11/16/2019

Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Maneno Husika ya Mungu:

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

11/15/2019

Hukumu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

11/14/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” (Dondoo)

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” (Dondoo)

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia, Ninawasubiri; Niko kando yenu…. Mikono yake ni yenye joto na thabiti; nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake linapita na kugeuka, linakumbatia binadamu wote; uso Wake ni mzuri na mtulivu. Hajawahi kuondoka, wala Hajatoweka. Usiku na mchana, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu.”

Kujua zaidi: Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

11/13/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Pili)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" (Sehemu ya Pili)

     Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kujua zaidi :Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

11/12/2019

23. Kuna tofauti ipi kati ya ngano na magugu?

Maneno Husika ya Mungu:

Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetani haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu. Kwa sababu Nimesema awali kwamba asili ya mwanadamu haibadiliki, ngano siku zote itakuwa ngano.

11/11/2019

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance

Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia,
mchangamfu na mwenye nguvu za ujana,
wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni.
Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu.
Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake.
Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.
Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku,
tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza.
Tunakubali uchunguzi wa Mungu, tunaishi mbele Yake.
Kumpenda Mungu kweli ni kuwa na furaha.

11/10/2019

Swahili Gospel Film "Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari"

Swahili Gospel Film "Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari"

      Zhong Xin ni mhubiri kutoka katika kanisa moja la nyumbani katika bara China. Amekuwa muumini katika Mungu kwa miaka mingi na kila mara amepitia kukamatwa na mateso ya CCP. Chuki yake ya CCP ni ya kina sana, na ameona wazi kwa muda mrefu sasa kwamba CCP ni utawala wa kishetani ambao unajiweka katika upinzani na Mungu. Kwa miaka ya hivi majuzi, ameona shutuma, kukamatwa na kuteswa kinyama kwa kanisa la Umeme wa Mashariki na serikali ya CCP na dunia ya kidini. Alichoona kuwa cha ajabu, hata hivyo, kilikuwa kwamba Umeme wa Mashariki halikukosa tu kushindwa, lakini kwa kinyume lilikuwa limenawiri zaidi na zaidi, na hivyo Zhong Xin alianza kutafakari tena: Je, hili Umeme wa Mashariki ni dhihirisho la kuonekana na kazi ya Bwana? 

11/09/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” (Dondoo 3)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Zaidi:Kueneza kwa Injili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu Nchini China

11/08/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Ishirini na Mbili”

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Zaidi:Kueneza kwa Injili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu Nchini China

11/07/2019

Sauti ya Mungu | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” (Dondoo 1)

Sauti ya Mungu | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” (Dondoo 1)

“Kumcha Mungu” hakumaanishi woga na hofu isiyotajika, wala kukwepa, wala kuweka umbali, wala si kuabudu kama mungu ama ushirikina. Ila, ni kutazama na kupendezwa, sifa, imani, kuelewa, kujali, kutii, kuweka wakfu, upendo, na pia ibada isiyo na vikwazo au malalamishi, malipo na kujisalimisha. Bila ya ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na kupendezwa halisi, imani halisi, kuelewa halisi, kujali halisi ama utiifu, ila tu hofu na kukosa utulivu, shaka pekee, kutoelewa, kukwepa, na kuepuka; bila maarifa halisi ya Mungu, binadamu hawatakuwa na utakatifu na malipo halisi; bila ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na ibada halisi na kujisalimisha, uabudu kama mungu upofu tu na ushirikina; bila maarifa halisi juu ya Mungu, binadamu hawawezi kutenda kulingana na njia ya Mungu, ama kumcha Mungu, ama kuepuka maovu. Badala yake, kila tendo na tabia ambayo mwanadamu anashiriki litajaa uasi na kutotii, na kumbukumbu zinazokashifu na hukumu ya usengenyaji kumhusu Yeye, na mienendo miovu inayokwenda kinyume na ukweli na maana ya kweli ya maneno ya Mungu.

11/06/2019

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV

Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.

11/05/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 3)

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 3)

Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, unaanza safari yako katika maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeunda, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, kwa maana yule Anayetawala kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa akitenda kazi Yake kwa njia hii, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mifuatano ya mabadiliko katika mambo yote na njia ambazo yanasongea. Pamoja na vitu vyote vingine, mwanadamu polepole na bila kujua anastawishwa na utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote vingine, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote.

11/04/2019

Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.