Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu |
Mwenyezi Mungu alisema, Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote. Kama kila kiumbe, mwanadamu bila kujua anapata lishe ya utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu.