Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Tisa
Kati ya kazi inayofanywa na watu, baadhi yake hutekelezwa kwa maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu, lakini kwa sehemu yake Mungu hatoi maagizo ya wazi, ikionyesha vya kutosha kwamba kile kinachofanywa na Mungu, leo, bado hakijafichuliwa kabisa—ambalo ni kusema, mengi bado yamefichwa na bado hayajajulikana na watu.
