Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu. Onyesha machapisho yote

4/13/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mwenyezi mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesha ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea. Labda hii ni hali moja ambayo kwayo wanadamu hushirikiana na Mungu, ni ushirikiano usiokusudiwa wa mwanadamu na Mungu, ili utekelezaji huu unaoelekezwa na Mungu uwe wa kupendeza na wenye uhai, dhahiri sana.

4/11/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mwenyezi mungu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Utakatifu wa Mungu (III)

    Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Anatumia maarifa, sayansi, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii kutupotosha.) Sahihi, hii ndiyo ilikuwa mada kuu tuliyojadili wakati uliopita.

3/28/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Majina na Utambulisho

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Majina na Utambulisho

    Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Watu watakuuliza yote kuhusu Biblia, na Agano la Kale, na nini Yesu alisema na kufanya wakati huo. Watasema, “Mungu wenu hajawaeleza haya yote? Kama Yeye (Mungu) hawezi kuwaeleza ni nini hasa yanayoendelea kwa Biblia, basi Yeye si Mungu;kama Anaweza, basi tumeamini,” Mwanzoni, Yesu alizungumzia sana Agano la Kale na wanafunzi Wake. Kila kitu walichosoma kilitoka Agano la Kale;

3/27/2018

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,siku za mwisho 
 
    Mwenyezi Mungu alisema :"Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki kamwe mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo.

2/28/2018

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6) 

Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wanakuwa vuguvugu katika kuingia ambako Mungu anataka na wanabakia wenye shaka[1], kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili.

2/26/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu  

Je, ni vitu vipi vya asili ya mwanadamu? Unajua tu kuhusu upotovu wa mwanadamu, uasi, upungufu, dosari, fikra, na dhamira, lakini huwezi kugundua sehemu za ndani za asili ya mwanadamu—unafahamu tu safu ya nje, lakini huwezi kugundua chanzo chake. Baadhi hata hufikiri haya mambo ya juu kuwa ni asili ya mwanadamu, wakisema, “Tazama, ninaelewa asili ya mwanadamu; ninatambua ufidhuli wangu. Je, hiyo si asili ya mwandamu?” Je, haitoshi kuikubali kikanuni pekee? Ufidhuli ni kitu cha asili ya mwanadamu; huu ni ukweli kabisa. Je, kuelewa asili ya mtu binafsi ni nini? Inawezaje kujulikana? Je, inajulikana kutoka kwa vipengele vipi? Aidha, vitu hivi vinavyofichuliwa kutoka kwa vipengele hivi tofauti vinapaswaje kutazamwa kwa uthabiti? Tazama asili ya mtu kupitia shauku yake.

1/27/2018

Fumbo la Kupata Mwili (1)

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu. Haijalishi aina ya imani Yake kabla ya hii—labda wakati mwingine ilikuwa dhaifu, au wakati mwingine ilikuwa na nguvu—hayo ndiyo yalikuwa maisha Yake ya kawaida ya binadamu kabla Afanye huduma Yake.

12/19/2017

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Tafuta Ufalme wa Mungu Kwanza,imani katika Mungu

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu alisema, Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi amabayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi.

11/19/2017

Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Umeme wa Mashariki | Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi
Mwenyezi Mungu alisema, Watu huhisi kuwa wao wanaweza tu kubadilika katika maisha yao ya kanisani, na kuwa iwapo hawaishi ndani ya kanisa, mbadiliko hauwezekani, kuwa hawawezi kutimiza mbadiliko katika maisha yao halisi. Mwaweza kutambua suala hili ni lipi? Nimeongea juu ya kumleta Mungu katika maisha halisi, na hii ndiyo njia kwa wale wanaomwamini Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, maisha ya kanisa ni njia ndogo tu ya kuwakamilisha watu. Mazingira ya msingi ya kuwakamilisha wanadamu bado ni maisha halisi. Hiki ndicho kitendo halisi na mafunzo halisi Niliyozungumzia, yanayowaruhusu wanadamu kutimiza maisha ya ubinadamu wa kawaida na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli katika maisha ya kila siku. Kipengele kimoja ni kwamba mtu lazima aelimike ili kuinua kiwango chake mwenyewe cha elimu, aweze kuelewa maneno ya Mungu, na kutimiza uwezo wa kuelewa.

11/18/2017

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.

11/17/2017

Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu.

11/14/2017

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli
Umeme wa Mashariki | Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana. Mwanzoni, ni kwa kuzishika tu amri ndipo mwanadamu anaweza kuutenda ukweli na kufikia kuipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Lakini hii sio nia ya awali ya Mungu.

11/10/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (2)

                                          Fumbo la Kupata Mwili (2)

Mwenyezi Mungu alisema, Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi.

11/09/2017

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Umeme wa Mashariki | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Mwenyezi Mungu  alisema, Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

11/06/2017

Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu
Mwenyezi Mungu alisema, Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu. Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu. Kile ambacho Mungu hufanya kimeaminiwa kwako, uko radhi kutekeleza kile ambacho Mungu anataka kufanya, na hivi ndivyo inavyomaanisha kuuchukua mzigo wa Mungu kama wako. Wakati huu, kula na kunywa kwako maneno ya Mungu kutalenga masuala katika vipengele hivi, na utafikiri, nitayatatuaje masuala haya? Nitawaruhusu vipi ndugu kufunguliwa, wawe na furaha katika nafsi zao?

11/05/2017

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?

Umeme wa Mashariki | Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?
Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu.

11/03/2017

Umeme wa Mashariki | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Umeme wa Mashariki | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu
Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu.

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Mwenyezi Mungu alisema, Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake.

11/02/2017

Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu
Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kusalimika kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza dunia nzima.

11/01/2017

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Saa ya Giza Kabla ya Mapambazuko"



    Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Filamu hii ya hali halisi inaelezea uzoefu wa kweli wa Mkristo Mchina, Yang Huizhia, ambaye alikamatwa na serikali CCP, akateswa, na kufa kutokana na kuteswa kwake kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Baada ya Yang Huizhi kufa, serikali ya CCP kwa uongo ilidai kuwa kifo chake kilikuwa kimetokana na mshtuko wa moyo. Familia yake ilitaka kutafuta haki kwa ajili yake, lakini hatimaye walishtuka hadi kutulia kwa sababu ya vitisho vya CCP.