Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” (Dondoo)
Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia, Ninawasubiri; Niko kando yenu…. Mikono yake ni yenye joto na thabiti; nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake linapita na kugeuka, linakumbatia binadamu wote; uso Wake ni mzuri na mtulivu. Hajawahi kuondoka, wala Hajatoweka. Usiku na mchana, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu.”
Kujua zaidi: Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu