
Mwenyezi Mungu alisema, Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simmalizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wa nguvu wake, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya tu kazi Yangu, na kuongea kama Nimekuwa Nikifanya daima, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua Mimi ndani kabisa ya nyoyo zao, na watakuja kunikumbuka Mimi kwenye mawazo yao.





