Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sodoma. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sodoma. Onyesha machapisho yote

3/12/2018

πŸ“–πŸ“–Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tabia ya Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa vile sasa mumesikiliza kikao cha ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mumejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kushika, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo-upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe.