2/11/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | 34 Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi

Neno la Mwenyezi Mungu  | 34  Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu. Je wewe hutenda vipi wakati watu walio chini yako wanakurai na kukupa sifa kwa matokeo unayozalisha katika kazi yako? Je wewe hutenda vipi wakati watu wanakupa mapendekezo? Je, wewe huomba mbele ya Mungu?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida

Kanisa la Mwenyezi Mungu,ndugu na dada,Wakristo wa China

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida

Watu wanapozidi kuwa wapokelevu wa maneno ya Mungu, ndivyo wanavyozidi kupata nuru na wanaendelea zaidi kufuatilia maarifa ya Mungu kwa njaa na kiu ya hali ya kuwa mwenye haki. Ni wale tu ambao wanapokea maneno ya Mungu wanaweza kuwa na matukio ya undani zaidi na yenye utajiri zaidi; ni wale tu ambao maisha yao yanakuwa ya kupendeza zaidi na zaidi. Kila mtu ambaye anafuatilia uzima lazima ashughulikie haya kana kwamba ni kazi yake, na ni sharti awe na hisia kuwa hawezi kuishi bila Mungu, na hakuna mafanikio yoyote bila Mungu, na kila kitu ni ubatili bila Mungu.

2/10/2018

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho "Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote



Mwenyezi Mungu alisema, "Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga."

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kumfuata Mungu

neno la Mwenyezi Mungu | Je, ushawishi wa giza ni nini?

Ushawishi wa giza ni utumwa wa Shetani, ni ushawishi wa Shetani, na ni ushawishi ambao una hali ya kifo.
Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako kwa Mungu kikamilifu, katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa ya Mungu, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya uangalizi na ulinzi wa Mungu.

2/09/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa
imani katika Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Nane

     Kufuatana na sifa za asili za wanadamu, yaani, uso halisi wa wanadamu, kuweza kuendelea hadi sasa hakujakuwa jambo rahisi kweli, na ni kwa njia hii tu ndio nguvu kuu ya Mungu imekuwa dhahiri. Kutegemea kiini cha mwili pamoja na upotovu wa joka kuu jekundu hadi sasa, isingekuwa uongozi wa Roho wa Mungu, mwanadamu angewezaje kusimama leo? Mwanadamu hastahili kuja mbele ya Mungu, lakini Anawapenda wanadamu kwa ajili ya usimamizi Wake na ili kazi Yake kuu iweze kufanikishwa kabla ya muda mrefu sana. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kulipa upendo wa Mungu kwa wanadamu katika maisha yao yote.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)

    Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. "Wanajificha wenyewe katika unyenyekevu." Ukweli ni kwamba, ni wachache miongoni mwenu mnaojua makusudi ya Mungu kuhusu siku za mwisho.

2/08/2018

Umeme wa Mashariki | 8. Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo

Umeme wa Mashariki | 8. Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo

Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi
Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau. Daima nimekuwa na hofu ya kuitembea njia ya Paulo, ambayo ndiyo sababu mimi kwa kawaida mara nyingi husoma maneno ya Mungu kuhusu uzoefu wa Petro ili kuona jinsi alivyopata kumjua Mungu. Baada ya kuishi hivi kwa muda, nilihisi kwamba nilikwishakuwa mtiifu zaidi kuliko hapo awali, hamu yangu ya sifa na hadhi ilikuwa imedidimia, na kwamba nilikuwa nimepata kujijua kidogo.

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani-Kanisa la Ukiwa Linatiwa Nguvu


Baada ya ndugu katika pahali pa mkutano pa kanisa la Mzee wa Kanisa Liu Zhizhong kutupilia mbali pingu za Biblia, walisoma mtandaoni kuhusu kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kwa kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, walistawishwa kwa maji hai ya maisha, na waliweza kurudisha imani na upendo wao wa asili na kuthibitisha ndani ya mioyo yao kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Wakati Mzee wa kanisa Liu Zhizhong aliona hili likifanyika, je, aliweza kuweka chini Biblia na kutafuta kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho? Tafadhali tazama video hii fupi!

2/07/2018

54 Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kumjua Mungu,
kumfuata Mungu
   Kama utajielewa, ni lazima uielewe hali yako ya kweli; jambo muhimu zaidi katika kuielewa hali yako mwenyewe ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zako na mawazo yako. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa; ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo. Hakuna mtu anayeweza kuzidhibiti fikira na mawazo yake. Je, fikira na mawazo haya hutoka wapi? Je, ni nini kiini cha matilaba haya? Je, fikira hizi na mawazo haya huzalishwaje? Je, zinadhibitiwa na nini? Asili za fikira na mawazo haya ni nini? Baada ya tabia yako kubadilika, fikira na mawazo yako, tamaa ambazo moyo wako unatafuta na maoni yako kwa ukimbizaji, ambazo zimefanyizwa kutokana na sehemu ambazo zimebadilika zitakuwa tofauti.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35

Siku hizi, binadamu wote, kwa viwango vinavyotofautiana, wameingia katika hali ya kuadibu. Kama tu alivyosema Mungu, “Naenda mbele na binadamu sako kwa bako.” Hii ni kweli kabisa, lakini watu bado hawawezi kulielewa kabisa wazo hili. Kutokana na hili, sehemu ya kazi ambayo wamefanya imekuwa si lazima. Mungu alisema, “Mimi husaidia na kuwaruzuku kwa mujibu wa kimo chao. Kwa kuwa wanadamu ndio wahusika wakuu wa mpango Wangu wote wa usimamizi, Natoa ushauri zaidi kwa walio katika hii nafasi ya “binadamu” ili waweze kuiigiza kwa moyo wote na kwa uwezo wao wote,” pamoja na, “Hata hivyo, Nakataa kukosoa dhamiri zao moja kwa moja;

2/06/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kumjua Mungu,
Mamlaka ya Mungu (I)

Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena

Mwenyezi Mungu alisema, Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Sauti-ya-Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Saba

Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani. 

2/05/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, na ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa.