3/05/2018

๐Ÿ˜‡๐Ÿ˜‡Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Ishirini Na Saba๐Ÿ“–๐ŸŒน

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Ishirini Na Saba

Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu kinachomhusu mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi.

3/04/2018

Umeme wa Mashariki | 62. Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Umeme wa Mashariki | 62. Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa
Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu wengine, baada ya kuhudhuria ushirika na mimi, waligeuka hasi, wanyonge na walikosa motisha ya kuendelea kutafuta. Wengine walisema ilikuwa vigumu sana kumwamini Mungu na walimwelewa Mungu visivyo. Wengine walisema kwamba hali zao zilikuwa nzuri kabla ya wao kukutana na mimi, lakini punde tu waliponiona, walihisi shinikizo kubwa mno na wasio na raha.

52 Dalili za Udanganyifu Ndani ya Mwanadamu na Asili ya Mwanadamu Ambazo Humsaliti Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ugumu ambao watu wanaweza kuukabili kwa urahisi katika uzoefu wao, vitu ambavyo vinawasababisha watu kuanguka kwa urahisi, na pahali ambapo udhaifu wa jaala wa kila mtu upo yote ni masuala ambayo lazima mtu awe na ujuzi nayo. Kwa nini unaanguka, unamwacha Mungu na kupoteza imani ya kuendelea na ukimbiziaji wako wa ukweli unapokabiliana na mambo fulani? Kwa sasa, kila mtu yumo hatarini mwa mambo haya. Bila kujali kiwango cha imani uliyo nayo kwa kawaida, shauku yako ni kubwa kiasi gani, wewe ni shupavu na asiyekubali kushindwa jinsi gani, ni kitu cha aina moja pekee kinaweza kufanyika ambacho kinaweza kufanya kila mmoja kushtuka na kuanguka kwa urahisi.

3/03/2018

7. Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Li Jing, Beijing
7 Agosti, mwaka wa 2012
Siku hiyo, ilianza kunyesha asubuhi. Nilikwenda kwa mkutano nyumbani mwa ndugu mmoja, wakati mvua ilipoendelea kuongezeka zaidi na zaidi kwa uzito. Kufikia alasiri ilikuwa ikinyesha kana kwamba ilitoka mbinguni moja kwa moja. Wakati tulipomaliza mkutano wetu, mvua ilikuwa imeingia katika ua wa ndugu yangu, lakini kwa sababu nilikuwa na wasiwasi juu ya familia yangu, nilijitahidi kwenda nyumbani. Nusu ya barabara huko, baadhi ya watu waliokimbia hatari waliniambia, "Je, si wewe unatoroka, bado unakwenda nyumbani?" Nilipofika nyumbani, mtoto wangu aliniuliza, "Je, mafuriko hayakukuzoa?" Ni hapo tu nilipojua kwamba sikuwa na Mungu moyoni mwangu.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (2)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (2)

Kazi na kuingia kwenu ni duni kabisa; mwanadamu hafikirii kwamba kazi ni muhimu na hata yeye ni mzembe zaidi na kuingia. Mwanadamu haoni haya kuwa mafunzo mazuri anayopaswa kuingia ndani; kwa hivyo, katika uzoefu wake wa kiroho, kwa kweli yote ambayo mwanadamu huona ni njozi za kiajabu. Si mengi yanatakiwa kutoka kwenu kuhusu uzoefu wenu katika kazi, lakini, kama yule anayetakiwa kukamilishwa na Mungu, mnapaswa kujifunza kumfanyia Mungu kazi ili hivi punde muweze kuupendeza moyo wa Mungu.

3/02/2018

Umeme wa Mashariki | Sura ya 5

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Sura ya 5

Mwenyezi Mungu alisema, Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? Je, unaweza thubutu kuweka wazi kila ulichofanya mbele Yangu? Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia za aibu, pia, bila mantiki yoyote! Wakati mmoja au mwingine, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu. Usithubutu kunidanganya, ukifikiri kwamba umesimama kwa ajili ya ushuhuda Wangu!

Yote kuhusu Mjadala wa "Iwapo Biblia Inatiwa Msukumo na Mungu"



Utambulisho
Kwa miaka elfu mbili, dunia ya kidini imetegemea kile alichosema Paulo kuhusu Biblia kutiwa msukumo na Mungu na daima iliamini kwamba “Biblia ni maneno ya Mungu,” na “Biblia inamwakilisha Bwana.” Je, mawazo haya ni sahihi? Video hii itafichua majibu kwako!

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.

3/01/2018

Umeme wa Mashariki | Ufalme wa Milenia Umewasili

Umeme wa Mashariki | Ufalme wa Milenia Umewasili

    Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

(I) Mhutasari juu ya Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.)

2/28/2018

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6) 

Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wanakuwa vuguvugu katika kuingia ambako Mungu anataka na wanabakia wenye shaka[1], kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili.

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sitisha Huduma ya Kidini  

    Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu huja hapa ulimwenguni kimatendo ili kufanya kazi Yake na kuwasiliana na watu ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake.

2/27/2018

Kubagua dhidi ya Watu wa Nje ni Uovu Sana!

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Hukumu

Kubagua dhidi ya Watu wa Nje ni Uovu Sana!

Xiaojin Kaunti ya Pan’an , Mkoa wa Zhejiang
Katika mwezi wa Februari mwaka wa 2007, kanisa lilipokea mpango wa kazi uitwao "Nyunyizia na Uwape Waumini Wapya ili Kuwasaidia Kukita Mizizi Haraka Iwezekanavyo." Ulisisitiza kuwa "Ni muhimu kuwatumia wale wote wanaofaa na walio na tajriba katika kuwanyunyizia waumini wapya ili kukamilisha kazi hii. Watu wasiofaa kuwanyunyizia waumini wapya hawapaswi kutumiwa; nafasi zao zinapaswa kuchukuliwa na wengine ili kuzuia kuchelewesha kazi" ("Masuala ambayo Kanisa Linakumbana nayo Sasa Ni Lazima Yatatuliwe" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi ya Kanisa I).

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita? (Kupitia kwa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ninaona kwamba Mungu hulea vitu vyote na hulea wanadamu. Katika siku zilizopita, kila mara nilifikiria kwamba Mungu anapompa mwanadamu, Anawapa tu watu Wake waliochaguliwa neno Lake, lakini kamwe sikuona, kupitia kwa sheria za vitu vyote, kwamba Mungu anawalea wanadamu.