11/27/2019

Mtu anafaaje kutenda kuingia kuwa mtu mwaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole.
kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili

11/26/2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtu mwaminifu na mtu mdanganyifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.
kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

11/25/2019

Mtu mdanganyifu ni nani? Kwa nini watu wadanganyifu hawawezi kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:
Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.
kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

11/24/2019

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu.
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

11/23/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” Mambo Muhimu 2: Kusherehekea Kuja kwa Mungu | Wimbo wa Kuabudu



Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” Mambo Muhimu 2: Kusherehekea Kuja kwa Mungu | Wimbo wa Kuabudu


Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?


Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?


11/22/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” Mambo Muhimu 1: Sherehe ya Ufalme | Wimbo wa Kuabudu


Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” Mambo Muhimu 1: Sherehe ya Ufalme | Wimbo wa Kuabudu


Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?


Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?

11/21/2019

Wimbo wa dini | "Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake"


Wimbo wa dini | "Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake"


Ni Wakati tu Mungu anapojinyenyekeza kwa kiwango fulani,


kumaanisha Anakuwa mwili ili kuishi kati ya wanadamu,


ndipo wataweza kuwa wasiri Wake,


ndipo watakuwa marafiki Zake wa karibu.


Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu


Wakati Mungu ni wa Roho, metukuka na mgumu kumwelewa?


Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu


mwanadamu ataweza mapenzi Yake, na kupatwa na Yeye.

11/20/2019

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu. Baada tu ya kuutoa moyo wako mzima katika Mungu ndipo utaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho hatua kwa hatua. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu.

11/19/2019

Inamaanisha nini kuomba kwa kweli?

Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema. Hii ndiyo maana ya kuomba kwa kweli. Baada ya kuomba kwa kweli, moyoni mwako utahisi kuwa na amani, na kufurahishwa; nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka, na utahisi kwamba hakuna kitu chochote katika maisha yako yote kinachostahili au ni muhimu zaidi kuliko kumpenda Mungu—na yote haya yatathibitisha kuwa maombi yako yamekuwa yenye ufanisi.

11/18/2019

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | "Upendo Safi Bila Dosari" (Lyrics Video)

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | "Upendo Safi Bila Dosari" (Lyrics Video)


I

Upendo ni hisia safi, safi bila dosari.

Tumia moyo, tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga.

Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki,

hutazamii kupata kitu, cha malipo.

Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

11/17/2019

Watu wanafaa kupitiaje hukumu na adabu ya Mungu ili kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:

Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu.Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. 

11/16/2019

Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Maneno Husika ya Mungu:

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

11/15/2019

Hukumu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.