1/13/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 32 Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,hukumu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | 32  Ni Watu wa Aina Gani Watakaoadhibiwa

   Kukufuru na kashfa   Kukufuru na kashfa dhidi ya Mungu ni dhambi ambayo haitasamehewa kwa enzi hii na enzi ijayo na wale wanaofanya dhambi hii hawatazaliwa upya kamwe. Hili linamaanisha kwamba tabia ya Mungu haiwezi kuvumilia kosa la wanadamu. Watu wengine wanaweza kusema maneno yasiyofaa au maneno mabaya wakati hawaelewi, au wanapodanganywa, kuwekewa vikwazo, kudhibitiwa, au kukandamizwa na wengine. Lakini wanapokubali njia ya ukweli katika siku zijazo watajawa na majuto. Halafu wao hufanya matendo mazuri ya kutosha na wanaweza kupata mabadiliko na kufikia ufahamu, na kwa njia hii kosa lao la awali halitakumbukwa tena. Nyinyi mnapaswa kumjua Mungu kwa ukamilifu, nyinyi mnapaswa kujua ni kwa nani maneno hayo ya Mungu yanaelekezwa na muktadha wa maneno hayo, na hampaswi kutumia maneno ya Mungu bila taratibu maalum, wala kufafanua maneno ya Mungu kiholela. Watu ambao hawana uzoefu hawajilinganishi wenyewe dhidi ya maneno ya Mungu katika chochote. Wakati ambapo watu wenye uzoefu kidogo au ufahamu fulani huelekea kuwa na wepesi wa kuhisi zaidi. Wanaposikia maneno ya Mungu yenye kulaani, kudharau, kuchukia au kuondoa watu kabisa, kwa yote wanachukua dhima. Hili linaonyesha kwamba hawalielewi neno la Mungu, na daima humwelewa Mungu vibaya. Baadhi ya watu humhukumu Mungu kabla hawajasoma kitabu chochote, hawajafanya uchunguzi wowote, hawajasikia ushirika wowote wa wale ambao wanaelewa kazi mpya ya Mungu, au sembuse wamepatiwa nuru yoyote ya Roho Mtakatifu. Baadaye, mtu fulani huwahubiria injili na wao huikubali. Baadaye, wao huhisi kujuta kwa ajili ya jambo hili, nao hutubu. Halafu, wao wataangaliwa kulingana na tabia zao za siku za usoni. Baada ya wao kuamini katika Mungu, kama tabia zao hasa ni mbaya, na wakijifikiria kuwa kitu kisicho na dhamani, wakisema "Kwa vyovyote vile, nimesema maneno ya kukufuru na maneno mabaya kabla. Mungu ametangaza kwamba watu kama mimi watahukumiwa. Naam, maisha yangu yamekwisha," basi watu kama hao hakika wamekwisha. Kuhusu hali za watu, wengine waliwahi kupinga, wengine waliasi, wengine walizungumza maneno ya malalamiko, walijishughulisha na mienendo mibaya, walifanya vitendo dhidi ya kanisa au walifanya mambo yaliyoharibu familia ya Mungu. Matokeo yao yataamuliwa kwa kuzingatia asili yao na upana kamili wa tabia zao. Watu wengine ni waovu, wengine ni wajinga, wengine ni wapumbavu, na wengine ni wanyama. Watu wote ni tofauti. Watu wengine waovu wamemilikiwa na mapepo, wakati wengine ni wajumbe wa ibilisi Shetani. Kwa kuzingatia asili zao, baadhi yao hasa ni wabaya, baadhi ni wa wadanganyifu hasa, wengine hasa ni wenye tamaa ya fedha, wakati wengine ni wazinzi. Tabia ya kila mtu ni tofauti, hivyo kila mtu anapaswa kutazamwa kikamilifu kulingana na asili na tabia yake binafsi. Kwa kuzingatia mwili wa mwanadamu wa kufa, yeyote awaye, silika yake ni kuwa tu na hiari huru, kuwa na uwezo wa kufikiri tu juu ya mambo lakini sio kuwa na welekevu wa kuingilia moja kwa moja katika ulimwengu wa kiroho. Kama tu wakati unapoamini katika Mungu wa kweli na ungependa kukubali hatua hii ya kazi Yake mpya, lakini bila ya mtu yeyote kuihubiri injili kwako, na Roho Mtakatifu akifanya kazi tu, Akikupatia nuru na kukuongoza wewe mahali fulani tu, ni vigumu kwako kujua kile Mungu atakachofanikisha katika siku zijazo. Watu hawawezi kumwelewa Mungu, hawana welekevu huu. Watu hawana welekevu wa kuuelewa moja kwa moja ulimwengu wa kiroho, au kubaini kazi ya Mungu, sembuse kusema kwamba watamtumikia Mungu kwa hiari zaidi kama malaika. Isipokuwa Mungu awe amewashinda, Amewaokoa na kuwabadilisha watu, ama Amewanyunyizia na kuwaruzuku watu kwa vitu ambavyo vimetolewa na Mungu, watu hawawezi kuikubali kazi mpya. Mungu asipofanya kazi hii, watu hawatakuwa na jambo hili ndani yao, na hili linaamuliwa na silika ya mwanadamu. Kwa hiyo, Mimi ninaposikia habari kama vile watu kupinga au kuasi, Mimi huelekea kuwa na hasira sana, lakini tena, wakati Mimi ninapofikiria silika za mwanadamu, Mimi hulishughulikia jambo hili tofauti. Kwa hiyo, kazi yoyote iliyofanywa na Mungu imepimwa vyema. Mungu hujua nini cha kufanya na jinsi ya kukifanya. Kwa mambo hayo watu hawawezi kufanya kisilika, kwa hakika Yeye hawatawaacha wayafanye. Mungu humshughulikia kila mtu kulingana na usuli wakati huo, hali halisi, vitendo vya watu, utendaji na semi, na hali na mazingira watu walimo. Mungu hatawahi kamwe kumkosea mtu yeyote. Hii ndiyo hali ya haki ya Mungu. Kama unavyoona, Hawa alikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya alipodanganywa na nyoka. Lakini Bwana hakumshutumu, Yeye alimshutumu? Yeye hakusema: "Kwa nini unakula? Mimi nilikwambia usile, kwa nini bado unakula? Unapaswa kuwa na ufahamu na unapaswa kujua kwamba nyoka huongea tu kukushawishi. " Yeye hakusema hivi, wala Yeye hakumlaumu. Kwa kuwa Yeye aliwaumba watu, Yeye anajua silika za watu zilivyo, kile silika zao zimetengenezwa kwacho, ni kwa kiasi gani watu wanaweza kuzidhibiti, na kile ambacho watu wanaweza kufanya. Wakati Mungu anapomshughulikia mtu, Yeye anapochukua msimamo kuelekea kwa mtu—kama ni kudharau, kuchukia, au kuchukizwa—Yeye hufanya hivyo kulingana na ufahamu kamili wa muktadha wa maneno ya watu na hali zao. Kila mara watu hudhani kuwa Mungu ana Uungu pekee, Mungu ni mwenye haki na asiyeweza kukosewa. Wao hufikiri kuwa Yeye hana ubinadamu wowote, kuwa hafikirii matatizo ya watu, na Yeye hajiweki mahali pao; kwamba Mungu atawaadhibu watu mradi hawafuati ukweli na kwamba Yeye atakumbuka ikiwa mtu hupinga hata kidogo, na Atamwadhibu baadaye. Hivi kwa kweli sivyo ilivyo. Ikiwa unauelewa haki ya Mungu, kazi ya Mungu, na utendeaji wa Mungu kwa watu kwa njia hii, basi wewe umekosea sana. Msingi ambao Mungu hutumia kuwashughulikia watu ni usiofikirika kwa mtu. Mungu ni mwenye haki na kwa kweli Atawashawishi watu wote siku moja.

kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni