5/22/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Tano

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Tano

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anapoweka mahitaji kwa wanadamu ambayo ni magumu kwao kueleza, na maneno Yake yanapogonga moja kwa moja katika moyo wa mwanadamu na watu wanatoa mioyo ya dhati ili Afurahie, basi Mungu huwapa watu nafasi ya kutafakari, kufanya uamuzi, na kutafuta njia ya kutenda. Kwa njia hii, wote ambao ni watu Wake kwa mara nyingine, ngumi zikiwa zimekunjwa kwa ujasiri, wanatoa hali zao zote kwa Mungu. Baadhi, labda, wanaweza kuunda mpango na kuanzisha ratiba ya kila siku, wanapojiandaa kujisisimua na kwenda kazini, wakitoa sehemu ya nguvu zao kwa mpango wa usimamizi wa Mungu, ili kuleta utukufu juu ya mpango huu na kuharakisha hitimisho lake. Na, kama vile watu wanavyojipata katika hali hii ya kisaikolojia, wakishikilia mambo haya akilini mwao wakati wanapokuwa wakiendelea na kazi zao, wanapozungumza, na wanapokuwa wakifanya kazi, Mungu, kwa haraka akifuatilia hili, Huanza kusema tena: “Wakati Roho Wangu anatoa sauti, anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, nyinyi mnalifahamu hili?” Kadri mwanadamu alivyo na uamuzi zaidi, ndivyo atakavyokuwa na tamaa zaidi ya kufahamu mapenzi ya Mungu na ndivyo atakavyotamani kwa bidii Mungu aweke madai kwake; na hivyo Mungu atawapa watu kile ambacho wanataka, Akitumia fursa hii kutoa maneno Yake, yaliyokuwa yamewekwa tayari kwa muda mrefu, chokomeani mwa maficho ya hali yao. Ingawa maneno haya yanaweza kuonekana kuwa makali au ya kukwaruza, kwa binadamu ni matamu zaidi kulinganishwa na kitu chochote. Mara moja, moyo unachanua kwa furaha, kana kwamba binadamu wako mbinguni, au wamepelekwa katika ulimwengu mwingine, paradiso ya hakika ya mawazo, ambako mambo ya nje ya ulimwengu hayawaathiri tena binadamu. Ili kwamba watu wasizungumze tena, kama walivyokuwa na tabia ya kufanya zamani, kwa nje na kutenda kwa nje, na hivyo kushindwa kuweka misingi thabiti: ili kuiepuka hatima hii, wakati kile ambacho watu wanatamani mioyoni mwao kimefanikiwa, na zaidi wanapojiandaa kwenda kazini kwa shauku kubwa, Mungu bado anabadili njia Yake ya kuzungumza kwa hali yao ya kisaikolojia, na, kwa ufupi na bila kujizuia, Hubainisha shauku yote na sherehe ya kidini ndani ya mioyo yao. Kama Mungu alivyosema: “Je, hakika mmeona umuhimu ulioko humu?” Ikiwa ni kabla au baada ya mwanadamu kuweka dhamira yake juu ya kitu fulani, haweki umuhimu mkubwa juu ya kumjua Mungu katika matendo Yake au kwa maneno Yake, lakini anaendelea kutafakari swali hili: "Ninaweza kumfanyanyia nini Mungu? Hilo ndilo suala muhimu!" Hii ndiyo maana Mungu anasema: “Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia ya aibu, pia, mantiki yoyote!” Mara tu baada ya Mungu kusema maneno haya, mara moja watu hutambua, na kana kwamba wamepatwa na mshtuko wa umeme, wanaharakisha wanaificha mikono yao kwenye vifua vyao, wakiogopa kuchochea ghadhabu ya Mungu mara ya pili. Kuongezea kwa hili, Mungu amesema pia: “Wakati mmoja au mwingine, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu. Usithubutu kunidanganya, ukifikiri kwamba umesimama kwa ajili ya ushuhuda Wangu! Wanaposikia maneno kama haya, watu wanaogopa hata zaidi, kama vile wangeogopa wakiwa wamemwona simba. Wanajua vizuri kabisa mioyoni mwao. Wao kwa upande mmoja wana wasiwasi wasiliwe na simba huku kwa upande mwingine wanahisi kutojua pa kutorokea. Wakati huu, mpango ndani ya moyo wa mwanadamu hupotea usionekane tena, kabisa na kwa kamilifu. Kupitia maneno ya Mungu, ninahisi kama ninaweza kuona kila kipengele cha aibu ya binadamu: Tabia ya kuinamisha kichwa na kuona aibu, kama mtahiniwa ambaye ameanguka mtihani wa kuingia chuo kikuu, maadili yake ya fahari sana, familia yenye furaha, siku za usoni zenye ufanisi, na kadhalika na kadhalika, yote yaligeuka—pamoja na Mpango wa Kufanya ya Kisasa wa Mwaka 2000—kuwa maongezi matupu, yanayosababisha mazingira ya kufikirika katika filamu ya sayansi ya ubunifu. Hii ni kubadilishana mambo ya kukaa tu na yale ya utendaji kazi, kuwafanya watu, ndani ya kutojishughulisha kwao, kusimama mahali ambapo Mungu amewaweka. Jambo muhimu la pekee ni ukweli kwamba wanadamu wanaogopa sana kupoteza cheo hiki, na hivyo wanakwamilia beji zao za ofisi kwa bidii yao yote, wakiogopa kuwa mtu anaweza kuzipokonya kutoka kwao. Wakati binadamu wako katika hali hii ya akili, Mungu hana wasiwasi kuwa watakuwa wenye kukaa tu, na kwa hiyo inavyostahili Yeye hubadili maneno Yake ya hukumu kwa maneno ya kuhoji. Hawapi watu fursa ya kupunga hewa tu, lakini pia Anawapa fursa ya kuchukua matarajio waliyokuwa nao kabla ya sasa na kuyatayarisha kwa ajili ya kuyaangalia baadaye: Kile ambacho hakifai kinaweza kubadilishwa. Hii ni kwa sababu Mungu bado Hajaanza kazi Yake—hii ni bahati nzuri katikati ya bahati mbaya sana—na, zaidi ya hayo, Hawahukumu. Kwa hiyo acha nindelee kumpa ibada yangu yote!
Halafu, hupaswi kamwe kwa sababu ya hofu yako, kuweka kando maneno ya Mungu. Angalia uone kama Mungu ana mahitaji yoyote mapya. Kwa hakika, utagundua aina hii ya mahitaji: “Kuanzia wakati huu na kuendelea, katika mambo yote lazima uingie katika ukweli wa kutenda; kupiga domo tu, kama ulivyokuwa ukifanya, hakutakusaidia tena.” Ndani yake pia kuna hekima ya Mungu. Mungu daima Amewalinda shahidi Wake mwenyewe, na wakati ukweli wa maneno ya zamani umefikia hitimisho lake, hakuna mtu yeyote anayeweza kufahamu ujuzi wa "ukweli wa utendaji.” Hii inatosha kuthibitisha ukweli wa kile ambacho Mungu alisema "Ninaanza kufanya kazi hiyo Mwenyewe.” Inahusiana na maana halisi ya kazi katika uungu, na pia inahusiana na sababu kwa nini wanadamu, baada ya kufikia hatua mpya ya mwanzo, bado hawawezi kuelewa maana halisi ya maneno ya Mungu. Hii ni kwa sababu, zamani, idadi kubwa ya watu ingeweza kushikamana na ukweli katika maneno ya Mungu, ilhali leo hawana ufahamu juu ya ukweli wa kutenda, lakini wanaelewa tu vipengele vya juu juu ya maneno haya bila kuelewa asili yao. Hata muhimu zaidi, ni kwa sababu leo, katika ujenzi wa ufalme, hakuna mtu anayeruhusiwa kuingilia kati, lakini kutii tu amri ya Mungu kama roboti. Kumbuka hili vizuri! Kila wakati ambao Mungu huleta mambo ya zamani, Yeye huanza kusema kuhusu hali halisi ya leo; hii ni namna ya kuzungumza ambayo inafanya tofauti kubwa sana kati ya kile kinachokuja kabla na kile kinachokuja baadaye, na kwa sababu hii inaweza kufikia matunda bora hata zaidi, ikiwawezesha watu kuiweka hali ya sasa sambamba na ile ya wakati uliopita, na kwa njia hii kuepuka kuchanganya tofauti iliyopo kati ya hizi mbili. Huu ni upande mmoja wa hekima ya Mungu, na lengo lake ni kufikia matunda ya kazi. Baada ya hili, Mungu kwa mara nyingine Hufunua uovu wa wanadamu, ili kwamba binadamu hawatasahau kamwe kula na kunywa maneno ya Mungu kila siku, na hata muhimu zaidi ili kwamba kila siku watajijua na kuchukua hili kama somo ambalo wanapaswa kujifunza kila siku.
Anapomaliza kuzungumza maneno hayo, Mungu amefanikisha matokeo ambayo Alinuia awali. Na kwa hiyo, bila kujali hata kidogo kama binadamu wamemwelewa, Yeye huipitia upesi sana kwa maneno machache, kwa sababu kazi ya Shetani haina uhusiano wowote na binadamu—kuhusu hili binadamu hawana ufahamu. Sasa, ukiacha ulimwengu wa roho, angalia zaidi jinsi Mungu anavyofanya mahitaji Yake kwa binadamu: “Ninapopumzika katika makaazi Yangu, Mimi huchunguza kwa karibu: Watu wote duniani wamo katika pilikapilika, "wakisafiri duniani kote" na kukimbia huku na kule, yote kwa ajili ya hatima yao, maisha yao ya baadaye. Lakini hakuna hata mmoja nguvu ya kutosha kwa ajili ya kujenga ufalme Wangu, hata nguvu kiasi cha ile mtu anayotumia kuvuta pumzi.” Baada ya kubadilishana mambo haya ya kawaida na wanadamu, Mungu bado hajali kuwahusu, lakini Anaendelea kuzungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, na kwa njia ya maneno haya, Anaonyesha hali ya maisha ya jamii ya wanadamu kwa ujumla. Ni wazi kuona, kutokana na "kusafiri duniani kote" na "kukimbia huku na kule," kwamba maisha ya binadamu hayana maudhui. Isingekuwa kwa ajili ya wokovu wenye nguvu Mungu, wale waliozaliwa katika familia ya chini na nje ya mstari wa kifalme wa China wangeishi maisha yote bure hata zaidi na ni heri waanguke Kuzimu na jahanamu kuliko kuja ulimwenguni. Chini ya utawala wa joka kuu jekundu, wao, bila kujua wenyewe, wamekosa dhidi ya Mungu na hivyo, kwa kawaida na tena bila kujua, wameanguka chini ya kuadibu kwa Mungu. Kwa sababu hii, Mungu amekwisha wachukua "waliookolewa kutokana na dhiki" na "wasio na shukrani" na kuwaweka pamoja kwa kuwalinganisha, kwamba wanadamu waweze kujitambua vizuri zaidi, na kuunda kutoka kwa hili foili kwa neema Yake ya kuokoa. Je! Hili halileti matokeo yanayofaa zaidi? Bila shaka, Sihitaji kusema kwa wazi, watu wanaweza, kutokana na yaliyomo katika mazungumzo ya Mungu, kuonyesha kipengele cha kukashifu, na tena, kipengele cha wokovu na rufaa, na hata tena, maonyesho mafupi ya huzuni. Wanaposoma maneno haya, watu huanza bila kujua kujisikia aina ya kukataa katika mioyo yao, na hawana budi ila kutoa machozi.... Lakini Mungu hatazuiliwa kwa sababu ya hisia chache za huzuni, wala Yeye, kwa sababu ya upotovu wa watu wote, Hataacha kazi Yake katika kuwaadhibu watu wake na kufanya mahitaji kwao. Kwa sababu hii, mada Zake mara moja hugusia juu ya hali kama hizo za leo, na zaidi ya hayo Anahubiri kwa binadamu uadhama wa amri Zake za utawala, ili kwamba mpango Wake uendelee kwenda mbele. Hii ndiyo sababu, baada ya hili kwa kasi ya kutosha na kumkunja samaki angali mbichi, Mungu anatangaza wazi wakati huu muhimu katiba ya wakati, katiba ambayo inapaswa kusomwa kwa uangalifu kwa karibu kila kifungu kabla binadamu waweze kuelewa mapenzi ya Mungu. Hakuna haja ya kuingia zaidi katika hili sasa—lazima tu wasome kwa makini zaidi.
Leo, nyinyi—hili kundi la watu hapa—ndio pekee ambao mnaweza kuona kwa kweli maneno ya Mungu. Hata hivyo, kwa kumjua Mungu, watu wa leo wamebaki nyuma ya mtu yeyote katika enzi zilizopita. Kutokana na hili ni wazi kabisa kiwango cha juhudi ambazo Shetani amewekeza juu ya watu kwa miaka hii elfu kadhaa, na kiwango ambacho zimewapotosha wanadamu, ambacho ni kikubwa sana kiasi kwamba, hata ingawa Mungu amesema maneno mengi, bado binadamu hawamwelewi wala hawamjui Mungu, lakini badala yake wanajaribu kusimama na kumpinga hadharani. Na hivyo Mungu mara nyingi huwafanya watu wa zamani kuwa mfano kama ulinganishi kwa watu wa leo, ili kuwapa watu wa leo, licha ya wao kuwa wasiohisi na waliochanganyikiwa, nafasi ya uhakika ya marejeo. Kwa sababu wanadamu hawana ujuzi wa Mungu, na kwa sababu hawana imani ya kweli ndani Yake, Mungu amewahukumu binadamu kuwa hawana sifa na mantiki, na hivyo, mara kwa mara, Amewaonyesha watu uvumilivu na kuwapa wokovu. Pigano linapiganwa kwa njia hii katika ulimwengu wa roho: Ni tumaini lisilofanikiwa la Shetani kuwapotosha wanadamu kwa kiwango fulani, kuufanya ulimwengu mbaya na mwovu, na hivyo kumvuta mwanadamu ndani ya matope na kuuharibu mpango wa Mungu. Lakini mpango wa Mungu sio kuwafanya binadamu wote kuwa watu wanaomjua, bali badala yake kuchagua sehemu ya kuwakilisha yote, na kuacha wengine kama bidhaa taka, kama bidhaa zilizoharibika, wanaofaa kutupwa kwenye rundo la takataka. Na hivyo, ingawa kutoka kwa mtazamo wa Shetani kuwamiliki watu wachache inaonekana kuwa fursa nzuri ya kuuharibu mpango wa Mungu, je, zuzu kama yeye anawezaje kujua kuhusu nia ya Mungu? Hii ndiyo maana Mungu alisema, zamani, "Nimeufunika uso wangu ili kuepuka kuangalia ulimwengu huu.” Tunajua kidogo kuhusu hili, na Mungu hahitaji kuwa wanadamu wawe na uwezo wa kufanya chochote, badala yake kwamba watambue kile Anachofanya kama miujiza na kisichoweza kueleweka na kumcha sana katika mioyo yao. Ikiwa, kama mtu anavyofikiria, Mungu angemwadibu bila kujali hali, basi dunia nzima ingekuwa imeangamia kwa muda mrefu. Je, si hii ingemaanisha kuanguka ndani ya mtego wa Shetani? Na hivyo Mungu hutumia maneno Yake tu kufikia matunda Aliyo nayo mawazoni; mara chache sana kuna ujio wa ukweli. Je! Huu sio mfano wa kile Alichosema: Kama Singeuonea huruma ukosefu wenu wa sifa za kustahili, mantiki, na ufahamu, basi nyote mngeangamia katika kuadibu Kwangu, na kutoweka kabisa ulimwenguni. Lakini hadi wakati Kazi Yangu hapa duniani itakapomalizika, Mimi Nitabaki mwenye huruma kwa wanadamu”?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni