10/17/2017

Umeme wa Mashariki | Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,kanisa
Umeme wa Mashariki | Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya
Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaisha, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya.

10/16/2017

Umeme wa Mashariki | Amri za Enzi Mpya

Umeme wa Mashariki ,Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Amri za Enzi Mpya
Mmeambiwa kuwa mjiandae kwa maneno ya Mungu, ya kuwa pasipo kujali kilichoandaliwa juu yenu, yote yamepangwa kwa mkono wa Mungu, na kwamba hakuna haja ya kuomba kwa bidii au kusali kwenu—haina maana. Ilhali kulingana na hali ya sasa, shida za kiutendaji mnazokumbana nazo hazitafakariki kwenu. Kama mnasubiri mipango ya Mungu tu, basi hatua zenu zitakaa zaidi, na kwa wale wasiojua kupitia kutakuwa na kulaza damu kwingi.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | ” (Video za Kikristo)

Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa


I

Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.

Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.

Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.

Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,

yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu.

10/15/2017

Umeme wa Mashariki | Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Mungu,Yesu,Umeme wa Mashariki,Ukweli
Umeme wa Mashariki | Maono ya Kazi ya Mungu (2)
Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole.

Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,Yesu,Injili
Umeme wa Mashariki | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumaini kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atasamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Wanatamani Yesu Mwokozi Awe Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi Ambaye Anapendeka, wa kirafiki na heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu.

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Umeme wa Mashariki ,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Maneno ya  Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini. Ni juu yenu basi kuwasiliana ufahamu wenu kuhusu hizi mada.
Mnapaswa kuelewa kusudi la Mungu na ni lazima muijue asili ya binadamu kupitia hii miaka saba ya majaribu. Kwa hakika, kila sentensi ya Mungu ina kusudi Lake, ambamo mmefichwa ukweli. Bila kujali ni suala gani linafanyiwa ushirika, au ni ukweli gani unaoenyeshwa, ndani yake mna njia ambayo watu wanapaswa kupitia, matakwa ya Mungu kwa watu, na kusudi la Mungu kwa wanaomtafuta.

Toeni Nyimbo za Sifa kwa Mungu - Muziki wa Akapela "Mpende Mungu Wa Vitendo Kwa Moyo Wetu Wote"

Mpende Mungu Wa Vitendo Kwa Moyo Wetu Wote

La … la la la … la la la….

La … la la la … la la la … la….

Jua la haki lapanda kutoka Mashariki.

Ee Mungu! Utukufu wako hujaza mbingu na dunia.

Mpenzi mrembo, upendo Wako huzingira moyo wangu.

Watu wanaofuatilia ukweli wote wanampenda Mungu.

Ingawa mimi huamka peke yangu asubuhi mapema, Ninahisi furaha ninapotafakaria neno la Mungu.

Maneno mororo ni kama mama mpenzi, maneno ya hukumu kama baba mkali. (Ala….)

10/13/2017

Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Umeme wa Mashariki | Kanisa la Mwenyezi Mungu | Injili
Umeme wa Mashariki | Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda
Hatua ya kazi ya watenda-huduma ni hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi; kwa sasa hii ni hatua ya pili ya kazi ya ushindi. Kwa nini ukamilifu unajadiliwa katika kazi ya ushindi? Ni kuujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye—kwa sasa hii ni hatua ya mwisho katika kazi ya kushinda, na baada ya hii, kazi ya kuwakamilisha watu itaanza rasmi wakati watakuwa wanapitia dhiki kuu. Jambo la msingi sasa ni ushindi; hata hivyo, hii pia ni hatua ya kwanza ya kukamilisha, kukamilisha ufahamu na utii wa watu, ambayo kwa kweli bado yanajenga msingi wa kazi ya kushinda. Kama unataka kukamilishwa, lazima uwe na uwezo wa kusimama imara katikati ya mateso ya siku za baadaye na uziweke nguvu zako zote katika kupanua hatua yenye kufuata ya kazi. Huku ni kukamilishwa, na huo ndio wakati ambao watu watakuwa wamepatwa na Mungu kabisa. Kile kinachojadiliwa hivi sasa ni kushindwa, ambako pia ni kukamilishwa;

10/12/2017

Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutumiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyacho, unapaswa kwanza kuelewa halisi kwa nini unalifanya hili na asili ya jambo hili ni lipi. Ikiwa imepangwa kama kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe? Hili ni jambo ambalo kwalo unapaswa kusogea karibu na Mungu. Kusogea karibu na Mungu ni kutafuta ukweli katika jambo hili, ni kutafuta jinsi ya kutenda, ni kutafuta mapenzi ya Mungu, na ni kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu.

10/11/2017

Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Umeme wa Mashariki | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya
Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru "mizigo" ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo. Inaonekana kwamba unafanya tu kazi hiyo kwa kutimiza wajibu, daima ukiamini kwamba unapaswa kufuata njia yako mwenyewe bila kujali jinsi watu wengine walivyo, na kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali jinsi watu wengine walivyo. Hamna uwezo wa kugundua uwezo wa wengine, na hamuwezi kujichunguza. Njia yenu ya kupokea vitu ni yenye makosa sana.

Upendo wa Mungu Huushinda Moyo wa Mwanadamu | "Wimbo wa Kifuasi cha Dhati" (Video Rasmi ya Muziki)

Wimbo wa Kifuasi cha Dhati

Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.

Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.

Hekima Yake, Uadilifu Wake, nayapenda yote.

Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana.

Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.

Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.

Hekima Yake, uadilifu Wake, nayapenda yote.

10/10/2017

Kuhusu Biblia (3)

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (3)
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (3)
Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa kibinadamu, na ufasiri wa ajabu wa kibinadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahahi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale.

10/09/2017

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana uwezo wa kujitenga na Mungu. Vilevile, Mungu Hajawahi kuwa na nia ya kujitenga na mwanadamu. Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu.