2/18/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Neema

2. Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi

Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote kupitia sheria Zake kwa ajili ya viumbe vyote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao. Hii pia ni mada kubwa sana kwenu. Kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote—je, hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kufanya? Binadamu wenyewe hawawezi. Watu wanaweza tu kuharibu.

2/17/2018

Sura ya 91. Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

    Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia. Iwapo umetambua jinsi ya kupata uzoefu katika hali zote, muktadha na mazingira, bila kushindwa hata kwenye mazingira ya kuchukiza zaidi, na iwapo katika mazingira mazuri kabisa na ya kustarehesha kabisa na katika hali za majaribu makubwa kabisa, haupotoshwi au kudanganyika na katu hauanguki, basi utakuwa umepiga hatua na kuzidisha kimo.

Umeme wa Mashariki | 75. Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

Umeme wa Mashariki | 75. Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu
Xiangwang Mkoa wa Sichuan
Ninahisi kuadibiwa sana moyoni mwangu kila mara ninapoona kwamba maneno ya Mungu yanasema: “Wanadamu dhalimu, wakatili! Kufumba macho na kula njama, kusukumana, kung’ang’ania sifa na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Mungu amezungumza maelfu na mamia ya maneno, ilhali hakuna hata mmoja ambaye amejifahamu. Wanatenda matendo kwa ajili ya familia zao na watoto wao, kazi zao, matarajio, hali katika jamii, majivuno na pesa, kwa sababu ya nguo, kwa sababu ya chakula na mwili—matendo ya nani kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao matendo yao ni kwa ajili ya Mungu, ni wachache tu wanaomfahamu Mungu.

2/16/2018

17 Ufahamu wa Kupata Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kupata Mwili
Bwana-Yesu, Kupata Mwili
Mwenyezi Mungu alisema, Kumjua Mungu kunapaswa kufanywa kupitia kwa kusoma neno la Mungu na kulielewa neno la Mungu. Watu wengine husema: "Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo nitawezaje kumjua Mungu?" Neno la Mungu kwa kweli ni maonyesho ya tabia ya Mungu. Kutoka kwa neno la Mungu unaweza kuuona upendo wa Mungu kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na jinsi Anavyowaokoa ... kwa sababu neno la Mungu linaonyeshwa na Mungu ikilinganishwa na Mungu kumtumia mwanadamu kuliandika.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Tatu

Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Ijapokuwa nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna aliyefahamu? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu. Kwa sababu Nimejivisha ubinadamu wa mwanadamu wa kawaida na kujivika ngozi ya mwanadamu, wanadamu hulitambua umbo Langu tu kwa nje ila hawatambui uhai uliomo ndani Yangu, wala hawatambui Mungu Roho, wanajua tu mtu wa mwili.

2/15/2018

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,wakristo

    Mwenyezi Mungu alisema,Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini. Ni juu yenu basi kuwasiliana ufahamu wenu kuhusu hizi mada

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,
3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
(Mat 18:12-14) Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi wale tisini na tisa, aende milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Na iwapo atapata kumwona, amini nawaambieni, anamfurahia huyo kondoo mmoja zaidi, kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni, kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.

2/14/2018

Upendo wa Mungu na wokovu | "Kutanafusi kwa Mwenye Uweza" Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho


Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake.

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 37. Kanuni Kuu za Jinsi Wafanyakazi Hufanya Kazi

    Katika kazi yao, wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mambo mawili: Moja ni kufanya kazi kabisa kulingana na kanuni zilizowekwa masharti na mipangilio ya kazi. Wafanyakazi hawapaswi kukiuka kanuni hizi, wasifanye kazi kulingana na mawazo yao wenyewe, na siyo kulingana na mapenzi yao. Wanapaswa kuonyesha uhusiano kwa kazi ya familia ya Mungu, na kuweka maslahi ya familia ya Mungu kwanza katika kila kitu wakifanyacho. Jambo jingine pia ni muhimu, na ni kwamba, katika kila kitu wakifanyacho, kuzingatia kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, na kufanya kila kitu kwa ukali kulingana na neno la Mungu.

2/13/2018

Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mtu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuwachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Kwa maneno mengine, binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa hiyo, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani.

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)

Tangu watu waanze kuikanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu.

2/12/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni. Tena, Nimeishi miongoni mwa binadamu, Nimeuhisi uchungu ulioko katika ulimwengu wa binadamu, Nimeona kwa macho Yangu hali zote tofauti zilizopo miongoni mwa wanadamu.

21 Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

 21 Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

     Mwenyezi Mungu alisema, Kama huna uzoefu wa kitu, basi wewe hakika hutajua jinsi ya kukisimamia na utakisimamia vibaya. Hata kama unakisimamia, na ufikiri: “Mimi nimeeleza kiasi haya yote na nikasema mengi kulihusu. Wao pia wamelisikiza mara nyingi. Nimeongea sana kulihusu. Nafikiri yote ambayo nimeshiriki kuhusu tatizo hili kimsingi ni kweli, sivyo?” lakini kwa kweli, yote tu ni mafundisho, na wewe unatumia mafundisho kutatua tatizo. Mbona unasema ni mafundisho? Kila neno unalosema ni sahihi, lakini kile unachosema hakijaelekezwa kwa tatizo na hakifikii kiini cha tatizo hili–ambapo tatizo hili lipo, shida yake ni nini, kwa nini hawa watu wanaweza kufanya mambo kama hayo au ni hali gani imejitokeza ndani yao.