4/04/2019

Neno la Mungu | Sura ya 34

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote , mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli kabisa! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vikasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi.

4/03/2019

Video ya Injili 2018 | "Kutoka Kinywani mwa Mauti" | Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha



Video ya Injili 2018 | "Kutoka Kinywani mwa Mauti" | Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Liu Zhen, mwenye umri wa miaka 78, ni mke wa nyumbani wa kawaida wa mashambani. Baada ya kumwamini Mungu, alihisi furaha isiyo na kisawe na kusoma maneno Yake na kuimba nyimbo za kumsifu siku zote, na mara nyingi kukusanyika pamoja na ndugu zake kushirikiana juu ya ukweli. ... Hata hivyo, mambo mazuri hayadumu. Anakamatwa na kuteswa na serikali ya Kikomunisti ya China, ikimtia katika shida mbaya sana. Polisi wanampeleka kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kuhojiwa mara tatu, na kumwonya asimwamini Mungu tena.

4/02/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo.

4/01/2019

Wimbo wa Injili | Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Nyimbo

Wimbo wa Injili | Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

I
Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu
wanaomwabudu na kumtii Yeye.
Ingawa wamepotoshwa na Shetani,
hawamwiti baba tena.
Wanajua ubaya wa Shetani, hivyo wanamkataa.
Wanakuja mbele ya Mungu, wanakubali adabu na hukumu.
Wanajua kile kilicho kibaya,
na kile ambacho ni kitakatifu.

3/31/2019

3. Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe.

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake

3. Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe.

Maneno Husika ya Mungu:
Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika.

3/30/2019

1.Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake

1. Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu.

3/29/2019

Swahili Gospel Movie "Vunja Pingu Na Ukimbie" | Bwana ni Mchungaji Wangu



Lee Chungmin alikuwa mzee wa kanisa fulani huko Seoul, Korea ya Kusini. Kwa zaidi ya miaka ishirini, alimtumikia Bwana kwa shauku kubwa, akamakinika kikamilifu juu ya kusoma Biblia. Akifuatia mfano wa viongozi wake wa kidini, alidhani kuwa kumwamini Bwana kulimaanisha kuiamini Biblia, na kwamba kuwa na imani katika Biblia kulikuwa sawa kabisa na kuwa na imani katika Bwana. Aliamini kwamba almuradi angeshika Biblia, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Dhana hizi zilimbana kama jozi ya pingu, zikimzuia kufuata nyayo za Mungu na kumwamini Mungu. 

3/28/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu"



Mwenyezi Mungu anasema, "Kama huelewi tabia ya Mungu, basi itakuwa haiwezekani kwako wewe kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, ndivyo pia haitawezekana kubakiza hali ya kumcha na kumwogopa Yeye, utakuwa ni uzembe na kuepuka kusema ukweli wote kwa kutojali, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, ilhali hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakinifu au kudadisi suala hili.

3/27/2019

Wimbo wa Dini | Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,nyimbo
I
Kazi ya Mungu inaendelea kuwa bora;
ingawa kusudi linabaki bila kubadilika,
mbinu ya kazi Yake inabadilika daima,
na hivyo pia wale wanaomfuata.
Kadiri ambavyo Mungu anafanya kazi zaidi,
ndivyo anavyozidi mwanadamu kumjua, kikamilifu,
ndivyo tabia ya mwanadamu inavyozidi kubadilika
pamoja na kazi Yake ifaavyo.
Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa;

3/26/2019

Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Mungu


I
Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu,
lazima tutafute mapenzi ya Mungu,
tutafute maneno ya Mungu na matamshi ya Mungu,
tutafute maneno ya Mungu na matamshi Yake.
Kwani palipo na maneno mapya ya Mungu,
pana sauti ya Mungu, sauti Yake;
palipo na nyayo za Mungu,
pana matendo ya Mungu, matendo ya Mungu.

3/25/2019

Kwa Nini Mungu Anapata Mwili Kufanya Kazi Yake katika Siku za Mwisho | Swahili Christian Movie Clip 3/6


"Nimewahi Treni ya Mwisho" (3) : Kwa Nini Mungu Anapata Mwili Kufanya Kazi Yake katika Siku za Mwisho 


Katika zile siku za mwisho, Bwana amerejea katika mwili kueleza ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu kuanzia na familia ya Mungu. Hata hivyo, ndugu wengi katika Bwana wanaendelea kuamini kwamba Yehova alifanya kazi kama Roho katika Agano la Kale na katika siku za mwisho Mungu ataendelea kufanya kazi katika umbo la Roho bila haja yoyote ya kupata mwili. Hivyo kwa nini Mungu anakuwa mwili ili kufanya kazi Yake katika siku za mwisho? Je, Roho wa Mungu hawezi kufanya kazi hii? Kuna tofauti gani kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya Roho?

Sikiliza zaidi:  New Swahili Gospel Movie "Jina la Mungu Limebadilika?!" | Kufunua Siri ya Jina la Mungu

3/24/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 18


         Kujenga kanisa si kitu rahisi cha kufanya! Niliweka moyo Wangu wote katika kulijenga na Shetani angefanya kila kitu ingeweza kuibomoa. Kama unataka kujengwa lazima uwe na maono; lazima uishi maisha kwa Mimi, kuwa shahidi wa Kristo, shikilia Kristo juu kwa juu, na kuwa mwaminifu Kwangu. Hupaswi kutoa visingizio, lakini badala yake kutii bila ya sharti; lazima uvumilie majaribu yoyote, na kukubali yote yanayotoka kwa Mimi.

3/23/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | Sura ya 20

Kazi ya Roho Mtakatifu hushina mbele, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yako. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya mioyo yenu na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya.