Mwenyezi Mungu alisema, Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, "kuingia" kwa mwanadamu[1] pia kumefikia kilele chake.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sitapumbazwa Tena na "Nia Njema"
Meng Yu Mji wa Pingdingshan, Mkoa wa Henan
Wakati mmoja nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, niliona kuwa ndugu fulani alikuwa akijaribu kuwafurahisha dada zake, maonyesho ya hali mbovu ya tabia yake machoni mwangu. Niliamua kutafuta fursa ya kumkumbusha haya mambo. Siku zilipita na nikaona utendaji wake wa wajibu ulikuwa wenye matokeo machache mazuri—ushahidi wa maoni yangu ya awali kumhusu.