3/12/2018

πŸ“–πŸ“–Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tabia ya Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa vile sasa mumesikiliza kikao cha ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mumejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kushika, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo-upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu. Sehemu ile nyingine ni nini, hivyo basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.
Nimeteua sehemu mbili kutoka kwenye Biblia ambazo ningependa tushiriki pamoja kuhusu mada ya leo: Jambo la kwanza linahusu kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu, ambalo linaweza kupatikana kwenye Mwanzo 19:1-11 na Mwanzo 19:24-25; jambo la pili linahusu ukombozi wa Ninawi na Mungu, ambalo linaweza kupatikana kwenye kitabu cha Yona 1:1-2, kuongezea sura zile za tatu na nne za kitabu hiki. Ninashuku kwamba nyinyi nyote mnasubiri kusikia kile Nilicho nacho kuhusu sehemu hizi mbili. Kile Ninachosema hakiwezi kwenda kando na mada ya kutaka kumjua Mungu Mwenyewe na kujua hali Yake halisi, lakini ni nini kitakachokuwa zingatio la ushirika wa leo? Je, yupo yeyote kati yenu anayejua? Ni sehemu zipi za ushirika Wangu kuhusu “Mamlaka ya Mungu” ziliweza kuwavutia? Kwa nini Nilisema kwamba yule tu anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizo ndiye Mungu mwenyewe? Ni nini Nilichotaka kuelezea kwa kusema hivyo? Ni nini ambacho Nilipenda kukufahamisha kuhusu? Je, mamlaka na nguvu za Mungu ni mtazamo mmoja unaoelezea kuhusu hadhi Yake halisi na inavyoonyeshwa? Je, mamlaka na nguvu hizi ni sehemu ya hali Yake halisi ambayo inathibitisha utambulisho Wake na hadhi? Je, maswali haya yamekufahamisha kile Ninachoenda kusema? Ni nini Ninachotaka uelewe? Fikiria hili kwa makini.
Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,hukumu

(I) Kwa Kupinga Mungu Kila Wakati, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu

Kwanza, hebu tuweze kuangalia mafungu mbalimbali ya maandiko yanayofafanua “kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu.”
(Mwa 19:1-11) Na wakaja malaika wawili Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma: na Lutu alipowaona akaondoka akaenda kuwalaki; akainama kifudifudi; Na akasema, tazama sasa, bwana zangu, ingieni ndani, nawasihi, ndani ya nyumba ya mtumwa wenu, na mlale usiku mzima, muoshe miguu yenu, na asubuhi muamke mwondoke na mapema mwende zenu. Wakasema, La; lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Na akawasihi sana; nao wakaja, na wakaingia katika nyumba yake; na akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyo na chachu, na wakala.
Lakini kabla hawajalala, watu wa mji, hata wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka sehemu zote: Na wakamwita Lutu, wakamwambia, Wako wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Walete kwetu, ili tuweze kuwajua. Lutu akaenda mlangoni walikokuwa, akafunga mlango nyuma yake. Na akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu wa kiume; niruhusu, nawasihi, nitawatolea kwenu muwafanyie vilivyo vizuri machoni penu: ila watu hawa msiwatende neno; kwa kuwa wamekuja chini ya kivuli cha paa yangu. Wakasema, Ondoka. Kisha wakasema tena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni, naye kumbe anataka kuhukumu: basi tutakutenda wewe vibaya, kuliko vile tutawatenda hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, hata Lutu, hata wakakaribia kuuvunja mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu nyumbani walikokuwa, na wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu waliokuwa mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa: kiasi kwamba wakachoka wasiweze kuutafuta mlango.
(Mwa 19:24-25) Kisha BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA; Na akaangusha miji hiyo, na bonde lote, na wakaaji wote wa miji hiyo, na yote yaliyomea kutoka katika nchi.
Kutoka kwenye mafungu haya, si vigumu kuona kwamba dhambi ya Sodoma na kupotoka kwake tayari vilikuwa vimefikia kiwango kilichochukiza binadamu na Mungu, na kwamba kwa macho ya Mungu mji ulifaa kuangamizwa. Lakini nini kilichofanyikia mji huu hapo awali kabla haujaangamizwa? Ni nini tunachoweza kujifunza kutoka kwenye matukio haya? Je, mtazamo wa Mungu katika matukio haya unatuonyesha nini kuhusu tabia yake? Ili kuelewa hadithi nzima, hebu na tuweze kusoma kwa makini kile kilichorekodiwa katika Maandiko ….

Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya chajio, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Walete kwetu, ili tuweze kuwajua..” Ni nani aliyesema maneno haya? Alikuwa akiwaambia kina nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakuhuzunisha? Je, unabubujikwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yananuka Shetani? Kupitia kwa maneno haya, unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na ushamba wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya hotuba yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; ule mtazamo tu wa mtu mwengine uliwafanya watu hawa kutaka kudhuru na kuwapotosha wao…. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potoshi na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za dhambi na umwagikaji wa damu.
Alipojipata uso-kwa-uso na genge la majambazi waliojaa ukatili, watu waliokuwa wamejaa na maono ya kupotosha-nafsi, Lutu aliitikia vipi? Kulingana na Maandiko: “Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu wa kiume; niruhusu, nawasihi, nitawatolea kwenu muwafanyie vilivyo vizuri machoni penu: ila watu hawa msiwatende neno; kwa kuwa wamekuja chini ya kivuli cha paa yangu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kutokana na akili razini, watu hawa wangekubali masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili pekee; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, wakiwa na motisha ya asili yao ya dhambi, hawakuliwachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu maono zaidi kuhusu asili ya kweli na potoshi ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.
Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Sodoma
Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Ondoka. Kisha wakasema tena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni, naye kumbe anataka kuhukumu: basi tutakutenda wewe vibaya, kuliko vile tutawatenda hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, hata Lutu, hata wakakaribia kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu kubwa zaidi ya kuwadhuru wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio lao, ilikuwa tu hali ya kujiamulia kufanya mambo kabla ya kujua ukweli wake, iliyoufanya mji huo kutaka kuwadhuru vibaya wajumbe hawa wawili; walitaka kuwadhuru watu wawili ambao hawakuhusiana kwa vyovyote vile na wao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potoshi ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.
Walipowaamuru watu hawa watoke kwa Lutu, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandishi yanayofuata tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawaje hakujua kuhusu sababu yao ya kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwakabidhi binti zake wawili badala ya watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kitendo cha haki ya Lutu; vilevile ni onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na hali halisi ya Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alijaribu hata kufanya biashara ya kuwabadilisha binti zake wawili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, kulikuwa na mtu yeyote mwengine ndani ya mji ambaye angefanya jambo kama hili? Kama vile hoja zinavyothibitsha—la! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa kuangamizwa pamoja na mlengwa aliyestahili kuangamizwa.

Sodoma Yaangamizwa kwa Kuchochea Hasira za Mungu

Wakati watu wa Sodoma walipowaona watu hawa wawili, hawakuuliza sababu ya wao kuja wala hakuna yule aliyeuliza kama walikuwa wamekuja kueneza mapenzi ya Mungu. Kinyume cha mambo, walikusanyika na kuwa umati wa watu na, bila kusubiri ufafanuzi wowote, walikuja kuwakamata watumishi hawa wawili ni kana kwamba walikuwa mbwakoko au mbwa mwitu. Je, Mungu aliyatazama mambo haya wakati yalipokuwa yakifanyika? Mungu alikuwa akifikiria nini katika moyo Wake kuhusiana na tabia hii ya binadamu, aina ya jambo hili? Mungu aliamua kuangamiza mji huu; Asingesita wala kusubiri, wala Asingeendelea kuonyesha subira yake. Siku yake ilikuwa imetimia, na kwa hivyo Aliweza kuweka wazi kazi Aliyopenda kufanya. Hivyo basi, Mwanzo 19:24-25 inasema, “Kisha BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA; Na akaangusha miji hiyo, na bonde lote, na wakaaji wote wa miji hiyo, na yote yaliyomea kutoka katika nchi.” Mistari hii miwili inawaambia watu mbinu ambayo kwayo Mungu aliuangamiza mji huu; pia inawaambia watu kile ambacho Mungu aliangamiza. Kwanza, Biblia inasimulia kwamba Mungu aliunguza mji kwa moto, na kwamba kiwango cha moto kilikuwa tosha kuangamiza watu wote na kila kitu kilichomea kwenye ardhi. Hii ni kusema kwamba, moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji; uliangamiza pia watu wote na vitu vilivyo hai ndani yake, vyote bila kuacha chochote nyuma. Baada ya mji kuangamizwa, ardhi ilikuwa tupu bila kitu chochote kilicho hai. Hakukuwa tena na maisha, wala dalili zozote za maisha. Mji ulikuwa umebadilika na kuwa ardhi iliyoharibiwa, mahali patupu palipojaa kimya cha kutisha. Kusingekuwa na matendo maovu zaidi dhidi ya Mungu mahali hapa; kusingekuwa na uchinjaji zaidi au umwagikaji wa damu.
Kwa nini Mungu alitaka kuuchoma mji huu kabisa? Ni nini unachoweza kuona hapa? Je, Mungu angevumilia kumwona mwanadamu na asili, viumbe Vyake mwenyewe, vikiangamia hivi? Kama unaweza kutambua ghadhabu ya Yehova Mungu kutokana na moto ule ambao uliangushwa kutoka mbinguni, basi si vigumu sana kuona kiwango Chake cha hasira kali kutoka kwenye lengo la maangamizo Yake pamoja na kiwango ambacho mji huo uliweza kuangamizwa. Wakati Mungu anadharau mji, Ataweza kutekeleza adhabu Yake juu ya mji huo. Wakati Mungu anachukizwa na mji, Ataweza kutoa maonyo mbalimbali akifahamisha watu kuhusu ghadhabu Yake. Hata hivyo, wakati Mungu anaamua kukomesha na kuangamiza mji—yaani, wakati hasira Yake na adhama vimekosewa—Hataweza kutoa maonyo au adhabu nyingine. Badala yake, Ataweza kuuangamiza moja kwa moja. Ataufanya kutoweka kabisa. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu.

Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaifuta Kabisa

Mara tu tunapokuwa na ufahamu wa jumla kuhusu tabia ya haki ya Mungu, tunaweza kurejesha umakinifu wetu kwenye mji wa Sodoma—kile ambacho Mungu aliona kuwa mji wa dhambi. Kwa kuelewa hali halisi ya mji huu, tunaweza kuelewa ni kwa nini Mungu alitaka kuuangamiza na ni kwa nini Aliuangamiza kabisa. Kutokana na haya, tunaweza kujua tabia ya haki ya Mungu.
Kutoka katika mtazamo wa binadamu, Sodoma ilikuwa ni mji ulioweza kutosheleza kikamilifu matamanio ya binadamu na maovu ya binadamu. Ulivutia na uliduwaza, kwa muziki na densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume kufurahia na kuruka kichwa. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na yakawaduwaza hadi kuzoroteka. Huu ulikuwa mji uliokuwa na roho chafu na roho za Shetani ziliduruduru hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda dhambi zisizohesabika za ukinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.
Ingawaje mafungu haya mawili hayarekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, ukweli mtupu unaweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, walijaa maovu na walimpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wakatili kwa uwepo wa Mungu, kuja Kwake, adhabu Yake, na hata zaidi, maonyo Yake. Hawakuona chochote kingine chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote ya uovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao ya uovu yaliyofichuliwa kwa kweli yalionekana tu kuwa madogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala Hakutumia zilizala, mtetemeko wa ardhi, tsunami au mbinu yoyote nyingine ya kuuangamiza mji huu. Kule kutumia moto na Mungu kuangamiza mji huu kulimaanisha nini? Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ulitoweka kabisa kutoka ulimwenguni na kutoka katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilisita kuwepo, baada ya kufutwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na mambo yote yaliyohusiana na mji huu yaliangamizwa. Kusingekuwa na maisha baada ya kifo au roho kuwa mwilini mwao; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka katika ubinadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingesita kuwepo na kuenea. Yalimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo liliupatia mji huo mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, matumizi ya moto na Mungu ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kupinga Mungu kwa kupotosha na kudanganya binadamu, na vilevile ni ishara ya kudhalilishwa kwa muda kwenye maendeleo ya ubinadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.
Wakati ule moto ambao Mungu alituma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungesita kuwepo, na vilevile kila kitu ndani ya mji wenyewe. Uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na adhama ya Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la kutowahi kuutazamia mji huo tena” la Mungu ni hasira Yake, pamoja na adhama Yake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo tena. Baada ya mji huo kuacha kuchomeka, huku ukiwa umeacha nyuma jivu pekee, ulikuwa kwa kweli umesita kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma kwa jumla na watu waliokuwa wamejaa dhambi ndani yake, wala kuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji uliokuwa umepatwa na dosari ya dhambi; hata zaidi, moto huu uliangamiza kumbukumbu za maovu na ukinzani wa binadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudio la Mungu kwa kuuchoma ule mji.
Ubinadamu ulikuwa umepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na kukufuru. Hata wakati watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba; vilevile hawakuacha mwenendo wao wa maovu. Kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na hali yao halisi ya uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba ukinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potoshi, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la matusi au kejeli iliyotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingeongeza hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haifai kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliotiririka na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alipenda kuwaondoa watu waliokuwa ndani yake na uzima wa dhambi zao kwa njia kamilifu zaidi, kuwafanya watu hawa wa mji kusita kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa kuongezeka. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kusita kuwepo.”

Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Namna Mungu alivyoshughulikia ubinadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anapokabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. Anaweza kuonyesha hasira Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.
Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa ubinadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya kimwili; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangesita kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia moja ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni dhana moja ya hali halisi ya hasira ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Yeye husita kufichua huruma au upole wa upendo wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa huruma Yake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kwa muda mfupi, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira Yake na adhama, ambayo binadamu hafai kukosea, na pia ni maonyesho ya dhana moja ya tabia Yake ya haki. Wakati watu wanaposhuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuuona adhama Yake au kuhisi kutovumilia Kwake kwa kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia ubinadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona picha ya upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huyu ni Mungu asiyevumilia kosa. Tabia ya Mungu isiyovumilia kosa inazidi yale mawazo ya kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe ambavyo havikuumbwa, hakuna kati ya hivyo kinachoweza kuhitilafiana na kingine au kuathiri kingine; lakini hata zaidi, hakiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, dhana hii ya tabia ya Mungu ndiyo ambayo ubinadamu unafaa kujua zaidi. Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo vya uovu vya Shetani—vya kupotosha na kudanganya wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya hali Yake halisi takatifu na isiyo na doa. Ni kwa sababu ya haya ndiposa Hataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumba au ambavyo havikuumbwa vimpinga waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu binafsi ambaye Aliwahi kumwonyesha huruma au kuchagua anahitaji tu kuchochea tabia Yake na kukiuka kanuni Yake ya subira na uvumilivu, na Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki bila ya huruma hata kidogo au kusitasita kokote—tabia isiyovumilia kosa lolote.

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Kwa kuielewa mifano hii ya hotuba, fikira na vitendo vya Mungu, je, unaweza kuielewa tabia ya haki ya Mungu, tabia isiyoweza kukosewa? Mwishowe, hii ni dhana ya tabia ya kipekee kwa Mungu Mwenyewe, bila ya kujali ni kiwango kipi ambacho binadamu anaweza kuelewa. Kutoweza kuvumilia kosa na Mungu ndiyo hali halisi Yake ya kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; adhama ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Mtu hana haja kutaja kwamba ni ishara pia ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya asili. Haibadiliki kamwe na kupita kwa muda, wala haibadiliki kila wakati mahali panapobadilika. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chaake halisi cha kweli. Haijalishi ni nani anayetekelezea kazi Yake, hali Yake halisi haibadiliki, na wala tabia ya haki Yake pia. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika hali Yake halisi au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake hukosewa katika tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anampima ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapojaribu kila mara ghadhabu ya Mungu—na ndio maana pia dhambi huongezeka—hasira ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu vinapopata changamoto, wakati nguvu za haki zinapata kuzuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya hali halisi ya Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na kushindana na Yeye ni za maovu, kupotoka na kutokuwa na dhalimu; zinatoka Kwake na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu bila dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.
Ingawaje kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni dhana ya maonyesho ya tabia ya haki Yake, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au haina kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa ghadhabu, wala Hakimbilii kufichua hasira Yake na adhama Yake. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashtumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya kusikia maneno waliyomzungumzia Ayubu? Je, Aliwashtumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu kuwasihi, kuwaombea; Mungu, kwa mkono mwingine, hakuchukua lawama zao na kutia moyoni. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo mkuu ambao Mungu anashughulikia ubinadamu uliopotoka, na usiojua. Kwa hivyo, kushushwa kwa hasira ya Mungu si kwa vyovyote vile maonyesho au hali ya kutoa nje hali Yake ya moyo. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu hawachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho ya tabia ya haki Yake na maonyesho halisi ya tabia ya haki Yake; ni ufunuo wa ishara ya hali Yake halisi takatifu. Mungu ni hasira, asiyevumilia kosa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni ubinadamu uliopotoka ambao unafuata mkondo wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii miongoni mwa sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mwanadamu aliyepotoka mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Binadamu atalipuka kwa ghadhabu na kutoa nje hisia zake ili kutetea uwepo wa dhambi, na matendo haya ndiyo njia ambayo binadamu anaonyesha kutotosheka kwake. Matendo haya yamejaa hadi pomoni kwa kuchafuliwa; yamejaa kwa mifumo na mbinu mbalimbali; yamejaa kupotoka na maovu ya binadamu; zaidi ya hayo, yanajaa kwa malengo na matamanio ya binadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, binadamu hataruka juu kwa ghadhabu ili kutetea uwepo wa haki; kinyume ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateshwa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kushtuka. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, kutoa nje ghadhabu kwa binadamu ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiositishwa wa binadamu wa kimwili. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote za kudhuru binadamu zitasitishwa; nguvu zote katili zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kudanganywa; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ujazo wa Mungu miongoni mwa mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni usalama unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kutapakaa kwa nguvu, na pia ni usalama unaolinda kuwepo na kuenea kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.
Unaweza kuona hali halisi ya hasira ya Mungu katika kuangamiza Kwake kwa Sodoma? Je, kuna jambo lolote lililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Ili kutumia maneno ya binadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa najisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kunayo njama yoyote? Je, zipo siri zozote zisizotamkika? Ninaweza kukwambia wazi na kwa makini: Hakuna sehemu ya hasira ya Mungu inayoweza kumwongoza mtu kwa shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa najisi na haijasheheni nia au shabaha zozote nyingine. Sababu ya ghadhabu Yake ni safi, haina lawama na haipingiki. Ni ufunuo wa kawaida na onyesho la hali Yake halisi ya utakatifu; ni kitu ambacho hakuna kiumbe chochote kinamiliki. Hii ni sehemu ya tabia ya kipekee ya haki ya Mungu, na ni utofauti wa wazi kati ya hali halisi husika ya Muumba na uumbaji Wake.
Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira yao au kulinda sura yao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapopenda bila ya hata kiwango kidogo zaidi cha kujizuia. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishi kusudi lake, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na hali halisi vinavyolingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira potoshi ya ubinadamu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ya kuacha, tabia ya binadamu iliyopotoshwa na Shetani inaanza kwa tamanio la kusalimisha kupotoka, na inatokana na kupotoka; hivyo basi, ghadhabu ya binadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na hasira ya Mungu, haijalishi ni bora namna gani kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za giza zinakaguliwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Shabaha ya ghadhabu ya Mungu si kusalimisha hadhi na utambulisho Wake binafsi, lakini kusalimisha uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, kusalimisha sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni bora sana, ya kiasili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna makusudi yoyote katika hasira Yake kali, wala hakuna udanganyifu au njama yoyote; au hata zaidi, hasira Yake kali haina tamanio lolote, ujanja, mambo ya kijicho, udhalimu, maovu, au kitu kingine ambacho binadamu wote waliopotoka huwa navyo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua hali halisi ya kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila suala Analofanya ni wazi kabisa, vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu wa kutowaza-kikamilifu; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hii ndiyo dhana ya kimatendo ya hasira ya Mungu, na ni kwa sababu ya dhana hii ya kimatendo ya hasira ya Mungu ambapo ubinadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, ubinadamu ungeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, virembo na vizuri vingeangamizwa na kusita kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na mpangilio unaotawala uumbaji vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ametumia bila kusita, tabia Yake ya haki kusalimisha na kuendeleza uwepo wa kawaida wa ubinadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na adhama, watu wote waovu, vitu, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa ubinadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Kwenye milenia mbalimbali zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na kuchukua nafasi ya wasaidizi wa Shetani na kusaidia katika kazi Yake ya kusimamia ubinadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu ya haki zaidi miongoni mwa binadamu haijawahi kuangamizwa.
Sasa kwa vile unao ufahamu wa hali halisi ya hasira ya Mungu, bila shaka lazima utakuwa na ufahamu bora zaidi wa namna ya kutofautisha maovu ya Shetani!

Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Hali Yake Halisi

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.
Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake maovu. Kati ya vitendo vyote vya maovu ambavyo Shetani ametekeleza kwa binadamu—tangu jitihada zake za mapema za kudanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, na ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kutambua na kumwacha—hakuna hata moja inayoshindwa kufichua hali halisi ya uovu wa Shetani; hakuna hata moja inayoshindwa kuthibitisha hoja kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata moja hushindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inasalimisha maovu yake, inadumisha maendelezo ya vitendo vyake vya maovu, inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa ubinadamu. Wao ni katili kwa Mungu, na ndio wale ambao hasira ya Mungu itaangamiza. Ingawaje Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake kali ni mbinu ya kutoa nje asili yake mbovu. Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti ubinadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila matumizi ya hasira ya Mungu huwa yanafichua sura halisi ya aibu ya Shetani; na pia kufichua na kuweka kwenye nuru matamanio ya maovu ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Kule kulipuka kwa hasira kali ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huwa ni ishara ya ulinzi na maendelezo ya mambo mazuri, na huwa ni ishara ya asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni