Umeme wa Mashariki | Juu ya Hatima |
Mwenyezi Mungu : Wakati wowote hatima inatajwa, muichukulie kwa uzito maalumu; nyinyi nyote ni mahususi hasa kuhusu jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye kuwa na hatima nzuri. Naweza jishirikisha na hamu yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Kabisa hamtaki miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kuishi kwa uhuru zaidi na kwa urahisi. Hivyo mnahisi wasiwasi hasa wakati wowote hatima inatajwa, mkihofia kwa undani kwamba msipokuwa waangalifu vya kutosha, mnaweza kosea Mungu na kuwa chini ya adhabu inayostahili. Hamjasita kufanya maafikiano kwa ajili ya hatima zenu, na wengi wenu ambao wakati mmoja walikuwa wa kuzunguka na wapuuzi hata kwa ghafla wamegeuka hususa wapole na wa dhati; unyofu wenu hata una mzizimo. Pasipo kutilia maanani, nyinyi nyote mna mioyo minyoofu, na kutoka mwanzo hadi mwisho mmejifungua wazi Kwangu bila kuficha siri zozote katika mioyo yenu, yawe lawama, udanganyifu, au ibada. Kwa jumla, "mmekiri" kwa uwazi Kwangu yale mambo muhimu katika pahali pa siri yenye kina kwenu. Mambo kama yalivyo, Sijawahi kuepuka aidha ya mambo kama haya, kwa sababu yamekuwa ya kawaida Kwangu.