1/13/2019

Swahili Gospel Video - Je, Kufanya Kazi Ngumu Kunamaanisha Tunafuata Mapenzi ya Baba wa Mbinguni?


Waumini wengine wa Bwana hufikiria kwamba yote tunayohitaji kufanya ni kuteseka na kulipa gharama ya kueneza injili ya Bwana, kubeba msalaba ili kumfuata Bwana, na kutenda unyenyekevu, subira na uvumilivu, na kwamba kwa kufanya mambo haya yote tunafuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, na pia wao huamini kwamba kila mara tukifuatilia imani yetu kwa njia hii, basi hatimaye tutaokolewa na Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Lakini je, ni sahihi kuwa na ufahamu wa aina hii na kutenda kwa njia hii? 

1/12/2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 103

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 103

Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami.

1/11/2019

Swahili Gospel Movie Clip (6) - Tofauti Kati ya Njia ya Toba na Njia ya Uzima wa Milele

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (6) - Tofauti Kati ya Njia ya Toba na Njia ya Uzima wa Milele

Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja. Bwana Yesu hufanya kazi ya ukombozi, Yeye anahubiri njia ya toba. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anafanya kazi ya hukumu ya kuwatakasa wanadamu, Yeye huleta njia ya uzima wa milele. Sasa, kama unataka kujua tofauti kati ya njia ya toba na njia ya uzima wa milele, tafadhali angalia hii video fupi.

1/10/2019

Umeme wa Mashariki | Sura ya 101

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Sura ya 101

Mwenyezi Mungu alisema, Sitakuwa mwenye huruma kwa yeyote anayeingilia usimamizi Wangu ama anayejaribu kuiharibu mipango Yangu. Kila mtu anapaswa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Ninayosema na lazima aelewe vizuri kile Ninachozungumzia. Kwa kuzingatia hali iliyopo, kila mtu anapaswa kujichunguza: Ni wajibu gani unaotekeleza? Unaishi kwa ajili Yangu, au unamtumikia Shetani? Je, kila moja ya matendo yako hutoka Kwangu, au hutoka kwa Shetani? Haya yote yapaswa kuwa dhahiri ili kuepuka kukosea amri Zangu za utawala na hivyo kupata ghadhabu Yangu.

1/09/2019

Ni Mungu tu Ana Njia ya Uzima

I
Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuwa nacho;
si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuipata kwa urahisi.
Kwani uzima unatoka tu kwa Mungu,
ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima,
ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima.

1/08/2019

"Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (5) - Ni Nani Anayempa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele?


Bwana Yesu alisema, "Lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa hatahisi kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujika katika uzima wa milele" (Yohana 4:14). Bwana Yesu ndiye chanzo cha maji hai ya uzima, Yeye ndiye njia ya uzima wa milele, lakini, kama ilivyoshudiwa na Umeme wa Mashariki, ni Kristo wa siku za mwisho pekee—Mwenyezi Mungu anaweza kuwapa watu njia ya uzima wa milele. Hivyo, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu wanatoka kwa chanzo kimoja? Je, kazi zao zinatekelezwa na Mungu mmoja? Kwa nini ni Kristo wa siku za mwisho pekee anayeweza kutupa njia ya uzima wa milele?

1/07/2019

Umeme wa Mashariki | Mabadiliko ya Kweli Humaanisha Nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Umeme wa Mashariki | Mabadiliko ya Kweli Humaanisha Nini?

Jinru    Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan
Wakati ndugu wa kiume au wa kike alipoonyesha dosari zangu au hakusikiza kauli yangu ama sikuhisi kushawishika au nilibishana nao. Nilijutia vitendo vyangu baadaye, lakini nilipokabiliwa na mambo haya, sikuweza kujizuia mwenyewe kuifichua tabia yangu potovu. Nilisumbuliwa na hili kwa kina, na nikafikiri: Kwa nini maneno ya wengine yanaweza kuniaibisha hadi kukasirika? Na kwa nini sijabadilika hata kidogo licha ya miaka minane ya kumfuata Mungu? Nilikuwa na wasiwasi na tena na tena nilimtafuta Mungu kwa jibu.

1/06/2019

Swahili Gospel Movie Clip (4) - Kwa nini Mungu Anatekeleza Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

Swahili Gospel Movie Clip (4) - Kwa nini Mungu Anatekeleza Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho?

Hata ingawa dhambi zetu husamehewa mara tunapokiri imani yetu katika Bwana, mara nyingi bado sisi hutenda dhambi. Hili ni tatizo ambalo huwakanganya waumini wote. Bila kujali tumeamini katika Bwana kwa miaka mingapi, na bila kujali jinsi tunavyotenda maneno ya Bwana au jinsi tunavyotegemea utashi wetu kujizuia, wakati wote bado hatuwezi kujiweka huru kutokana na udhibiti wa asili yetu ya dhambi.

1/05/2019

Umeme wa Mashariki | Sura ya 44

Umeme wa Mashariki | Sura ya 44

Mwenyezi Mungu alisema, Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe.

1/04/2019

Swahili Christian Video "Bwana Anakuja Kwa Namna Gani Hasa?" | The Son of Man Has Come to Earth


Katika siku za mwisho, hali ya moyo ya Wakristo wanaongoja kurudi kwa Bwana Yesu inakuwa kali sana, lakini ni kwa vipi, hasa, Bwana atarudi? Baadhi wanasema, "Bwana Yesu atakuja na mawingu." Wengine wanasema, "Unabii unaotabiri kurudi Kwake nao unasema, 'Tazama, mimi nakuja kama mwizi' (Ufu 16:15). 'Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki' (Luka 17:25). 'Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha' (Mat 25:6).

1/03/2019

Umeme wa Mashariki | Sura ya 100

Umeme wa Mashariki | Sura ya 100

Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu.

1/02/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?"


Mwenyezi Mungu anasema, "Mnamtamani na kumcha tu Mungu msiyemwona aliye mbinguni lakini hauna haja na Kristo Anayeishi duniani. Hii pia si ni ukosefu wa imani? Mnamtamani tu Mungu Aliyefanya kazi kitambo kile lakini hutaki kukumbana na Kristo wa leo. Hizi ndizo huwa 'imani' zilizochanganyika katika mioyo yenu isiyomwamini Kristo wa leo. Sikuchukulii kwa hali ya chini kwa maana ndani yako mna kutoamini kwingi, ndani yenu mna uchafu mwingi sana ambao lazima uchunguzwe kwa kina.

1/01/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Matendo Ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu


I
Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu,
na Anatawala vitu vyote kutoka juu.
Wakati huo huo,
Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia.
Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati,
kila hatua ya mwanadamu,
kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu
kama kiganja cha mkono Wake.