9/12/2018

Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Maneno Husika ya Mungu:
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu!

Latest Swahili Christian Video "Njia ya mwenendo wa Binadamu" | Hukumu ya Mungu



Tangu umri mdogo, wazazi wa Cheng Jianguang na walimu walimfundisha sheria kama vile "Uwiano ni hazina, uvumilivu ni wema," "Kunyamazia makosa ya rafiki wazuri hudumisha urafiki mzuri na wa muda mrefu," "Ingawa utaona makosa, ni vyema useme machache" zilikuwa ni nguzo za kudumisha uhusiano mzuri na watu wengine. Alichukua mafunzo haya kwa moyo, na kujifinza kamwe kutowakosea wengine katika matendo na mazungumzo yake, na daima kutunza uhusiano wake na wengine, hivi kumpatia sifa ya "mtu mzuri" kwa wale wliokuwa karibu naye.

9/11/2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu💗😇


"Yehova" na "Yesu" yalikuwa ni majina ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na imetabiriwa katika Ufunuo kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho. Ni kwa nini Mungu anaitwa kwa majina tofauti katika enzi mbalimbali? Majina haya mawili ya "Yehova" na "Yesu" yana umuhimu gani? Video hii fupi itakusaidia kukutatulia fumbo hili.

Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ee Mungu, Unajua Nakukosa Wewe

Moyo wangu unakupenda sana. Lakini nahisi kuwa sifai upendo Wako.
Mnyonge sana sifai kuwa katika uwepo Wako, nina hofu sana na wasiwasi!
Naweza tu kuamua; kutoa nafsi yangu yote Kwako.
Nitateseka kwa ajili Yako, nipipitie mateso yote, hadi pumzi ya mwisho ya maisha yangu.
Mungu! Unajua kuwa nasubiri, nasubiri Wewe urejee.

9/10/2018

Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. 

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?


🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌻🌻🌻🌻🌻🌻💗💗💗💗💗😇😇😇😇😇
Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini mara nyingi huhubiri kwa waumini kuwa jina la Bwana Yesu haliwezi kamwe kubadilika na kuwa ni kwa kutegemea tu jina la Bwana Yesu ndio tunaweza kuokolewa. Je, mtazamo wa aina hii unaambatana na kuweli? Yehova Mungu alisema, "kabla yangu hakukuwa na Mungu aliyeumbwa, wala hakutakuwa baada yangu. Mimi, hata mimi, ni BWANA; na isipokuwa mimi hakuna mwokozi" (Isaya 43:10-11).Katika Enzi ya Neema, Mungu mwenye mwili alichukua jina la Yesu.

9/09/2018

Je, Kuna Maneno Mengine ya Mungu Kando ya Yale Yaliyo kwenye Biblia🎬💗


Biblia inasema, "Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kilichofungwa kwa mihuri saba" (Ufunuo 5:1). "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa; Kwa yule ashindaye nitampa mana iliyofichwa aile" (Ufunuo 2:17). Kulingana na Biblia, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho Atafungua kitabu, afungue mihuri saba na ampe mwanadamu mana iliyofichwa.

Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Momo     Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui
Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, "Hakuna maumivu, hakuna faida," na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu.

9/08/2018

Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

4. Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini kinashirikishwa ndani ya ubinadamu wa kawaida? Utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida.

"Imani katika Mungu" (6) - Imani ya Kweli katika Mungu Inamaanisha Nini?


Watu wengi wanaamini kwamba imani katika Mungu ni imani katika Biblia, na kwamba kumfanyia Bwana kazi kwa bidii ni uhalisi wa kuamini katika Mungu. Hakuna mtu katika ulimwengu wa dini ana uwezo wa kuelewa kabisa imani ya kweli katika Mungu ina maana gani. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Imani katika Mungu’ inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu.Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu sio sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini.

9/07/2018

Je, Kufanya Kazi kwa Bidii kwa ajili ya Bwana ni Uhalisi wa Imani katika Bwana?


Waumini wengi huamini kwamba mradi tunalilinda jina la Bwana, kuomba mara kwa mara, kusoma Biblia na kuwa na mikutano, na mradi sisi huyaacha vitu, hutumia rasilmali na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Bwana, basi hii ni imani ya kweli katika Bwana, na tutaweza kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Je, aina hii ya mtazamo ni sahihi? Wengi wataniita siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujafanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Katika Mapana na Marefu, Mwaminifu Hadi Kifo

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Katika Mapana na Marefu, Mwaminifu Hadi Kifo

Kutoka mbinguni hadi duniani, Akijificha katika mwili.
Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, katika upepo na mvua.
Ukachukua njia ngumu, ukafungua enzi mpya.
Kumkomboa mwanadamu, kutoa maisha Yako na kumwaga damu.
Upepo na mvua, miaka mingi sana. Kutelekezwa na kila mwanadamu.

9/06/2018

Hatimaye Nimemwona Mungu

Nilikuja katika uwepo Wako siku hiyo, moyo wangu ukiwa umejaa tamaa ya kina.
Macho yangu yalipojawa na machozi, mkono Wako ulinipapasa.
Majonzi na huzuni ulimwagika kutoka moyoni mwangu.
Maisha yangu ya awali yakipita mbele ya macho yangu; majonzi na uchungu vikigongana kwa kutanafusi.
Mungu, nakupa Wewe upendo wangu.