12/04/2017

Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video

 Kanisa la Mwenyezi Mungu | Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video

           I
Kama nisingeokolewa na Mungu,
ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi;
kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Kama nisingeokolewa na Mungu,
bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake,
bila kujua maisha yangu yangekuwaje.

56 Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Makusudi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu

56  Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Mwenyezi Mungu alisema, Upendo wa Mungu, ambaye alikuwa mwili, unajidhihirisha wapi kwa binadamu? Baada ya kupitia uzoefu wa kazi hatua kwa hatua, mnaweza kuona kwamba Mungu anapozungumza katika kila hatua ya kazi, anatumia ruwaza fulani, anazungumza unabii fulani, na anaonyesha ukweli fulani na tabia ya Mungu, na watu wote wana mijibizo. Mijibizo yao ni nini? Hawajinyenyekeshi kwa Mungu, hususan hawachukui hatua ya kutafuta ukweli, au hawapo radhi kukubali kazi ya Mungu. Wote wana mitazamo hasi na wabishi, na wanakanganyikiwa, wanakataa na hawakubali.

12/03/2017

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Uzoefu wa Maisha Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani


Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Uzoefu wa Maisha Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani

I
Nimerudi kwa familia ya Mungu,
mchangamfu na mwenye furaha.
Mikono yangu imemshika mpendwa wangu,
moyo wangu ni miliki Yake.
Japo nimepitia Bonde la Machozi,
nimeyaona mapenzi ya Mungu.
Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku,
Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu,
moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.

12/01/2017

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Yesu Kristo | Baba Wa Mbinguni

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe;

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mitume
ushuhuda| uaminifu| mitume

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wa watu unaegemea upande mmoja sana. Bila kufahamu hali nyingi kwa kweli, huwezi kufikia mbadiliko katika tabia yako. Ikiwa umeelewa hali nyingi, basi utaweza kuelewa maonyesho mbalimbali ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuona wazi na kutambua mengi ya kazi ya pepo wabaya. Lazima ufunue mawazo mengi ya wanadamu na uende moja kwa moja kwenye kiini cha suala hili;

11/29/2017

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ndugu na dada
watu wa Mungu ,kumwabudu Mungu

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi

Mwenyezi Mungu alisema, Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kiwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi. Mambo si rahisi kama ulivyofikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hapo ndipo unapoumiliki uhalisi, hapo ndipo umeupata uelewa na kimo cha kweli.

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea.Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache.

11/27/2017

Umeme wa Mashariki | Waovu Lazima Waadhibiwe

Umeme wa Mashariki  Waovu Lazima Waadhibiwe 
    Mwenyezi Mungu alisema, Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Zaidi ya unavyokubali neno la Mungu wakati huu, ndivyo unavyoweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo unavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake. Haya ndiyo maagizo ya Mungu kwako na kile unapaswa kufikia.

11/26/2017

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,uaminifu
Umeme wa Mashariki | Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

    Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu?

11/25/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

Umeme wa Mashariki | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

   
      Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma.

11/24/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.Mnaelewa? Rudieni nyuma Yangu: kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu.

11/23/2017

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu
Mwenyezi Mungu alisema, Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungukwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye?

11/22/2017

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani.Suala hili si lile ambalo ni geni sana kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo kwenye suala hili.