5/12/2018

Umeme wa Mashariki | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Umeme wa Mashariki | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

    Mwenyezi Mungu alisema, Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. Moabu ilifukuzwa hadi nchi hii baada ya kulaaniwa. Ukoo wa wana wa Moabu umerithishwa mpaka leo, na ninyi nyote ni uzao wake. Hakuna kitu ambacho Ninaweza kufanya—nani aliyekusababisha uzaliwe katika nyumba ya Moabu? Ninakuhurumia na Siko radhi uwe hivi, lakini ukweli hauwezi kubadilishwa na watu.

5/11/2018

Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

Fu Jinhua alikuwa mzee wa kanisa la nyumba nchini China. Kama Wakristo wengine wengi, alijitolea kwa Bwana kwa shauku kubwa, na alifanya kazi kwa bidii katika kazi yake kwa ajili Yake. Alikuwa hasa mwenye kujiamini, na alijiona kuwa mtu ambaye alimpenda Bwana kweli. Baada ya kumfuata Bwana kwa miaka mingi, aliamini kwa moyo wote kwamba Biblia ilikuwa imefunuliwa na Mungu, na kwamba maneno katika Biblia yote yalikuwa maneno ya Mungu. Kwa hivyo, akilini mwake, alilinganisha kuamini katika Bwana na kuamini katika Biblia. Alidhani kwamba wale walioachana na Biblia hawakuweza kuitwa wafuasi wa Bwana. Pia aliamini kwamba alihitaji tu kufuata Biblia ili kuchukuliwa kuenda katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaposhuka na mawingu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Ingawa wale waliozaliwa katika enzi hii wametiishwa chini ya upotovu wa Shetani na mapepo wachafu sana, pia ni kweli kwamba wanaweza kupata wokovu mkuu kutokana na upotovu huu, hata mkubwa kuliko mifugo wanaotanda milima na tambarare na mali nyingi ya familia ambayo Ayubu alipata, na pia ni zaidi ya baraka ambayo Ayubu alipokea ya kumwona Yehova baada ya majaribu yake. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kupitia jaribio la kifo ndipo angeweza kuyasikia maneno ya Yehova na angeweza kusikia sauti Yake ya mshindo kutoka mawinguni. Hata hivyo, hakuuona uso wa Yehova na hakujua tabia Yake. Kile Ayubu alipata kilikuwa tu mali ya kimwili ambayo hutoa furaha za mwili na watoto wazuri mno katika miji jirani pamoja na ulinzi kutoka kwa malaika wa mbinguni.

5/10/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 21

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Mwenyezi Mungu alisema, Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa marejesho Yangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulukane waliko na gharika hii ya urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini mwandadamu hajawahi kunitabua;

Christian Testimony Video Swahili "Moyo Uliopotea Waja Nyumbani" Wokovu wa Ajabu wa Mungu


Tangu alipokuwa mdogo, Novo alimwamini Bwana Yesu, kama mama yake tu. Hata kama alisoma Biblia, kuomba, na kuhudhuria mahubiri mara kwa mara, mara nyingi hangeweza kujizuia bali kufuata mielekeo mibaya ya dunia, kutamani raha za mwili, na kudanganya na kusema uwongo…. Alikusudia mara nyingi kuyaacha maisha ya aina hiyo ya kuzunguka katika kutenda dhambi na kukiri, kukiri na kutenda dhambi. Hata hivyo, kila wakati hakufaulu. Baadaye Novo alipokuwa akifanya kazi nchini Taiwan alisikia injili ya ufalme, na kwa kuyasoma maneno Yake Mwenyezi Mungu alifikia hitimisho kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu, na kuwa kazi Yake ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho ina uwezo wa kusuluhisha kikamilifu tatizo la asili ya mwanadamu ya dhambi.

5/09/2018

Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?

Kristo wa siku za mwisho amekuwa akifanya kazi Yake nchini China kwa zaidi ya miaka 20, kazi ambayo imetetemesha makundi mbalimbali ya kidini kwa kina. Swali la kufadhaisha zaidi kwa jumuiya za kidini wakati huu limekuwa: Wachungaji wengi na wazee wa kanisa katika jumuiya ya kidini wamefanya liwezekanalo kuuhukumu na kuushambulia Umeme wa Mashariki kupitia njia mbalimbali kama vile kueneza uvumi kuhusu na kuukashifu Umeme wa Mashariki. Zaidi ya hayo, hata wamezingia makanisa yao na hata kuthubutu kushirikiana na serikali ya CCP kuwakamata na kuwatesa Wakristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu.

Umeme wa Mashariki | Kuibuka kwa Marekani na Misheni Yake

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kumfuata Mungu
Wapuriti walitetea dhana za uhuru, usawa, na demokrasia pamoja na mafundisho ya Mungu. Pia walichanganya Azimio la Uhuru la Marekani na Katiba ya Marekani na mambo haya. …Kwa hiyo Wapuriti hakuwa tu kiini cha uanzishwaji wa Marekani, lakini pia walikuwa waasisi walioifanya Marekani kuwa kuu.…Marekani imetekeleza jukumu muhimu katika kuimarisha hali ya kimataifa na kusawazisha utaratibu wa dunia. Jukumu hili haliwezi kufidika katika kulinda na kuimarisha hali ya kimataifa.
Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida.

5/08/2018

Sura ya 19. Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anapata mwili ili ateseke kwa niaba ya mwanadamu, na kwa kufanya hivyo atasababisha hatima iliyo ya ajabu ambayo itafuata kwa ajili ya mwanadamu. Hatua hiyo ya kazi iliyokamilishwa na Yesu ilikuwa tu kuwa Kwake mfano wa mwili wenye dhambi na kusulubiwa, kuhudumu Kwake kama sadaka ya dhambi na kuwakomboa wanadamu wote, na hii iliweka msingi wa kuingia kwa baadaye kwa mwanadamu katika hatima iliyo ya ajabu. Alizichukua dhambi zote za mwanadamu juu Yake na akawa mfano wa mwili wenye dhambi na akasulubiwa; Alisulubiwa kwa niaba ya wanadamu wote, na baada ya hapo wanadamu wote walikombolewa.

Umeme wa Mashariki | Kuibuka kwa Falme ya Uingereza Ikiendesha Maendeleo ya Wanadamu

     Wakati wa upanuzi wa kikoloni wa Uingereza, elimu na kuwaza kwa hali ya juu katika nyanja kama vile mifumo ya kisiasa ya Magharibi, utamaduni, dini, elimu, na dawa zilianzishwa katika koloni. Utaratibu wa zamani wa kutawala wa nchi zilizotiwa ukoloni ulipinduliwa, na itikadi zilizokuwepo kabla za kikabaila ziliangamizwa. Hili liliweka msingi kwa koloni bila kujua kuanzisha njia ya demokrasia ya kikatiba…
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mungu
    Mwenyezi Mungu alisema, Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu.

5/07/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (4)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (4)

Amani na furaha Nizungumziayo leo sio sawa na yale ambayo unaamini na kufahamu. Ulikuwa ukifikiri kwamba amani na furaha yalimaanisha kuwa na furaha siku nzima, kutokuwako kwa magonjwa au misiba katika familia yako, kuwa mwenye furaha kila mara ndani ya moyo wako, bila hisia zozote za huzuni, na furaha isiyoelezeka ndani yako haijalishi kiasi cha urefu wa maisha yako mwenyewe. Hilo lilikuwa ni pamoja na nyongeza katika mshahara wa mume wako na mwanao kuingia katika chuo kikuu karibuni.

AmaJuda Eya Ekudingisweni Kwelinye Izwe Kanye Nokusabalaliswa Kwevangeli Lombuso Wezulu

Ngo-70 A.D., iminyaka engamashumi amathathu nesikhombisa emva kokuvuka nokwenyukela ezulwini kweNkosi uJesu, impi yamaRoma yathumba iJerusalema. Futhi abafuduki bamaJuda bazula emhlabeni emva kokukhishwa ezweni lakwa-Israyeli. Noma babelahlekelwe yizwe labo, bahamba bephethe ivangeli leNkosi uJesu lombuso wezulu elalikade livaleleke eJudiya base belisabalalisa kuwo wonke amagumbi omhlaba.

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili
Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa njia timilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu.

5/06/2018

Swahili Gospel Movie "Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni"


Song Ruiming ni mchungaji wa kanisa huko Korea Kusini. Kama mfuasi wa dhati wa Bwana kwa miaka mingi, amekuwa akifuatilia imani yake kwa bidii sana na kumfanyia kazi Bwana huku akisubiri kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa akihisi kuchanganyikiwa sana na mwenye udhaifu anapokuwa akiona kwamba Kanisa halina kazi ya Roho Mtakatifu na linazidi kuwa na ukiwa. Hapo ndipo aliposikia kuhusu dhehebu kwa jina la Umeme wa Mashariki linaloibuka nchini China ambalo linashuhudia kurudi kwa Bwana YesuMwenyezi Mungu, ambaye Anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho kwa kuonyesha ukweli. Hivyo Song Ruiming na mhubiri Cui Cheng'en walisafiri kwenda China kujifunza Umeme wa Mashariki, ambapo hatimaye waliyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na kugundua kwamba maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, sauti ya Mungu!

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Kanisa la Mwenyezi Mungu hunyunyizia na kuwaongoza waumini wake kwa mujibu kamili wa maneno ya Mungu katika Biblia na Neno Laonekana Katika Mwili yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ili kwamba kila muumini anaweza, chini ya uongozi, utolewaji, unyunyiziwaji, na uongozwaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, kuelewa ukweli wote katika maneno ya Mungu, kumiliki mtazamo sahihi juu ya maisha na maadili, kuwa na malengo sahihi ya kufuatilia, kufuata njia ya Mungu, kushikilia maagizo ya Mungu, kumtukuza Mungu kwa kuwa nuru na chumvi ya dunia, na kusifiwa na Mungu, na kuwa na sifa kamili kurithi ahadi za Mungu.