8/23/2019

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Na Bong, Philippines
Nataka Kuwa Tajiri
“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.
Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”

8/22/2019

Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God



Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God


Li Qingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina ambaye amekuwa mwaminifu kwa Bwana kwa miaka mingi. Siku zote kwa shauku kubwa anaifanya kazi ya Bwana ya kuieneza injili, akisubiri kwa uangalifu kuja kwa Bwana ili amlete hadi kwenye ufalme wa mbinguni. Katika miaka ya hivi majuzi, Li Qingxin amegundua kwamba vikundi na makanisa mbalimbali yamekuwa na ukiwa zaidi. Umeme wa Mashariki, hata hivyo, limekuwa la kusisimua zaidi, licha ya shutuma na mateso mengi yenye mhemko kutoka kwa serikali ya Kikomunisti ya Uchina na jamii ya dini. Kondoo wazuri zaidi na zaidi na kondoo viongozi wa madhehebu na vikundi mbalimbali wamekubali Umeme wa Mashariki. 

8/21/2019

2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Mwanzo na Mustakabali wa Wanadamu" (Swahili Subtitles)


2018 Gospel Music "Mungu Kuutawala Mwanzo na Mustakabali wa Wanadamu" (Swahili Subtitles)


Kutoka wakati tunapoingia ulimwenguni tukilia kwa huzuni, sisi huanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha. Sisi husogea kutoka kuzaliwa hadi ugonjwa hadi uzee hadi kifo; sisi huenda kati ya furaha na huzuni…. Wnadamu hasa hutoka wapi, na kwa kweli tutaenda wapi? Ni nani aliyeudhibiti mwanzo wa mwanadamu, na ni nani huamuru mustakabali wake? Leo, yote yatafichuliwa …

Tazama Video: Mungu Amekuja Mungu Ametawala | "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"

8/20/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 83

Hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu; hujui kwamba mambo yote na vitu vyote viko chini ya udhibiti Wangu! Maana ya kila kitu huumbwa na kukamilishwa na Mimi ni nini? Baraka au misiba ya kila mtu hutegemea utimilifu Wangu, matendo Yangu. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu anaweza kufanikisha nini kwa kufikiri? Katika enzi hii ya mwisho, katika enzi hii potovu, katika dunia hii ya giza ambayo Shetani ameipotosha sana, ni kina nani wachache ambao wako jinsi Nipendavyo? Ikiwa ni leo, jana, au katika siku zijazo zisizo mbali, maisha ya kila mtu huamuliwa na Mimi. 

8/19/2019

Wimbo wa Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation


Wimbo wa Kuabudu "Niko Tayari Kutekeleza Wajibu Wangu kwa Uaminifu" | God Is My Salvation


Mpendwa Mwenyezi Mungu, ni Wewe ndiye Unayenipenda,
uliniinua kutoka kwa rundo la kinyesi hadi kwa mazoezi ya ufalme.
Maneno Yako yamenitakasa,
yakanifanya nianze kuishi maisha ya furaha.
Moyoni mwangu nahisi, kwa kweli, ni upendo Wako mkuu.
Aa … aa … aa … aa … Mpendwa Mwenyezi Mungu!
Maneno Yako yote ni ukweli.
Unastahili upendo wa binadamu.
Ee Mungu! Ukipuuza uasi wangu wa zamani,
Unanijali na kufanya kazi kuniokoa.
Unaniongoza katika njia ya kweli,
Ukitazama kila wakati katika upande wangu,
natarajia tu nitakua na kuwa mtu mpya.

8/18/2019

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi.

8/17/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85


Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole na wanaokuwa na uhakika zaidi kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).

8/16/2019

Kazi na Kuingia (3)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni.

8/15/2019

Matamshi ya Mungu | Kazi na Kuingia (5)

Leo wote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia katika enzi nyingine, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuvuka mipaka ya enzi hii ya kale ya giza, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, ili kila mtu aweze kuishi katika ulimwengu wa uhuru.

8/14/2019

Neno la Mungu | Sura ya 116

Kati ya maneno Yangu, mengi huwafanya watu kuhisi woga, mengi huwafanya watu watetemeke kwa hofu; bado mengine mengi sana huwafanya watu kuteseka na kukata tamaa, na bado mengine mengi husababisha uangamizaji wa watu. Wingi wa maneno Yangu, hakuna mtu anayeweza kuelewa au kufahamu vizuri. Ni wakati tu Ninapowaambia maneno Yangu na kuyafichua kwenu sentensi baada ya sentensi ndipo mnaweza kujua hali ya jumla; ukweli wa mambo maalum ya hakika, bado hamuelewi. Basi, Nitatumia ukweli kufichua maneno Yangu yote, hivyo kuwaruhusu mpate ufahamu wa juu zaidi.

8/13/2019

New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?



New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?


Lin Bo'en alikuwa mzee wa kanisa katika kanisa la nyumbani Uchina. Wakati wa miaka yake yote kama muumini, alihisi kwamba ameheshimiwa kuteseka kwa ajili ya Bwana, na alithamini kumfahamu na kumpata Bwana Yesu Kristo zaidi ya kitu kingine chochote duniani. Siku moja ya jaala, alienda nje kuhubiri na akasikia habari fulani za kushtua: Bwana Yesu amerudi katika mwili, na Yeye ni Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu! Lin Bo'en alikanganyikiwa. 

8/12/2019

“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Tunaweza Kupata Uzima kwa Kuamini Katika Biblia? | Swahili Gospel Movie Clip 6/6



“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Tunaweza Kupata Uzima kwa Kuamini Katika Biblia? | Swahili Gospel Movie Clip 6/6


Mara kwa mara wachungaji na wazee huwafundisha watu kuwa hawawezi kuitwa waumini wakiondoka kwenye Biblia, na kwamba kwa kushikilia Biblia pekee ndiyo wanaweza kupata uzima na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, je, kweli hatuwezi kupata uzima tukiondoka kwenye Biblia? Je, ni Biblia ambayo inaweza kutupa uzima, au ni Mungu ambaye anaweza kutupa uzima? Bwana Yesu alisema, "Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai" (Yohana 5:38-40).  

8/11/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 41

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na uwe sauti Yangu.