Christian Video Swahili "Uaminifu ni wa Thamani Mno" | Wokovu wa Bwana
Zhen Cheng alikuwa mmiliki wa duka la urekebishaji wa vifaa vya stima. Alikuwa mkarimu, mwaminifu, na alifanya biashara inavyopasa kufanywa. Hangejaribu kumdanganya mtu, lakini alikuwa anachuma tu pesa za kutosha angalau kuimudu tu famillia yake. Baada ya muda, mmoja wa jamaa yake na mfanya biashara mwenza alimhimiza atende kulingana na sheria zisizoandikwa za biashara, na Zhen Cheng alianza kuamini katika misemo inayowakilisha falsafa ya kama vile: "Mwanaume bila kipato cha pili hawezi kamwe kuwa tajiri kama tu jinsi farasi aliyenyimwa nyasi kavu usiku hawezi kamwe kuongeza uzani,” “Wajasiri hufa kwa ajili ya tamaa; waoga hufa kwa njaa," "Pesa si kila kitu, lakini bila pesa, huwezi kufanya chochote," na "Pesa kwanza."