Maneno Husika ya Mungu:
Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.