
Liu Heng Mkoa wa Jiangxi
Kupitia neema na kuinuliwa kwa Mungu, nilichukua jukumu la kuwa kiongozi wa kanisa. Wakati huo, nilikuwa na shauku mno na niliweka azimio mbele ya Mungu: Bila kujali kinachonikabili, sitayatelekeza majukumu yangu. Nitafanya kazi vizuri na yule dada mwingine na nitakuwa mtu anayetafuta ukweli. Lakini nilikuwa nimeamua tu, na sikujua jinsi ya kuingia katika uhalisi wa uhusiano wa kufanya kazi kwa mpangilio wa kuridhisha.
