
Kijiji cha kishamba kilichojikokota kimaendeleo, wazazi wangu waliochoka kwa sababu ya kazi zao, maisha ya shida za kifedha … kumbukumbu hizi za huzuni zilitia alama kwa mawazo yangu machanga, zilikuwa ni hisia yangu ya kwanza ya “majaliwa.” Baada ya kuanza kwenda shule, mara ya kwanza nilipomsikia mwalimu wangu akisema kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” niliweka maneno haya imara mawazoni mwangu. Niliamini kuwa ingawa sikuweza kubadili ukweli kwamba nilizaliwa katika umaskini, ningeweza bado kubadili majaliwa yangu kwa kufanya kazi kwa bidii.