Mwenyezi Mungu alisema, Kundi la watu ambao Mungu anataka kupata sasa ni wale ambao wanajitahidi kushirikiana na Mungu, wanaoweza kuiheshimu kazi Yake, na wanaoamini kuwa maneno Anayonena Mungu ni ya kweli, wale wanaoweza kuweka mahitaji ya Mungu katika vitendo. Ni wale walio na uelewa wa kweli katika mioyo yao. Ni hao ndio wanaoweza kukamilishwa, na wale ambao bila shaka watatembea katika njia ya ukamilisho. Wale wasio na uelewa wa wazi wa kazi ya Mungu, wale wasiokula na kunywa neno la Mungu, wale wasiotilia maanani neno la Mungu, na wale wasio na upendo wowote kwa Mungu katika mioyo yao—watu kama hao hawawezi kufanywa wakamilifu.
"Mungu anatekeleza hatua ya kazi kubwa kila wakati yeye hujifunua. Kazi hii ni tofauti na ile ya enzi mwingine yoyote. Haiwezi kufikiriwa na mtu, na haijawahi kujifunza na mwanadamu. Ni kazi ambayo huanza enzi mpya na huhitimisha enzi, na ni aina mpya ya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu; Zaidi ya hayo, ni kazi ya kuwaleta wanadamu katika wakati mpya. Hiyo ni umuhimu wa kuonekana kwa Mungu. kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili"
5/04/2018
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako
Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.
5/03/2018
C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na daima hawako tayari kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu.
Majaribu ya Shetani | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “amuru kwamba mawe haya yawe mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Halina maana. Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa usaliti na uovu wake wote, tunaona upuuzi na ujinga wake, siyo? Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake ovu na unaona akiharibu kazi ya Mungu.
5/02/2018
Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X
Neno la Mwenyezi Mungu | 3) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu
Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomwamini Mungu wanaweza kugawika. Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji-huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na Akawaita “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum.Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X
Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, anathibitisha majina yao, anwani, umri, na walichokifanya maishani mwao.
5/01/2018
Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu.
Umeme wa Mashariki | Sura ya 15
Umeme wa Mashariki | Sura ya 15
Mwenyezi Mungu alisema, Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika. Yeye bado anafanya kama Ninavyofanya akiwa mbele Yangu, lakini nyuma Yangu anaanza kufanya “shughuli” zake mwenyewe za kipekee. Hata hivyo, mara hiyo inapokamilika na anarudi mbele Yangu tena, yeye huwa kama mwanadamu tofauti, akiwa na hali ya utulivu safihi, hali yake ni shwari, na mpigo wa moyo wake ni mtulivu.
4/30/2018
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (3)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (3)
Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa ni Enzi ya Ufalme, na mwanadamu ameingia katika zoezi la ufalme. Hatua hii ya kazi si kazi ya mwanadamu au ya kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani; ni kuimaliza sehemu ya kazi ya Mungu. Kazi Yake si kazi ya mwanadamu na si kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani kabla ya kuondoka duniani; ni kutimiza huduma Yake kwa ukamilifu na kuimaliza kazi ambayo Anapaswa kuifanya, ambayo ni kutengeneza mipango ya kufaa ya kazi Yake duniani, na hivyo kupata kutukuka.Umeme wa Mashariki | Sura ya 16
Mwenyezi Mungu alisema, Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simmalizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wa nguvu wake, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya tu kazi Yangu, na kuongea kama Nimekuwa Nikifanya daima, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua Mimi ndani kabisa ya nyoyo zao, na watakuja kunikumbuka Mimi kwenye mawazo yao.
4/29/2018
Maneno ya Mungu Yameniamsha
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maneno ya Mungu Yameniamsha
Miao Xiao Mji wa Jinan, Mkoa wa Shandong
Katika siku zilizopita, nilikuwa daima nikifikiri kuwa Mungu aliposema “ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi” Alikuwa anaashiria wale wanaoikubali hatua hii ya kazi lakini wanaishia kurudi nyuma kwa sababu hawako radhi kustahimili mateso ya kuadibu na hukumu Yake. Kwa hivyo, wakati wowote nilipoona ndugu wakijiondoa katika njia hii kwa sababu yoyote ile, moyo wangu ungejawa na dharau kwao. Huyo, kibaraka na msaliti mwingine anatoroka kutoka kwa kiti kikuu cheupe cha enzi ambaye atapokea adhabu ya Mungu. Wakati uo huo, nilijihisi nikiwa nikitenda ifaavyo kwa kukubali hukumu ya Mungu na nilikuwa siko mbali na kukubali ukombozi wake Mungu.
Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Saba
Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Saba
Mwenyezi Mungu alisema, Kotekote katika enzi, kazi yote Niliyoifanya—kila hatua ya kazi hiyo—imekuwa na mbinu Zangu zinazofaa za kazi. Ni kwa sababu ya hili ndio watu Wangu wapendwa wamekuwa watakatifu zaidi na zaidi, na wa kufaa zaidi na zaidi kwa matumizi Yangu. Kwa sababu hiyo hiyo, hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba kadri mbinu Zangu za kazi zinavyoongezeka, idadi ya watu inapungua, ambalo husababisha watu kuzama katika kutafakari. Bila shaka, Kazi Yangu leo sio tofauti na watu wengi wamejikuta tena katika kutafakari, kwa hiyo kwa sababu ya mabadiliko ya mbinu Zangu, kuna sehemu ya watu ambao watajiondoa. Inaweza kuelezwa kwa njia hii: Hili lilikuwa limeamuliwa na Mimi kabla, lakini halikufanywa na Mimi.4/28/2018
Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Kama hatua ya mwisho ya kazi ya ushindi ingeanzia Israeli, basi kazi ya ushindi isingekuwa na maana. Kazi ni ya umuhimu zaidi wakati ikiwa inafanyika nchini humu, inapofanyika kwenu enyi watu. Ninyi ni watu wanyenyekevu zaidi, watu walio na hadhi ndogo zaidi. Ninyi ni watu katika ngazi ya chini kabisa ya jamii hii na ninyi ndio ambao walimtambua Mungu kwa kiwango cha chini sana mwanzoni . Ninyi ni watu ambao wamekwenda mbali zaidi na Mungu, na ni wale ambao wamejeruhiwa vibaya. Kwa sababu hatua hii ya kazi ni kwa ajili tu ya ushindi, je, haifai zaidi kuwachagua kuwa na ushuhuda ujao?
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)