10/11/2017

Upendo wa Mungu Huushinda Moyo wa Mwanadamu | "Wimbo wa Kifuasi cha Dhati" (Video Rasmi ya Muziki)

Wimbo wa Kifuasi cha Dhati

Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.

Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.

Hekima Yake, Uadilifu Wake, nayapenda yote.

Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana.

Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.

Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.

Hekima Yake, uadilifu Wake, nayapenda yote.

10/10/2017

Kuhusu Biblia (3)

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (3)
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (3)
Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa kibinadamu, na ufasiri wa ajabu wa kibinadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahahi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale.

10/09/2017

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana uwezo wa kujitenga na Mungu. Vilevile, Mungu Hajawahi kuwa na nia ya kujitenga na mwanadamu. Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu.

10/08/2017

Mbingu Mpya na Nchi Mpya | Tamthilia ya Jukwaa "Kwaya ya Injili ya Kichina 13"


 Kanisa la Mwenyezi Mungu| Tamthilia ya Jukwaa "Tamasha la Kwaya ya Kichina 13"

1. WANADAMU WAMEUPATA TENA UTAKATIFU WAO WALIOKUWA NAO AWALI

La … la … la … la …

Wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo (du ba du ba), haki ya Mungu na utakatifu wa Mungu vimeenda ugenini kote ulimwenguni (ba ba ba …), na binadamu wote wanavisifu bila kikomo. (Du … ba … ba la ba ba) Miji ya mbingu inacheka kwa furaha (du ba du ba), na falme za nchi zinacheza kwa shangwe (Ba ba ba …) Ni nani wakati huu ambaye haonyeshi furaha? Na ni nani wakati huu ambaye halii? (Du … ba … ba la ba ba) Nchi ni miliki ya mbingu, na mbingu imeungana na nchi. Mwanadamu ni ugwe unaounganisha mbingu na nchi, na kwa sababu ya utakatifu wake, kwa sababu ya mwanadamu kufanywa upya, mbingu haijafichwa tena kwa nchi, na nchi haiko kimya tena kwa mbingu. (Da la … da la da … oh …) Nyuso za ubinadamu zimezingirwa na, zimezingirwa na tabasamu za shukurani, na nyoyo zao zinadondokwa na utamu usiokuwa na kifani, utamu usiokuwa na kifani. (Da la … da la da da da la da) Mwanadamu hagombani na mwanadamu (beng …), wala binadamu kupigana wenyewe kwa wenyewe. (Beng …) Kunao wale ambao, katika mwanga wa Mungu, hawaishi kwa furaha na wenzao? Kunao wale ambao, katika siku za Mungu, hufedhehesha jina Lake?

Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo.

10/06/2017

Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu

Umeme wa Mashariki | Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu
Umeme wa Mashariki | Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu

             Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu

Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli.

10/05/2017

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kuficha Uhalifu"



       Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inayoonyesha kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Mkristo Mchina aliyeitwa Song Xiaolan–kifo ambacho kwacho polisi wa CCP walitoa maelezo yasiyopatana na yaliyogongana. Baada ya kuchunguza, familia ya Song iligundua kwamba polisi walikuwa wakidanganya wakati wote huo.

Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?
Umeme wa Mashariki | Je, Utatu Mtakatifu Upo?
Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu.

10/04/2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (2)

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (2)
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (2)
Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe).

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (1)

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (1)
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (1)
Biblia inapaswa kuangaliwaje kuhusiana na imani kwa Mungu? Hili ni swali muhimu sana. Kwa nini tunawasiliana swali hili? Kwa sababu wakati ujao utaeneza injili na kupanua kazi ya Enzi ya Ufalme, na haitoshi tu kuweza kuzungumza juu ya kazi ya Mungu leo. Ili kupanua kazi Yake, ni muhimu zaidi kwamba unakuwa na uwezo wa kubadilisha dhana za watu za dini ya kale na njia za kale za imani, na kuwaacha wakiwa wameshawishika kabisa—na kufikia katika hoja hiyo Biblia inahusishwa. Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni madhehebu maovu, na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia. Ni kusema kwamba, kama unasema unamwamini Bwana, basi ni lazima usome Biblia, unapaswa kula na kunywa Biblia, na nje ya Biblia hupaswi kuabudu kitabu kingine ambacho hakihusishi Biblia. Ikiwa utafanya hivyo, basi unamsalilti Mungu.

10/03/2017

Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana


Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana

I

Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaimba nyimbo za sifa kubwa Kwako.

Wewe hutuleta katika maisha ya ufalme.

Sisi watu wa ufalme tu katika karamu yako ya fahari,

tukifurahia maneno Yako, tukitakaswa upotovu wetu.

Neno Lako hutuongoza na sisi kukufuata kwa karibu.

Ni neema ya Mungu kwamba tabia yetu ya kishetani imetupiliwa mbali.

10/02/2017

Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu
Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kuishi Kwa Ajili Ya Ukweli Kwa Maana Unamwamini Mungu

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusishaMungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake.

10/01/2017

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Mhalifu ni Nani?"


Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Mhalifu ni Nani?"


Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.