2/24/2018

Umeme wa Mashariki | Njia… (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Njia… (4)  

Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu.

2/23/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. Nimetembea ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo.

Umeme wa Mashariki | Wimbo wa Mapenzi Matamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Nyimbo

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha

Wimbo wa Mapenzi Matamu

I

Kinani mwa moyo wangu, ni mapenzi Yako.
Ni matamu sana, nakaa karibu yako.
Kukutunza hukoleza moyo wangu;
kukutumikia na mawazo yangu yote.
Kuongoza moyo wangu, ni mapenzi Yako;
mimi hufuata nyayo zako za mapenzi.
Mimi hujisogeza kulingana na macho Yako;

2/22/2018

Best Swahili Christian Worship Song “Maisha Yetu Sio Bure”



UtambulishoMaisha yetu sio bure. Maisha yetu sio bure.




Leo tunakutana na Mungu, tunapitia kazi Yake.

Tumemjua Mungu katika mwili, wa utendaji na wa hakika.

Tumeiona kazi Yake, nzuri na ya ajabu.

Kila siku ya maisha yetu sio bure.

Tunamshuhudia Kristo kama ukweli na uzima!

Kufahamu na kukumbatia fumbo hili.

Umeme wa Mashariki | Njia… (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Umeme wa Mashariki |

Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja na Mimi: “Ee Mungu! Roho Wako aliye mbinguni awape neema watu walio duniani ili moyo Wangu uweze kukugeukia Wewe kikamilifu, kwamba Roho Yangu iweze kusisimuliwa Nawe, na kwamba Niweze kuona kupendeza Kwako ndani ya moyo Wangu na Roho Yangu, ili wale walio duniani wabarikiwe kuuona uzuri Wako.

2/21/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Mbili

Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Nilichunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu! Hivi vitu viko wazi kabisa Kwangu! Leo, sauti ya wokovu Wangu inapopazwa nje, je, kumekuwa na ongezeko la upendo wenu Kwangu? Je, sehemu ya uaminifu wenu Kwangu imekuwa safi?

2/20/2018

Sura ya 49. Unapaswa Kuutumia Ukweli Kumaliza Hali Yako Hasi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

    Mwenyezi Mungu alisema,Watu wengi wana hali hizi ambazo tumejadiliana hapo awali, hata ingawa si wazi kama hapo awali. Hii ni kwa sababu watu hawakuwa na ufahamu wowote wa ukweli wakati huo, na hawakuelewa chochote. Siku hizi, unasikiliza zaidi, na kwa kiwango cha chini kabisa, nyote mnaelewa baadhi ya mafundisho. Hata hivyo, una hali fulani zilizojikita ndani ambazo hazijafunuliwa. Una uwezo wa kuuona upotovu kwa wazi ambao mara nyingi hufunuliwa na kuwa na ufahamu mara tu unapofunuliwa; unajua asili ya malengo yako yaliyofunuliwa, maneno, na vitendo. Lakini sasa hivi, hujui mambo yaliyo ndani yako, mambo yaliyofichwa zaidi na vitu vinavyowasilisha asili ya kibinadamu.

Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Mwenyezi Mungu alisema, Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane kuhusu mada ya kumfuata Mungu.

2/19/2018

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

    Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu. Wanadamu wote wakitofautishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Ninayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Ninawauliza wakubali kazi Yangu katika siku za mwisho.Wakati uo huo, Ninawatofautisha wanadamu kulingana na aina, kisha Ninawatunukia au kuwaadhibu kila mmoja kulingana na matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuishwa katika kazi Yangu.Sasa Ninaishi duniani na Ninaishi miongoni mwa wanadamu.

2/18/2018

Swahili Christian Testimony Video "Utamu katika Shida" | Mungu Ndiye Nguvu Wangu


 Utambulisho

Han Lu ni kiongozi wa Kanisa la Mwenyezi Mungu katika China bara. Ameamini katika Mungu kwa zaidi ya muongo mmoja na amepitia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Anaelewa baadhi ya ukweli na anajua kwamba ni kupitia tu Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ndiyo mwanadamu ataweza kuwekwa huru kutoka dhambini na kuishi maisha yenye maana. Ametupa mbali kila kitu kumfuata Mwenyezi Mungu, na ametembea huku na huku na kushuhudia kuonekana kwa Mungu na kazi katika siku za mwisho. Hata hivyo, nchini China ambako chama cha kisiasa kikanamungu cha CCP kiko mamlakani, hakuna uhuru wa imani ya dini kwa vyovyote.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Neema

2. Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi

Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote kupitia sheria Zake kwa ajili ya viumbe vyote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao. Hii pia ni mada kubwa sana kwenu. Kuweka uwiano wa uhusiano kati ya vitu vyote—je, hiki ni kitu ambacho watu wanaweza kufanya? Binadamu wenyewe hawawezi. Watu wanaweza tu kuharibu.