Ngurumo Saba Zatoa Sauti- Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni
Mimi hueneza kazi Yangu katika mataifa. Katika ulimwengu mzima unang’aa utukufu Wangu; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi Ninayosambaza. Kuanzia sasa, Ninaingia enzi mpya na kuleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Ninaporudi katika "nchi Yangu," Ninaanza sehemu nyingine ya kazi katika mpango Wangu wa awali ili mwanadamu aje kujua zaidi kunihusu. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, hivyo Mimi Nasafiri huku na kule kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Ni enzi mpya, licha ya yote, na Ninaleta kazi mpya ili niwachukue watu wapya zaidi katika enzi mpya na kuwatupa kando zaidi ya wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Ninatekeleza hatua ya kazi isiyoweza kueleweka na mwanadamu na kuwafanya kutingika katika upepo, ambapo baadaye wengi kwa kimya watabebwa na upepo unaovuma.