4/29/2019

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu (Clip 5/7)

Filamu za Injili | “Sauti Nzuri Ajabu” Movie Clip: Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu

   
        Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu? Maneno ya Mungu yanasema: "Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu."

4/28/2019

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Saa ya Giza Kabla ya Mapambazuko"


Utambulisho


Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

4/27/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 22

Kumwamini Mungu si jambo rahisi kufanya. Ninyi mnajiboronga, mkiteketeza kila kitu mbele yenu mkifikiri kuwa haya yote ni ya kuvutia sana, matamu mno! Kuna baadhi ambao bado wanashangilia—wao tu hawana utambuzi katika roho zao. Ni vyema kuchukua muda wa kuuweka katika muhtasari uzoefu huu. Katika siku za mwisho, kila aina za pepo huibuka kutekeleza majukumu yao, wakikaidi kwa uwazi hatua za mbele za wana wa Mungu na kushiriki katika kuuvunja ujenzi wa kanisa.

4/26/2019

Kusonga kwa Kazi ya Mungu Ulimwenguni

Watu duniani watakubali kushindwa na Mungu, watiifu kama malaika walivyo,bila kutaka kupinga ama kuasi; hii ni kazi ya Mungu katika ulimwengu mzima.
I
Mungu amekuwa na mwanadamu kwa miaka, hakuna ambaye amekuwa na ufahamu,
hakuna yule ambaye amemjua Yeye; sasa maneno ya Mugu yanawaambia Yeye yuko hapa.

4/25/2019

Swahili Christian Video 2018 | "Ni Vizuri Sana Kutupa Mbali Pingu za Hadhi" | Wokovu wa Mungu


Baada ya Liang Zhi kumwamini Mungu, bila kukoma alitafuta kwa shauku, na kujitosa katika kutimiza wajibu wake. Baada ya miaka kadhaa, alichaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Wakati alipokuwa akitekeleza wajibu wake kama kiongozi wa kanisa, aligundua kwamba baadhi ya ndugu walikuwa na uwezo zaidi kumliko, ambayo ilimfanya asiwe na furaha kwa kiasi kwamba alikuwa na wivu kwao. Ili kuokoa uso na kulinda hali yake, alishindana nao kwa siri ili kuona ni nani aliyekuwa bora, na alikimbilia umaarufu na hadhi. Umaarufu na hadhi vilionekana kama pingu zisizoonekana zilizomfunga sana, kumnyima uhuru, kumsababisha afanye mambo kinyume na ukweli na kupinga Mungu.

4/24/2019

Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu


Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu

Upendo na huruma za Mungu 
hupenyeza kazi Yake 
ya usimamizi kwa utondoti.
I
Ikiwa mwanadamu ahisi mapenzi Yake ya huruma au la, 
Yeye hachoki kufuatilia kazi Anayohitaji kufanya.
Ikiwa mwanadamu aelewa usimamizi Wake au la, 
kazi Yake huleta usaidizi na utoaji unaoweza kuhisiwa na wote.
Upendo na huruma za Mungu 
hupenyeza kazi Yake 
ya usimamizi kwa utondoti.

4/23/2019

Maonyesho ya Mungu | "Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu"

\

Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake.

4/22/2019

Maonyesho ya Mungu | "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"


Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu wa siku za mwisho hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu.

4/21/2019

Neno la Mungu | "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" (Sehemu ya Kwanza)

Utambulisho

Neno la Mungu | "Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu" (Sehemu ya Kwanza)


     Mwenyezi Mungu anasema, "Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri. Itakuwa mwanzo wa maisha ya mwanadamu na Mungu duniani.

4/20/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Utambulisho

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Mwenyezi Mungu anasema, "Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika vishawishi vya wanadamu?

4/19/2019

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Utambulisho

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Maombi ni njia moja ya mwanadamu kushirikiana na Mungu,

kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.

Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia.

Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.

4/18/2019

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)

Utambulisho

Maonyesho ya Mungu | "Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo" (sehemu ya kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. … Hutekeleza kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo. Kwake Yeye, kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kwa ugonjwa;

4/17/2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (6) : Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu

Utambulisho

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (6) : Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu

Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, Wayahudi walishikilia kwa ukaidi sheria yao na kukataa kukubali kazi ya Bwana Yesu, ambayo iliwafanya waanguke katika giza na kupoteza wokovu wa Mungu. Sasa katika zile siku za mwisho, dunia nzima ya kidini inalinda tu jina la Bwana Yesu na kukataa kumkubali Mwenyezi Mungu, na hivyo kuisababisha kuwa na ukiwa zaidi na zaidi na kuwa jangwa lilisoweza kuzaa matunda. Kwa nini hasa iko hivi? Ni kwa sababu Mungu pekee ndiye chemchemi ya maji yaliyo hai ya uzima na Yeye ndiye chanzo cha uzima wa vitu vyote.