8/19/2019

Wimbo wa Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation


Wimbo wa Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation


Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda,
uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme.
Maneno Yako yamenitakasa,
yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha.
Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu.
Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu!
Maneno Yako yote ni ukweli.
Unastahili upendo wa binadamu.
Ee Mungu! Ukipuuza uasi wangu wa zamani,
Unanijali na kufanya kazi kuniokoa.
Unaniongoza katika njia ya kweli,
Ukitazama kila wakati katika upande wangu,
natarajia tu nitakua na kuwa mtu mpya.

8/18/2019

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi.

8/17/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85


Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole na wanaokuwa na uhakika zaidi kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).

8/16/2019

Kazi na Kuingia (3)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni.

8/15/2019

Matamshi ya Mungu | Kazi na Kuingia (5)

Leo wote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia katika enzi nyingine, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuvuka mipaka ya enzi hii ya kale ya giza, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, ili kila mtu aweze kuishi katika ulimwengu wa uhuru.

8/14/2019

Neno la Mungu | Sura ya 116

Kati ya maneno Yangu, mengi huwafanya watu kuhisi woga, mengi huwafanya watu watetemeke kwa hofu; bado mengine mengi sana huwafanya watu kuteseka na kukata tamaa, na bado mengine mengi husababisha uangamizaji wa watu. Wingi wa maneno Yangu, hakuna mtu anayeweza kuelewa au kufahamu vizuri. Ni wakati tu Ninapowaambia maneno Yangu na kuyafichua kwenu sentensi baada ya sentensi ndipo mnaweza kujua hali ya jumla; ukweli wa mambo maalum ya hakika, bado hamuelewi. Basi, Nitatumia ukweli kufichua maneno Yangu yote, hivyo kuwaruhusu mpate ufahamu wa juu zaidi.

8/13/2019

New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?



New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?


Lin Bo'en alikuwa mzee wa kanisa katika kanisa la nyumbani Uchina. Wakati wa miaka yake yote kama muumini, alihisi kwamba ameheshimiwa kuteseka kwa ajili ya Bwana, na alithamini kumfahamu na kumpata Bwana Yesu Kristo zaidi ya kitu kingine chochote duniani. Siku moja ya jaala, alienda nje kuhubiri na akasikia habari fulani za kushtua: Bwana Yesu amerudi katika mwili, na Yeye ni Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu! Lin Bo'en alikanganyikiwa. 

8/12/2019

“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Tunaweza Kupata Uzima kwa Kuamini Katika Biblia? | Swahili Gospel Movie Clip 6/6



“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Tunaweza Kupata Uzima kwa Kuamini Katika Biblia? | Swahili Gospel Movie Clip 6/6


Mara kwa mara wachungaji na wazee huwafundisha watu kuwa hawawezi kuitwa waumini wakiondoka kwenye Biblia, na kwamba kwa kushikilia Biblia pekee ndiyo wanaweza kupata uzima na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, je, kweli hatuwezi kupata uzima tukiondoka kwenye Biblia? Je, ni Biblia ambayo inaweza kutupa uzima, au ni Mungu ambaye anaweza kutupa uzima? Bwana Yesu alisema, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai" (Yohana 5:38-40).  

8/11/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 41

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na uwe sauti Yangu.

8/10/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"



Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"


I Mungu alikuja duniani hasa kutimiza ukweli wa "Neno kuwa mwili." (tofauti na Agano la Kale, katika siku za Musa, Mungu alizingumza moja kwa moja kutoka mbinguni). Kisha, yote yatatimizwa katika enzi ya Ufalme wa Milenia kuwa ukweli ambao watu wanaweza kuona, ili watu waweze kuona utimizaji hasa kwa macho yao wenyewe. Hii ni maana ya kina ya Mungu kuwa mwili. Yaani, kazi ya Roho imekamilika kupitia kwa mwili na neno. Hii ni maana ya kweli ya "Neno kuwa mwili, Neno kuonekana katika mwili."

8/09/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 53

Mimi ndiye mwanzo, na Mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyefufuka na kamili. Nasema maneno Yangu mbele yenu, na lazima muamini Ninachosema kwa thabiti. Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au mstari mmoja wa kile Ninachosema kitawahi kupita. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Punde ambapo Nimesema, hakuna neno hata moja limewahi kurudishwa na kila neno litatimizwa. Sasa wakati umewadia na lazima muingie katika uhalisi kwa haraka. Hakuna muda mwingi. 

8/08/2019

Neno la Mungu | Sura ya 57

Je, umechunguza kila fikira na mawazo yako, na kila tendo lako? Uko wazi kuhusu gani kati ya haya yanalingana na mapenzi Yangu na gani hayalingani? Huna uwezo wa kutambua haya! Mbona hujaja mbele Yangu? Je, ni kwa sababu Sitakuambia, au ni kwa ajili ya sababu nyingine? Unapaswa kujua hili! Kujua kwamba wale walio wazembe hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu kabisa au kupokea mwangaza na ufunuo mkuu.

8/07/2019

“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Ni Vipi Kuna Makosa Ndani ya Biblia? | Clip 5/6



“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Ni Vipi Kuna Makosa Ndani ya Biblia? | Swahili Gospel Movie Clip 5/6

Watu wengi wanaamini kwamba Biblia yote imetiwa msukumo na Mungu, kwamba imetoka kabisa kwa Roho Mtakatifu, na kwamba hakuna hata neno moja lililo na kosa. Je, mtazamo wa aina hii unawiana na ukweli? Biblia iliandikwa na waandishi zaidi ya 40, yaliyomo yaliandikwa na kupangwa na mwanadamu, na haikufunuliwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Ilikuwa vigumu kuepuka kuingiza mawazo na makosa ya mwanadamu wakati ambapo ilikuwa ikiandikwa na kupangwa na mwanadamu.