2/27/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.

2/26/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu  

Je, ni vitu vipi vya asili ya mwanadamu? Unajua tu kuhusu upotovu wa mwanadamu, uasi, upungufu, dosari, fikra, na dhamira, lakini huwezi kugundua sehemu za ndani za asili ya mwanadamu—unafahamu tu safu ya nje, lakini huwezi kugundua chanzo chake. Baadhi hata hufikiri haya mambo ya juu kuwa ni asili ya mwanadamu, wakisema, “Tazama, ninaelewa asili ya mwanadamu; ninatambua ufidhuli wangu. Je, hiyo si asili ya mwandamu?” Je, haitoshi kuikubali kikanuni pekee? Ufidhuli ni kitu cha asili ya mwanadamu; huu ni ukweli kabisa. Je, kuelewa asili ya mtu binafsi ni nini? Inawezaje kujulikana? Je, inajulikana kutoka kwa vipengele vipi? Aidha, vitu hivi vinavyofichuliwa kutoka kwa vipengele hivi tofauti vinapaswaje kutazamwa kwa uthabiti? Tazama asili ya mtu kupitia shauku yake.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 20

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini

Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kwa wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakifuata halaiki ya watu, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kuimarisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana. Kwa sababu ya njia na desturi za mwanadamu zilizoanzishwa kitambo, miili ya watu wote imejawa na harufu ya udongo wa ardhini.Kwa sababu hii, binadamu amekuwa sugu; hana hisia zozote kwa ukiwa wa ulimwengu, na yeye badala yake hujishughulisha na kazi ya kujifurahisha katika dunia hii iliyoganda.

2/25/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)

Mwenyezi Mungu alisema, Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumfanyia kazi mwanadamu ili aweze kurudi katika asili yake na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani. Huu ushindi huja mapema katika mchakato wa kumfinyanga mwanadamu, ikiwa na maana kwamba ni hatua ya kwanza ya kazi. Kukamilisha ni hatua ya pili, au hitimisho la kazi. Kila mwanadamu ni lazima apitie hali ya kushindwa;

Sura ya 44. Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine 
Mwenyezi Mungu alisema,Ikiwa mnataka kufanya kazi nzuri katika kuwaongoza wengine na kuhudumu kama mashahidi wa Mungu, la muhimu zaidi, lazima uwe na ufahamu wa kina wa kusudi la Mungu katika kuwaokoa watu na kusudi la kazi Yake. Lazima uyaelewe mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake mbalimbali ya watu. Unapaswa kuwa mwenye utendaji katika juhudi zenu; upitie tu kiasi unachoelewa na kuwasiliana tu kile unachokijua. Usijisifu, usitie chumvi, na usiseme maneno yasiyopaswa. Ukitia chumvi, watu watakuchukia na utahisi mwenye kushutumiwa baadaye;

2/24/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (2)


Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako.

Umeme wa Mashariki | Njia… (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Njia… (4)  

Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu.

2/23/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. Nimetembea ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo.

Umeme wa Mashariki | Wimbo wa Mapenzi Matamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Nyimbo

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha

Wimbo wa Mapenzi Matamu

I

Kinani mwa moyo wangu, ni mapenzi Yako.
Ni matamu sana, nakaa karibu yako.
Kukutunza hukoleza moyo wangu;
kukutumikia na mawazo yangu yote.
Kuongoza moyo wangu, ni mapenzi Yako;
mimi hufuata nyayo zako za mapenzi.
Mimi hujisogeza kulingana na macho Yako;

2/22/2018

Best Swahili Christian Worship Song “Maisha Yetu Sio Bure”



UtambulishoMaisha yetu sio bure. Maisha yetu sio bure.




Leo tunakutana na Mungu, tunapitia kazi Yake.

Tumemjua Mungu katika mwili, wa utendaji na wa hakika.

Tumeiona kazi Yake, nzuri na ya ajabu.

Kila siku ya maisha yetu sio bure.

Tunamshuhudia Kristo kama ukweli na uzima!

Kufahamu na kukumbatia fumbo hili.

Umeme wa Mashariki | Njia… (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Umeme wa Mashariki |

Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja na Mimi: “Ee Mungu! Roho Wako aliye mbinguni awape neema watu walio duniani ili moyo Wangu uweze kukugeukia Wewe kikamilifu, kwamba Roho Yangu iweze kusisimuliwa Nawe, na kwamba Niweze kuona kupendeza Kwako ndani ya moyo Wangu na Roho Yangu, ili wale walio duniani wabarikiwe kuuona uzuri Wako.

2/21/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Mbili

Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Nilichunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu! Hivi vitu viko wazi kabisa Kwangu! Leo, sauti ya wokovu Wangu inapopazwa nje, je, kumekuwa na ongezeko la upendo wenu Kwangu? Je, sehemu ya uaminifu wenu Kwangu imekuwa safi?