9/08/2018

"Imani katika Mungu" (6) - Imani ya Kweli katika Mungu Inamaanisha Nini?


Watu wengi wanaamini kwamba imani katika Mungu ni imani katika Biblia, na kwamba kumfanyia Bwana kazi kwa bidii ni uhalisi wa kuamini katika Mungu. Hakuna mtu katika ulimwengu wa dini ana uwezo wa kuelewa kabisa imani ya kweli katika Mungu ina maana gani. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Imani katika Mungu’ inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu.Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu sio sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini.

9/07/2018

Je, Kufanya Kazi kwa Bidii kwa ajili ya Bwana ni Uhalisi wa Imani katika Bwana?


Waumini wengi huamini kwamba mradi tunalilinda jina la Bwana, kuomba mara kwa mara, kusoma Biblia na kuwa na mikutano, na mradi sisi huyaacha vitu, hutumia rasilmali na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Bwana, basi hii ni imani ya kweli katika Bwana, na tutaweza kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Je, aina hii ya mtazamo ni sahihi? Wengi wataniita siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujafanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Katika Mapana na Marefu, Mwaminifu Hadi Kifo

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Katika Mapana na Marefu, Mwaminifu Hadi Kifo

Kutoka mbinguni hadi duniani, Akijificha katika mwili.
Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, katika upepo na mvua.
Ukachukua njia ngumu, ukafungua enzi mpya.
Kumkomboa mwanadamu, kutoa maisha Yako na kumwaga damu.
Upepo na mvua, miaka mingi sana. Kutelekezwa na kila mwanadamu.

9/06/2018

Hatimaye Nimemwona Mungu

Nilikuja katika uwepo Wako siku hiyo, moyo wangu ukiwa umejaa tamaa ya kina.
Macho yangu yalipojawa na machozi, mkono Wako ulinipapasa.
Majonzi na huzuni ulimwagika kutoka moyoni mwangu.
Maisha yangu ya awali yakipita mbele ya macho yangu; majonzi na uchungu vikigongana kwa kutanafusi.
Mungu, nakupa Wewe upendo wangu.

Imani katika Mungu" (4) - Je, Kuamini katika Biblia ni Sawa na Kuamini katika Bwana?


🌺🌺🌺🌺🌺🌺************💓💓💓💓💓💓

Imani katika Mungu" (4) - Je, Kuamini katika Biblia ni Sawa na Kuamini katika Bwana?

Watu wengi zaidi katika ulimwengu wa dini huamini kwamba Biblia ni kanuni ya Ukristo, kwamba mtu lazima ashikilie Biblia na kuweka msingi wa imani yake katika Bwana kwenye Biblia kabisa, na kwamba mtu hawezi kuitwa muumini akipotoka kutoka kwenye Biblia. Hivyo imani katika Bwana na imani katika Biblia ni sawa? Uhusiano kati ya Biblia na Bwana ni upi hasa? Bwana Yesu aliwakaripia Mafarisayo wakati fulani kwa maneno haya, "Tafuta katika maandiko;

9/05/2018

Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu.

Je, Kazi ya Mungu na Kuonekana kwa Mungu Kunaleta Nini katika Jamii ya Dini?



Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili na kuonekana ili kufanya kazi Yake, nguvu za uovu za Shetani hupinga na kulaani njia ya kweli kwa ghadhabu. Kwa njia hii, vita vinatokea ndani ya dunia ya kiroho ambavyo hugawanya na kufunua ulimwengu wa dini. Bwana Yesu alisema, “Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani: sikuja kuleta amani, bali upanga”(Mathayo 10:34). Wakati ambapo Bwana Yesu alionekana na kufanya kazi katika Enzi ya Neema, dini ya Kiyahudi iligawanyika katika vikundi vingi.

9/04/2018

Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

3. Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

Je, Njia Inayoshutumiwa na CCP na Miongoni mwa Watu wa Dini Siyo Njia ya kweli?🌻⭐



🙌🙌🙌🙌🙌🙌o(* ̄▽ ̄*)ブ@@@o(* ̄▽ ̄*)ブ🙌🙌🙌🙌🙌
👉👉👉👉👉👉👉👉-------^^^^^------👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Watu wengi hutafuta na kuchunguza njia ya kweli pasipo kutegemeza vitendo hivi katika maneno na kazi ya Mungu. Badala yake, wao hufuata mitindo ya ulimwengu wa dini na wanaamini kwamba kile ambacho serikali ya kikomunisti ya China na ulimwengu wa dini inalaani sio njia ya kweli—je, hii ni njia sahihi ya kuelekea? Biblia inasema, "dunia nzima hukaa ndani ya maovu" (1 Yohana 5:19).

9/03/2018

"Imani katika Mungu" (1) - Je, Utiifu kwa Wale Walio Madarakani Kweli ni Sawa na Utiifu kwa Mungu?🎬👇



Katika Biblia, Paulo alisema, "Acha kila nafsi itii mamlaka ya juu zaidi. Kwani hakuna mamlaka isipokuwa ya Mungu: mamlaka yaliyoko yameamriwa na Mungu. Yeyote yule anayepinga nguvu, anapinga amri ya Mungu: na yule anayepinga atapokea laana” (Warumi 13:1-2). Sisi waumini tunapaswa kuwatendea vipi wale walio madarakani? Je, utiifu kwa wale walio madarakani ni sawa na utiifu kwa Mungu kweli?

Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mfuate Mungu Katika Njia Yenye Mabonde

Kila ambacho nimewahi kuwa nacho, mimi hukitumia kwa Mungu.
Kila nilicho nacho nakitoa; najitoa mwenyewe Kwake.
Familia imenitelekeza; nimekashifiwa na dunia.
Basi, njia ya kumfuata Mungu ina mabonde, imejaa na mawe na miiba.
Nilitoa kila kitu changu ili kueneza ufalme wa Mungu mbali.

9/02/2018

Christian Video Swahili "Bahati na Bahati Mbaya" | Mshukuru Mungu kwa Neema Yake ya Ajabu🎬



💞💞💞💞💞💞💞💞  ~~~~~👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏
😇😇😇😇😇😇😇😇😇**************🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Kwa sababu yeye alitoka katika familia iliyo masikini, tangu akiwa na umri mdogo Du Juan alikusudia kutengeneza pesa nyingi sana apate kuishi maisha mazuri. Ili kufikia lengo hili, aliacha shule mapema zaidi kwenda kufanya kazi ya mikono, chochote angeweza kufanya ili apate pesa. Yeye hakulalamika wakati kazi ilikuwa ngumu na ya kuchokesha. Hata hivyo, yeye hakupata matokeo aliyotaka. Bila kujali jinsi alivyofanya kazi kwa bidii, hakuweza kupata yale maisha aliyojitakia mwenyewe.

Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu.