12/24/2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Upendo Safi Bila Dosari


I
Upendo ni hisia safi, safi bila dosari.
Tumia moyo, tumia moyo,
kupenda, kuhisi, kutunza.
Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga.
Tumia moyo, Tumia moyo,
kupenda, kuhisi, kutunza.
Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki,
hutazamii kupata kitu, cha malipo.
Ukipenda utajitolea, ukubali taabu,
kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

12/23/2018

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)


Mwenyezi Mungu anasema, "Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri.

12/22/2018

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

1. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake.

12/21/2018

Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?


Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alitabiri, "Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki" (Mathayo 25:6). "Tazama, nasimama mlangoni, na kubisha: mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja na yeye, na yeye pamoja na mimi" (Ufunuo 3:20). Kwa miaka elfu mbili iliyopita, waumini katika Bwana wamekuwa makini na wakingoja Bwana abishe mlango, kwa hivyo, Atabishaje mlango wa binadamu 2Atakaporudi?

12/20/2018

Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele


I
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele.
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Thamani na maana ya maneno Yake yanabainishwa na kiini chao,
sio kama mwanadamu anayakubali ama kuyatambua.
Hata kama hakuna mwanadamu ulimwenguni anayepokea maneno Yake,
thamani yao na usaidizi kwa mwanadamu hayapimiki.

12/19/2018

Swahili Christian Skit | "Baba Yangu, Mchungaji" | A Debate on the Bible in a Family


Swahili Christian Skit | "Baba Yangu, Mchungaji" | A Debate on the Bible in a Family

Chi Shou, mchungaji wa dini ambaye amekuwa muumini wa Bwana kwa miaka arubaini, daima ameshikilia mitazamo kwamba "maneno na kazi yote ya Bwana yako ndani ya Biblia," na kwamba "imani katika Bwana haiwezi kuacha Biblia, na kuiamini Biblia humaanisha kumwamini Bwana." Inapojulikana kwamba binti yake ameikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, anafanya mpango na mke wake kumkomesha. Katika siku hii, binti yao anarudi nyumbani kushuhudia injili ya kurudi kwa Bwana, na mjadala mkali, mcheshi, ilhali mzito wa familia unatokea ...

12/18/2018

Upendo na Kiini cha Mungu ni Vikarimu

Mungu anatoa kilicho bora zaidi, Anatoa upande Wake ulio mzuri.
Vitu vizuri, vitu vizuri zaidi, Anatoa.
I
Bila kufichua ama kuonyesha kuteseka Kwake.
Mungu, Anavumilia, Akingoja kwa kimya.
Sio baridi ama Aliyeganda, sio dalili ya unyonge.
Kiini cha Mungu na upendo Wake ni mkarimu kila wakati.

12/17/2018

Swahili Gospel Movie Segment "Mungu Anashikilia Ukuu Juu Ya Kila Kitu Katika Ulimweng"


Swahili Gospel Movie Segment "Mungu Anashikilia Ukuu Juu Ya Kila Kitu Katika Ulimweng"

Wanadamu wamekuwa wakitafuta majibu haya kwa miaka elfu kadhaa: Miili ya mbingu katika ulimwengu inawezaje kwendelea mbele kwa taratibu timilifu kama hiyo? Kwa nini vitu vyote vilivyo hai daima husogea kwa miviringo inayofuata kanuni zisizobadilika? Kwa nini watu huzaliwa, na halafu kwa nini sisi hufa? Ni nani kweli aliyeamua kanuni na sheria hizi zote? Ni nani kweli huutawala ulimwengu na vitu vyote? Sehemu hii ya ajabu kutoka kwa filamu ya Kikristo, "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu Ya Kila Kitu", itakuongoza ufikie kiini cha maswali haya na kufunua mafumbo yote haya.

Yaliyopendekezwa: Nyimbo za injili, Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

12/16/2018

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)


Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Xiaoxue, Malesia
Siku moja baada ya mlo mkuu wa siku, nilimfundisha mwanangu mvulana mkubwa jinsi ya kusoma Kichina—maneno rahisi tu, “Mbinguni, dunia, watu, na, dunia, baba, mama….” Nilimfundisha mara chache hasa, lakini bado hakuweza kuandika. Angeandika neno la kwanza na kisha kusahau lililofuata. Hasira ndani yangu ilipanda, na kunyakua rula iliyokuwa juu ya meza na kumgonga mara kadhaa. Nilimpigia kelele kwa sauti kubwa: “Wewe ni mpumbavu jinsi gani! Huwezi hata kujifunza maneno haya machache!”

12/15/2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini"

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika nyakati zilizopita, watu wengi walifuatilia kwa jitihada na fikira za mwanadamu na kwa ajili ya matumaini ya mwanadamu. Mambo haya hayatajadiliwa sasa. La muhimu ni kupata njia ya kutenda ambayo itawezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele ya Mungu na hatimaye kuvunja pingu za ushawishi wa Shetani, ili mpate kuwa wakubalika wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha duniani matakwa ya Mungu kwenu. Ni haya tu yanayoweza kutimiza mapenzi ya Mungu."

Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

12/14/2018

Nyimbo za kanisa | Kanuni za Kutafuta Njia ya Kweli

Nyimbo za kanisa | Kanuni za Kutafuta Njia ya Kweli

I
Ni kanuni gani za msingi zinazoonyesha njia ya kweli?
Ona kama Roho anafanya kazi, kwa ukweli unaonyeshwa;
ona ni nani anayeshuhudiwa, na anakuletea nini.
Kwani imani kwa Mungu inamaanisha imani kwa Roho wa Mungu.

12/13/2018

"Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (1) - Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Kazi ya Mungu


Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (1) - Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Kazi ya Mungu

Tunapokabiliana na ukiwa wa makanisa na giza iliyo katika roho, tunapaswa kuanza kutafuta nyayo za Bwana vipi? Tangu nyakati za kale njia ya kweli hupatwa mara kwa mara na mateso, na kuonekana na kazi ya Mungu wa kweli siku zote vitakumbana na ukandamizaji wa kikatili zaidi na mateso na upinzani wa hasira na hukumu ya ulimwengu wa kidini na Mungu serikali. Kama inavyosema katika Biblia, "dunia nzima hukaa ndani ya maovu" (1 Yohana 5:19). Hivyo, popote ambapo Mungu wa kweli huonekana kufanya kazi Yake bila shaka patakuwa ambapo sauti zinazomlaani zi kubwa zaidi. Hii ndiyo njia ya kutafuta nyayo za Bwana.

Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

12/12/2018

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu.