sahihi, hii ndiyo ilikuwa mada kuu tuliyojadili wakati uliopita.