1/25/2018

Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Mwenyezi Mungu alisema,Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Wewe daima huainisha vitabu hivi au vifaa hivyo, na hivyo unapata umiliki wa kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini huwaje unapomaliza kusema? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu na hawana ufahamu wao wenyewe pia. Mwishowe, vitu vyote watakavyokuwa wamepata ni fomyula na sheria. Unaweza kuzungumza juu ya mambo hayo lakini hakuna kitu kingine, hivyo kama Mungu akifanya jambo jipya, je, mafundisho yote unayoyajua yanaweza kufanana na kile Mungu anachofanya? Kwa hiyo, mambo hayo yako ni sheria tu na wewe unawafanya watu wajifunze theolojia tu: Wewe huwaruhusu kupitia neno la Mungu au kupitia ukweli. Hivyo vitabu hivi ambavyo unavipitia vinaweza kuwaleta watu kwa teolojia na ujuzi tu, katika fomyula mpya na katika sheria na mila. Haviwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, au kuwaruhusu watu kuuelewa ukweli au kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kuuliza swali baada ya swali kuhusu maneno hayo, kisha kujibu, wafanya kielelezo au muhtasari, na unadhani kuwa wale walio chini wanaweza kuelewa kwa urahisi. Mbali na kuwa rahisi kukumbuka, wao wana uhakika juu ya maswali haya kwa tazamo la haraka, na unafikiri ni vizuri kufanya mambo kwa njia hii. Lakini kile wanachokielewa siyo maana iliyokusudiwa; inatofautiana na ukweli na ni maneno ya mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Unafanya mambo haya kuwaongoza watu kuelewa ujuzi na weledi wa elimu. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate Mungu na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, si wewe ni sawa tu na Paulo? Ninyi hufikiri kwamba kupata weledi wa ujuzi wa ukweli ni muhimu hasa, na pia kujifunza kwa moyo mafungu mengi ya maneno ya Mungu. Lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Ninyi hudhani ni muhimu sana kwa watu kuweza kukariri mengi ya maneno ya Mungu, kuweza kuzungumza mafundisho mengi na kugundua fomyula nyingi ndani ya maneno ya Mungu. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili kila mtu awe akiimba wimbo mmoja na kusema mambo hayo hayo, ili kila mtu aongee mafundisho sawa na wengine, awe na maarifa sawa na huweka sheria sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi hufanya hivi kana kwamba kuwafanya watu waelewe vizuri zaidi, wakati kwa kinyume chake hamjui kwamba kwa kufanya hivi mnawaingiza watu katikati ya sheria ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu. Ili kuwafanya watu wawe na ufahamu halisi, ni lazima ujiunge na uhalisi, jiunge na kazi, na uwalete watu mbele ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ambapo watu wanaweza kuwa na weledi wa ukweli. Ikiwa jitihada zako zinaelekezwa tu kwa kutumia fomyula na sheria kwa maneno yaliyoandikwa, basi hutaweza kufikia ufahamu wa kweli, hutaweza kuwaongoza wengine kwa uhalisi, na seuze kuweza kuwaruhusu wengine kupitia mabadiliko zaidi au kujielewa wenyewe zaidi. Kama neno lililoandikwa lingekuwa badala ya watu, basi hamngehitaji kufanya chochote kamwe. Nyinyi bado hamjagundua sheria za maneno ya Mungu, na watu wengi husema hivi: "Hakuna mantiki kwa maneno ya Mungu. Kila makala ina ya maudhui ya aina zote na kuna maana tofauti katika kila kifungu na kila sentensi hali inayofanya kuwa vigumu kwetu kukumbuka na vigumu kuelewa. Hata siyo rahisi kufupisha wazo la jumla la ibara. "Neno la Mungu siyo riwaya, wala si nadhari au kazi ya fasihi. Ni ukweli; ni neno ambalo humpa mtu uzima. Neno silo jambo ambalo linaweza kueleweka kwa kufikiriwa kwa akili zenu, wala sheria zake haziwezi kufupishwa kwa juhudi kidogo. Kwa hiyo bila kujali ni kipengele kipi watu wana ufahamu mdogo wacho au wana ufahamu wa sheria zake, inaweza tu kuwa ufahamu wa upande mmoja, wa juu juu tu, kama tone moja tu katika bahari, na kimsingi hauwezi kufikia kile alichokusudia Mungu awali. Makala yoyote ya maneno ya Mungu itakuwa na vipengele kadhaa vya ukweli. Kwa mfano, makala kuhusu fumbo la Mungu kupata mwili itajumuisha umuhimu wa kupata mwili pamoja na kazi inayofanywa na upataji wa mwili. Na pia itakuwa na jinsi watu wanavyopaswa kuamini katika Mungu, na labda inaweza pia kuwa na jinsi watu wanavyopaswa kumwelewa na kumpenda Mungu; itajumuisha mambo mengi ya ukweli. Kama, kwa mujibu wa mawazo yako, umuhimu wa kupata mwili ulikuwa na vipengele vichache tu na unaweza kujumlishwa katika sentensi chache, ni matokeo yapi ambayo kazi ya Mungu kwa mtu yangeweza kufanikisha? Watu hufanywa kuelewa umuhimu wa kupata mwili ili kuwafanya wamwelewe Mungu. Baada ya mtu kumwelewa Mungu, kwa kawaida anakuwa na moyo ambao humcha Mungu, na hili sasa linahusisha matendo ya mtu. Hivyo hakuna kipengele cha maneno ya Mungu na hakuna kipengele cha ukweli kilicho rahisi kama unavyofikiria. Ikiwa wewe hutazama neno la Mungu na lugha ya Mungu kuwa rahisi, ukifikiri kwamba swali lolote linaweza kujibiwa kwa ibara, basi huo si ukweli. Kila makala ina mitazamo mingi ambayo maneno ya Mungu huzungumzwa kwayo na hakuna njia ya watu kufupisha au ya kutoa muhtasari wa maneno yake. Angalieni yale ambayo mliyatolea muhtasari. Unafikiri fungu hili limejibu swali lililo hapo juu, lakini fungu hili pia linahusiana na maswali mengine. Kwa hiyo unasema nini kwa hilo? Ukweli una mambo mengi. Kwa nini husemwa kuwa ukweli ni uzima, kwamba unaweza kuleta starehe kwa mtu, kwamba hauwezi kupitiwa kwa ukamilifu wake kwa aushi kadhaa au miaka mia kadhaa? Kwa mfano ulikuwa uvitolee muhtasari baadhi ya vipengele vya ukweli au kifungu fulani cha maneno ya Mungu, halafu uulize swali kulihusu hilo. Kisha, kuzingatia swali hili, ulikuwa usome kifungu hiki, kisha ingekuwa dhahiri kuwa hiki kifungu kimesomwa kwa kulijibu swali hilo. Kwa hiyo kifungu hiki kimekuwa fomyula, kanuni na mafundisho, na si ukweli. Ingawa hakuna hata moja ya maneno ya awali limebadilika, hiki kwa dhahiri sana ni kipande cha mafundisho, na sio ukweli. Kwa nini? Kwa sababu swali ulilouliza uliliuliza vibaya. Liliwaongoza watu kupotea na kuwaingiza katika mafundisho, likawafanya kufikiri, kuwaza, kufikiria swali hili, na walisoma kifungu hiki kwa mujibu wa mafundisho yako, kukisoma wakitumia mtazamo wako wa mafundisho. Kisha wangekisoma tena na kurudia, wakiona swali moja pekee na bila kuona kitu kingine chochote. Mwishowe wao wangeletwa mahali ambapo hawawezi kupata ukweli na hawawezi kupitia neno la Mungu, mahali ambapo wanaweza kujiandaa tu na kujadili mafundisho na ni mahali ambapo hawawezi kumwelewa Mungu. Yote ambayo wangeweza kuzungumza yangekuwa mafundisho yenye kupendeza, mafundisho sahihi, lakini hakungekuwa na uhalisi ndani yao na hawangekuwa na njia ya kutembelea. Aina hii ya kuongoza kweli hufanya madhara makubwa! Ni nini mwiko mkubwa katika huduma ya mtu kwa Mungu? Unajua? Wale miongoni mwenu ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli mlivyo viongozi wakuu. Hata hivyo, nyinyi hamzingatii kufahamu ukweli na kuingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Nyinyi daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi? Wengine hata husema: "Kwa kufanya hivi nina uhakika kwamba Mungu atafurahi sana; Yeye kweli atapenda sana. Wakati huu nitaacha Mungu aone, kumpa Yeye mshangao mzuri. "Mshangao huu inavyoonekana si tatizo, lakini unaondolewa kutokana na haya! Lakini usifanye tu chochote kijacho akilini mwako bila kufikiri. Je, inawezaje kuwa sawa kutozingatia matokeo hayo? Wakati wale kati yenu ambao huudhi tabia ya Mungu na kuziudhi amri Zake za utawala wataondolewa wakati huo, hakutakuwa na maneno mnayoweza kusema. Bila kujali dhamira yako, bila kujali kama wewe hufanya hivyo kwa makusudi au la, kama wewe huelewi tabia ya Mungu au huyaelewi mapenzi ya Mungu, kwa urahisi utamkosea Mungu na kwa urahisi utaziudhi amri Zake za utawala: Hiki ni kitu ambacho kila mtu ni lazima ajichunge dhidi yake. Mara unapoziudhi amri za utawala za Mungu au kuiudhi tabia ya Mungu, Mungu hataangalia kama ulifanya hivyo makusudi au bila kukusudia; hiki ni kitu ambacho ni lazima uone kwa dhahiri. Ikiwa huwezi kuona ukweli halisi wa suala hili, basi unahakikishiwa kuwa na tatizo. Katika kumhudumia Mungu, watu wanataka kupiga hatua kubwa, kufanya mambo makubwa, kusema maneno makubwa, kufanya kazi kubwa, kuchapisha vitabu vikubwa, kufanya mikutano mikubwa na kuwa viongozi wakuu. Kama siku zote una matarajio makuu, basi utaziudhi amri kuu za utawala za Mungu; watu kama hawa watakufa haraka. Kama wewe si mtiifu, mwenye kumcha Mungu au mwenye busara katika kumhudumia Mungu, ipo siku utaziudhi amri za utawala za Mungu. Kama ukikosea tabia ya Mungu, kuziudhi amri Zake za kiutawala, na hivyo kutenda dhambi dhidi ya Mungu, basi Yeye hataangalia kuona ni kwa sababu gani ulitenda hivi, wala kuona nia zako, hivyo mniambie Mimi, je, Mungu hana busara? Je, Yeye amekosa huruma kwa mwanadamu? Hapana. Kwa nini Mimi Ninasema hapana? Kwa sababu wewe si kiziwi, mjinga au kipofu. Nyote mnaweza kuona na kusikia, na bado mnasababisha kosa. Ni sababu gani unaweza kuizungumzia bado? Hata kama wewe huhifadhi nia zozote, mara unapomkosea Mungu, lazima utaangamia na kupata adhabu. Kuna haja ya hali yoyote yako izingatiwe? Hakuna mtu yeyote anayelazimishwa kwa kisu kuzikosea amri za utawala za Mungu au tabia ya Mungu. Hili halifanyiki kamwe. Mtu alikuwekea kisu kooni na kukulazimisha, akisema: "Mlaani Mungu wenu. Baada ya kumlaani Yeye nitakupa pesa na sitakuua. "Labda katika hali aina hii ungesema maneno ya kukufuru kwa sababu tu unaogopa kufa. Je, hali ya aina hii inaweza kutokea? Mambo huwa hayafiki kiwango hiki, ama hufika? Kwamba tabia ya Mungu haitaruhusu kosa ina maana yake iliyodokezwa. Hata hivyo adhabu za Mungu zinategemeza hali za watu na asili zao. Hali moja ni pale ambapo mtu hajui kuwa Yeye ni Mungu naye humkosea Yeye. Kujua kwamba Yeye ni Mungu na bado kumkosea Yeye kwa makusudi ni hali nyingine. Ikiwa mtu anafahamu kikamilifu kwamba Yeye ni Mungu na bado humkosea, basi mtu huyo ni lazima aadhibiwe. Mungu huonyesha kiasi cha tabia Yake katika kila hatua ya kazi Yake—watu wanafahamu chochote kwa hili? Yeye amefanya kazi kwa miaka mingi, watu wanajua tabia Yake na ni vitu vipi ambavyo watu hufanya au kusema ambavyo vinaweza kumchukiza Mungu kwa urahisi? Na vitu ambavyo vimefafanuliwa na amri za utawala za Mungu—kile watu wanapaswa kufanya na kile hawapaswi kufanya—Je, watu hawajui hayo pia? Watu hawawezi kuelewa mambo fulani ambayo yanahusiana na ukweli au na kanuni. Hiyo ni kwa sababu hawajapitia kufikia kiwango hicho, na hivyo hawana njia ya kuelewa. Lakini amri za utawala za Mungu ziko ndani ya mawanda yaliyofafanuliwa na yanastahili kuwa ya sheria. Sio lazima kwa watu kuzielewa kwa njia yoyote, ni kwamba tu wafuate maana yazo halisi. Je, si hili ni jambo ambalo mtu sharti apambane nalo? Wewe huzingatii zaidi kitu chochote na humwogopi Mungu, kwa hiyo ni lazima upate adhabu!

Haya ndiyo maisha ambayo yanastahili ubinadamu wa kawaida, ilhali watu wanayaona kama kitu kinachochukiwa na Mungu. Utendaji wao tu ni wao kufuata kanuni chache, na hii huwasababisha kuishi maisha yanayochosha sana, bila maana yoyote. Katika hali halisi, Mungu hajawahi kumhitaji mtu kufanya hivyo. Watu wanataka kukatiza tabia zao wenyewe, wakiomba bila kukoma katika roho zao ili wawe karibu na Mungu, mawazo yao daima yakiwa yamemilikiwa na kufikiria kuhusu mambo ya kimungu, macho yao mara kwa mara yakiangalia huku na kule, wakiangalia suala hili na suala lile, wakihofia kwa kiasi kikubwa kwamba uhusiano wao kwa Mungu utatengwa kwa namna fulani. Haya ni mambo yote ambayo mtu amejijumlishia mwenyewe; ni sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya mtu na mtu wenyewe. Usipoelewa kiini chako mwenyewe au kile kiwango ambacho mwenyewe unaweza kufikia, basi hutakuwa na namna yoyote ya kufahamu hasa viwango ni vipi ambavyo Mungu anahitaji kwa ajili ya mtu, na basi hutakuwa na namna yoyote ya kupata matendo ambayo yanatekelezwa katika hatua mwafaka. Akili yako daima inageuka upande huu na ule, unafikiria kila namna iwezekanayo kujifunza na kuhisi njia yako jinsi gani unaweza kusisimuliwa na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu, na matokeo kwamba unaweka muhtasari seti za njia za kutenda ambazo unadhani zitakusaidia kupata kuingia. Unapotenda kwa njia hii, hujui nini hasa ambacho Mungu anataka kutoka kwako; unatenda tu kwa njia yako mwenyewe, ukihisi starehe kabisa, bila kujali kuhusu matokeo wala kujali hata kidogo kuhusu iwapo kupotoka na makosa yapo. unapoendelea kwa njia hii, kutenda kwako kunakosa mambo mengi makubwa, kama vile pongezi ya Mungu, uthibitisho na Roho Mtakatifu na matokeo yanayopatikana kwa matakwa ya Mungu. Hata inakosa ubinadamu wowote wa kawaida au hisia za kawaida za mtu za mantiki. Kutenda kwako ni kufuata sheria tu, au kwamba uendelee kuongeza mzigo wako kimakusudi ili ujizuie, ili ujidhibiti. Na hata unafikiri kuwa kutenda kwako kuko sahihi, bila kujua kwamba sehemu kubwa ya kile unachotenda ni mchakato au utunzaji ambao si lazima. Kuna wengi ambao wanatenda hivi kwa miaka mingi bila mabadiliko kimsingi katika tabia zao, bila ufahamu mpya, na bila kuingia kupya. Wanazitekeleza kwa kutojua asili zao za kinyama, hata hadi hatua ambapo kuna mara nyingi wakati wanafanya mambo bila busara, mambo ya kinyama na mara nyingi wakifanya mambo ambayo huwapa watu kusita na ambayo hayaeleweki. Je, si aina hii ya mtu ni mtu ambaye amebadilika?
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni