
Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia. Iwapo umetambua jinsi ya kupata uzoefu katika hali zote, muktadha na mazingira, bila kushindwa hata kwenye mazingira ya kuchukiza zaidi, na iwapo katika mazingira mazuri kabisa na ya kustarehesha kabisa na katika hali za majaribu makubwa kabisa, haupotoshwi au kudanganyika na katu hauanguki, basi utakuwa umepiga hatua na kuzidisha kimo.