Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya
kanisa, kula na kunywa
maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme. Sala za mtu wa aina hii,
nyimbo zake, na kula na kunywa kwake maneno ya Mungu yote yanafuata amri, wanalazimika kufanya hayo, na yanafanyika katika kufuata mitindo, hayafanyiki kwa hiari wala kufanyika kutoka moyoni. Haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanaomba au kuimba, hakutakuwa na matokeo kamwe, kwa sababu yote wanayofanya ni amri na mila za kidini, na wao hawatendi neno la Mungu. Kwa kulenga tu mbinu, na kuchukua maneno ya Mungu kama amri ya kuhifadhi, mtu wa aina hii hatendi neno la Mungu, bali tu anaridhisha mwili, na anafanya vitu ili kujionyesha kwa wengine. Aina hii ya matambiko ya dini na amri yanatoka kwa mwanadamu, si kwa Mungu. Mungu hahifadhi sheria, Hazingatii sheria yoyote; Anafanya mambo mapya kila siku na Anafanya kazi ya vitendo. Kama watu katika Kanisa la Nafsi Tatu ambao wamewekewa mipaka kwa ulinzi wa kila asubuhi, sala ya jioni, kutoa shukrani kabla ya kula, kuonyesha shukrani katika kila kitu, na matendo mengine kama haya, haijalishi ni kiasi gani watu hawa wanafanya, au muda wanatenda, hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama watu huishi ndani ya amri, na mioyo yao ikiwa katika vitendo, basi Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi, kwa sababu mioyo ya watu inachukuliwa na amri, inachukuliwa na dhana za kibinadamu; kwa hiyo Mungu hana njia ya kufanya kazi; watu daima watakuwa wakiishi tu chini ya utawala wa sheria, mtu wa aina hii kamwe hataweza kupokea sifa za Mungu.