Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi Na Nane
Maneno yote ya Mungu yana sehemu ya tabia Yake; tabia Yake haiwezi kuonyeshwa kwa ukamilifu kwa maneno, kwa hiyo hii inaonyesha kiasi gani cha utajiri kiko ndani Yake. Kile ambacho watu wanaweza kukiona na kukigusa ni, hata hivyo, finyu, kama ulivyo uwezo wa watu. Ingawa maneno ya Mungu ni dhahiri, watu hawawezi kuyaelewa kwa ukamilifu. Kama maneno haya tu: "Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja.
