Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Mbili
Maneno ya Mungu huwaacha watu wakikuna vichwa vyao; ni kana kwamba, Anapozungumza, Mungu anaepukana na mwanadamu na kuzungumza na hewa, kana kwamba Hafikirii hata kidogo kuzingatia zaidi matendo ya mwanadamu, na Hatilii maanani kabisa kimo cha mwanadamu, kana kwamba maneno Anayozungumza hayaelekezwi kwa dhana za watu, lakini kuepukana na mwanadamu, kama lilivyokuwa kusudi la Mungu la asili. Kwa sababu nyingi sana, maneno ya Mungu hayaeleweki na mwanadamu hawezi kuyapenya. Hili halishangazi. Lengo la asili la maneno yote ya Mungu si kwa watu kupata ujuzi au ustadi kwayo; badala yake, ni njia moja kati ya zile Mungu ametumia kufanya kazi kutoka mwanzo hadi leo.