5/03/2018

C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, uaminifu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na daima hawako tayari kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu.

Majaribu ya Shetani | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “amuru kwamba mawe haya yawe mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Halina maana. Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa usaliti na uovu wake wote, tunaona upuuzi na ujinga wake, siyo? Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake ovu na unaona akiharibu kazi ya Mungu.

5/02/2018

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Neno la Mwenyezi Mungu | 3) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

    Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomwamini Mungu wanaweza kugawika. Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji-huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na Akawaita “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum.

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

     Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, anathibitisha majina yao, anwani, umri, na walichokifanya maishani mwao.

5/01/2018

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu.

Umeme wa Mashariki | Sura ya 15

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Sura ya 15

Mwenyezi Mungu alisema, Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika. Yeye bado anafanya kama Ninavyofanya akiwa mbele Yangu, lakini nyuma Yangu anaanza kufanya “shughuli” zake mwenyewe za kipekee. Hata hivyo, mara hiyo inapokamilika na anarudi mbele Yangu tena, yeye huwa kama mwanadamu tofauti, akiwa na hali ya utulivu safihi, hali yake ni shwari, na mpigo wa moyo wake ni mtulivu.

4/30/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (3)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (3)

    Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa ni Enzi ya Ufalme, na mwanadamu ameingia katika zoezi la ufalme. Hatua hii ya kazi si kazi ya mwanadamu au ya kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani; ni kuimaliza sehemu ya kazi ya Mungu. Kazi Yake si kazi ya mwanadamu na si kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani kabla ya kuondoka duniani; ni kutimiza huduma Yake kwa ukamilifu na kuimaliza kazi ambayo Anapaswa kuifanya, ambayo ni kutengeneza mipango ya kufaa ya kazi Yake duniani, na hivyo kupata kutukuka.

Umeme wa Mashariki | Sura ya 16

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simmalizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wa nguvu wake, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya tu kazi Yangu, na kuongea kama Nimekuwa Nikifanya daima, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua Mimi ndani kabisa ya nyoyo zao, na watakuja kunikumbuka Mimi kwenye mawazo yao.

4/29/2018

Maneno ya Mungu Yameniamsha

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maneno ya Mungu Yameniamsha

Miao Xiao Mji wa Jinan, Mkoa wa Shandong
Katika siku zilizopita, nilikuwa daima nikifikiri kuwa Mungu aliposema “ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi” Alikuwa anaashiria wale wanaoikubali hatua hii ya kazi lakini wanaishia kurudi nyuma kwa sababu hawako radhi kustahimili mateso ya kuadibu na hukumu Yake. Kwa hivyo, wakati wowote nilipoona ndugu wakijiondoa katika njia hii kwa sababu yoyote ile, moyo wangu ungejawa na dharau kwao. Huyo, kibaraka na msaliti mwingine anatoroka kutoka kwa kiti kikuu cheupe cha enzi ambaye atapokea adhabu ya Mungu. Wakati uo huo, nilijihisi nikiwa nikitenda ifaavyo kwa kukubali hukumu ya Mungu na nilikuwa siko mbali na kukubali ukombozi wake Mungu.

Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Saba

    Mwenyezi Mungu alisema, Kotekote katika enzi, kazi yote Niliyoifanya—kila hatua ya kazi hiyo—imekuwa na mbinu Zangu zinazofaa za kazi. Ni kwa sababu ya hili ndio watu Wangu wapendwa wamekuwa watakatifu zaidi na zaidi, na wa kufaa zaidi na zaidi kwa matumizi Yangu. Kwa sababu hiyo hiyo, hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba kadri mbinu Zangu za kazi zinavyoongezeka, idadi ya watu inapungua, ambalo husababisha watu kuzama katika kutafakari. Bila shaka, Kazi Yangu leo sio tofauti na watu wengi wamejikuta tena katika kutafakari, kwa hiyo kwa sababu ya mabadiliko ya mbinu Zangu, kuna sehemu ya watu ambao watajiondoa. Inaweza kuelezwa kwa njia hii: Hili lilikuwa limeamuliwa na Mimi kabla, lakini halikufanywa na Mimi.

4/28/2018

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Kama hatua ya mwisho ya kazi ya ushindi ingeanzia Israeli, basi kazi ya ushindi isingekuwa na maana. Kazi ni ya umuhimu zaidi wakati ikiwa inafanyika nchini humu, inapofanyika kwenu enyi watu. Ninyi ni watu wanyenyekevu zaidi, watu walio na hadhi ndogo zaidi. Ninyi ni watu katika ngazi ya chini kabisa ya jamii hii na ninyi ndio ambao walimtambua Mungu kwa kiwango cha chini sana mwanzoni . Ninyi ni watu ambao wamekwenda mbali zaidi na Mungu, na ni wale ambao wamejeruhiwa vibaya. Kwa sababu hatua hii ya kazi ni kwa ajili tu ya ushindi, je, haifai zaidi kuwachagua kuwa na ushuhuda ujao?

Kwa nini Chama cha Kikomunisti cha China Huwalazimisha Wakristo Kujiunga na Kanisa la Utatu Binafsi?🎬👍

🎬******^^*******😥******^^*****👍******^^********💪

Nchini China, makanisa ya nyumbani yameteseka moja kwa moja matokeo ya ukandamizaji na utesaji wenye wayowayo wa serikali kanamungu ya Kikomunisti ya China. Wanawalazimisha kuingia katika Kanisa la Utatu Binafsi ambalo linadhibitiwa na Idara ya Kazi ya Muungano. Chama cha Kikomunisti cha China kinaficha siri gani kwa kufanya hili? Wakristo wanakabili hatari ya kufungwa jela na hata kupoteza maisha yao ili kueneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Ni kwa nini hasa wanafanya hili?

4/27/2018

Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.
2. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu.
3. Yafanye mazoea ya kawaida kutafakari na kuzingatia maneno ya Mungu na kufikiri kazi ya Mungu na moyo wako.